Nimekutana na skin walker usiku wa kuamkia leo. Alikuwa binadamu, akageuka kuwa mbwa

Nimekutana na skin walker usiku wa kuamkia leo. Alikuwa binadamu, akageuka kuwa mbwa

Mkuu habari ya uzima.

Huku malizia ile ya yule joka alikuwa na madini mkiani mlikutana nae maeneo ya Tabora.
NItamalizia ndugu yangu...nilisubiri upepo utulie kidogo katika ule ubishi wa ile mbuga na aina za wanyama.
 
Mimi ni mtu mkimya Sanaa...siku moja majira ya saa 7 mchana nilikatiza KATIKATI ya uwanja mkubwa shule moja ya serikali..

Uwanjani pale huwa Kuna MTI mmoja mkubwa sana ambao huwezi kuukumbatia...gafla akaonekana Binti kavalia HIJABU mpaka Chini nilipo geuka Mara ya pili nilimwona tukakutanisha macho ni mwanamke mzuri asiye mithilika (nikagundua sio KIUMBE wa kawaida)

Gafla tuka kutanisha macho nikamwangalia Chini mpaka juu miguu haionekani kashikilia mti ule mkubwa huku kanikazia macho tukaangalia Mimi nikaogopa sikumwangalia tenaa nikatembea fasta fasta mpaka nikaumaliza uwanja nilipo geuka Tena hakukua na mtu Tena kwenye ule mti.

Nikaondoka nikaenda kwenye sherehe TUMBO likaanza kuuma Nika harisha Sanaa nikapata homa Kali sanaa...siku hiyo nikawaza ikifika usiku itakuaje...nikaenda wanapo uza chair fire nikala kitimoto nikaomba mafutaa kwenye kichupa pia Nikachukua mifupa ya kitimoto nikawa natembea nayo mfukoni😊☺️

Nikachukua mavi makavu ya kitimoto nikaweka dirishani mlangoni kwa juu na kwenye kila Kona mlangoni pamoja na mifupa ya nguruwe pia nikawa kwenye mto naweka BIBLE

Baada ya hapo sikupata tenaa maluwe luwe ya jini yule..

Hii formula niliitumia mwaka mzima natembea na kipande Cha mifupa wa nguruwe

Acha tu baadae Nika achana na hiyo formula baada ya mwaka na ushee kupitaa
Siku niliyo shuhudia Jamaa yetu, aki chapwa Kofi na mtu asiye onekana ndo nili jua shit happen.
 
Usiku wa kuamkia Leo, muda ya saa Saba usiku, nikiwa na mwanangu wa chuo kikuu cha UDSM, mke wangu, Binti wangu wa sekondari na mtoto wa kaka yangu tulikiwa tunatoka hotelini, tunalisogelea gari letu lililokuwepo maeneo ya maegesho ya Golden Tulip, Oyster Bay.

Mwanga wa eneo la maegesho tulikiwa mkali, tukiwa umbali wa kama Meta kumi kutoka kwenye gari, tuliona mwanaume mwenye kama urefu wa futi SITA amesismama wima kwenye mlango wa nyuma wa gari yangu.

Wote tukiwa tumemkazia macho, alageuza pozi akawa kainama kama anafunga kamba za viatu, mara akageuka kuwa mbwa, na kutokomea. Wote tukapigwa na mshangao.

Mke wangu akaogopa kabisa hata kuingia kwenye gari, akawa anaogopa hata Sauti za mawimbi ya bahari.

Nikajaribu kumtuliza lakini kiwango chake cha taharuki kikawa juu sana, hadi walinzi ikabidi waje kujua kuna Nini?

Nikawaelezea tukio, wakabisha, wakasema twende kwenye CCTV camera kuangalia footage.

Basi wakaridisha video ya eneo like, na wenyewe wakaona hakika kilichotokea.

Tukajaribu kuomba copy ya kipande hicho cha video tumekataliwa.

Lakini hakika ukistaajabu ya Musa, utayaona ya uncle Firauni.
Hiyo kawaida sana mbona?
 
Back
Top Bottom