SawaHujui unachokiongea
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
SawaHujui unachokiongea
Sasa sisi barabarani tunaosafiri wenyewe usiku tunaona mengi na tukisimulia inaonekana kama hadithi za kutunga.....na hata hivyo kuna watu watabisha....Usiku wa kuamkia Leo, muda ya saa Saba usiku, nikiwa na mwanangu wa chuo kikuu cha UDSM, mke wangu, Binti wangu wa sekondari na mtoto wa kaka yangu tulikiwa tunatoka hotelini, tunalisogelea gari letu lililokuwepo maeneo ya maegesho ya Golden Tulip, Oyster Bay.
Mwanga wa eneo la maegesho tulikiwa mkali, tukiwa umbali WA kama meta kumi kutoka kwenye gari, tuliona mwanaume mwenye kama urefu wa futi SITA amesismama wima kwenye mlango wa nyuma wa gari yangu.
Wote tukiwa tumemkazia macho, alageuza pozi akawa kainama kama anafunga kamba za viatu, mara akageuka kuwa mbwa, na kutokomea. Wote tukapigwa na mshangao.
Mke wangu akaogopa kabisa hata kuingia kwenye gari, akawa anaogopa hata Sauti za mawimbi ya bahari.
Nikajaribu kumtuliza lakini kiwango chake cha taharuki kikawa juu sana, hadi walinzi ikabidi waje kujua kuna Nini?
Nikawaelezea tukio, wakabisha, wakasema twende kwenye CCTV camera kuangalia footage.
Basi wakaridisha video ya eneo like, na wenyewe wakaona hakika kilichotokea.
Tukajaribu kuomba copy ya kipande hicho cha video tumekataliwa.
Lakini hakika ukistaajabu ya Musa, utayaona ya uncle Firauni.
ChaiTukajaribu kuomba copy ya kipande hicho cha video tumekataliwa.
Mshangazi !Acheni pombe wewe na mkeo.
Ni bora mvute bangi
Maji yake yamegawanya kwenye chupa huwa yanauzwa na ukiyanywa kwa kiwango kikubwa yanakupa wenge ukiona mjusi unafikiri kenge na kenge unahisi Mamba hata mtu akiinama unafikiri mbwa!Dar Kuna ziwa Victoria?
Omba yasikukute....Acheni pombe wewe na mkeo.
Ni bora mvute bangi
Unajua macho ya binadamu hayana uwezo wa kuona baadhi ya vitu kutokana na sababu kadhaaa.....Haya mambo sikuwa nikiyaamini kabisa mpaka ile siku yaliponikuta ndo ulikuwa mwanzo wa mimi kuamini kuhusu hao viumbe 😣
huwa wanaonekana...hii kitu hata sayansi inakubali kutokana na mazingira..... frequency ...nanometers....pia ultra violet,,n.k.CCTV Haionyeshi hao viumbe ni uwongo
🤣🤣🤣🤣 ni mwendo wa dipresheni tu kila kona.
Wanaobisha ni watoto wamamaSasa sisi barabarani tunaosafiri wenyewe usiku tunaona mengi na tukisimulia inaonekana kama hadithi za kutunga.....na hata hivyo kuna watu watabisha....
Vitoto vya 2000s huwa ni vibishi sana na vikishapata degree basi wanajua wameimaliza dunia! Huwezi kuimaliza dunia halisi kwa karatasi (kusoma) ,tembea huko duniani ujionee!alivaa kanzu nyeupee na alipokaribia gari nikaona macho yake mekundu kama mkaa wa moto
Ulimwengu wa Giza ni dhahiriOmba yasikukute....
Kuna stori nilishaleta hapa kitambo,,,,,nilikuwa nasafiri peke yangu usiku kama saa nane hivi maeneo kati ya Kwedikwazu na Michungwani...nikakutana na mwanamke ananiomba lift sikusimama baada ya kuendelea umbali kadhaa nikamuona tena ananisimamisha...... ghafla gari ikaanza kukosa nguvu na kuzima hata hivyo niliwahi kulitoa nje ya barabara kuepusha madhara....wakati natafakari nini kimetokea nikaona mtu mrefu anakuja uelekea wa nilipo ni mrefu kuliko cabin ya SCANIA alivaa kanzu nyeupee na alipokaribia gari nikaona macho yake mekundu kama mkaa wa moto,,,nilipoteza fahamu,,,,kuja kushtuka ni saa mbili asubuhi wananiamsha madereva wenzangu marehemu Tembo na Ngilangwa hii ni baada ya kuitambua gari niliyokuwa nayo,,,,,haya maajabu yapo ...TEMBEA UONE>>>
inaonyesha vizuri sana CCTV hata ukifunga nyumbani kwako wale wachawi wanaoyeyuka na kutokea kwenye ukuta hayo yote utayaona..kitu ambacho akili yako fupi haikiamini au hujawai kushuhudia haimaanishi hicho kitu hakipo kwani uwezo wako wa akili na utambuzi ulipoishia basi wengine ndipo wanapoanzia.. fungua akili yako ujifunze usiyoyajua na sio yale tu unayojua ww na uliyokubaliana na akili yako eti ndio mwisho.!CCTV Haionyeshi hao viumbe ni uwongo
Ume research au unabisha tu kama hayawani?Camera irekodi jini? Mmhh hii chai umezidisha viungo