Nimekutana na skin walker usiku wa kuamkia leo. Alikuwa binadamu, akageuka kuwa mbwa

poleni kwa taharuki hiyo kiongozi. nnachoweza kusema ni kweli mambo hayo yapo mimi pia nimeshwai kushuhudia tukio kama lako. kwa upande wangu lilikua hivi
Ilikua alfajiri mishale ya saa Tisa usiku, nyumba nzima tulikua tumetoka nje tukiwa tukipiga soga za hapa na pale baada ya vibaka/wezi kutaka kujaribu kuvunja kitasa cha mlango na kutuibia. Kipindi icho kulikua na shida ya maji mjini Dar es salaam ivyo wakina mama walikua wanajihimu asubui kwa ajili ya kuchota maji. Sisi nyumba yetu ilikua karibu kabisa na kisima ambacho kilikua kinasaidia jamii yote katika kitongoji chetu na kwakua tulikua karibia magereza wakati mwingine hata wafungwa waliongongozana na askari magereza kuja kupata maji eneo katika kisima hicho. Hivyo basi wakati tunaendelea kupiga soga juu ya mwizi alipita jirani yetu(mama Eva) akiwa amebeba ndoo zake za maji kuelekea kisimani na akatupa pole kwa kujarbiwa kuibiwa. wakati mama eva ameshapita maeneo ya nyumbani ghafla tulimuona akirudi mbio na kupiga yowee na sisi wote tukawa tunaangalia anapotokea mtu mzima nini kimemsibu. wakati mama eva anakaribia nyumba nyuma yake anapotokea kulimuona mtu akikatiza kutoka upande mmjo wa barabara kuvuka nakuingia nyumba ya jirani ambayo ipo upande mwingine wa barabara. Mama Eva break ya kwanza ikawa nyumbani ambapo sisi tumesimama tunamuuliza kulikoni ndo anasema 'nimemuona mtu sio mtu mbwa sio mbwa' maana yake aliona mbwa akijibadilisha kurudi katika umbo la kibinadamu. Sisi tuliamini maana kweli tuliona mtu nyuma yake akiambuka barabara na ile nyumba alioingia yule mtu, wenye nyumba walikua wakisifika kua ni Wachawi/Wanga wanaweza kubadilika kua Mbwa au hata Paka wakati mwingine.
 
Duniani Kuna mambo
 
Ungemtandika mtama mkuu, mbona kama alileta pigo sio.
 
Hapo uli Mix by Yas 😂😂😂 Ukapata Yas Magift kwa Angel wa Mbinguni
 
Duuh
 
 
Mitaa hiyo wala si ajabu, huyo aliwaacha mlikua wengi kaona kazi kuwabeba kaghairi.
Ungekuwa peke yako angesepa na wewe sa hizi.
Au wife ni mzito mkuu angalia hilo.
 
Sasa sisi barabarani tunaosafiri wenyewe usiku tunaona mengi na tukisimulia inaonekana kama hadithi za kutunga.....na hata hivyo kuna watu watabisha....
Mkuu habari ya uzima.

Huku malizia ile ya yule joka alikuwa na madini mkiani mlikutana nae maeneo ya Tabora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…