Nimekutana na Wanandoa wenye tarehe ya kuzaliwa inayofanana

Nimekutana na Wanandoa wenye tarehe ya kuzaliwa inayofanana

Tony Laurent

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2011
Posts
5,606
Reaction score
7,032
Siku kadhaa zilizopita, kuna wanandoa wawili walikuja kupata huduma ofisi ninayofanyia kazi. Katika huduma hiyo kuna fomu walitakiwa kujaza kila mmoja, na kulikuwa na k kipengele cha kuzaja tarehe ya kuzaliwa.

Baada ya kuzipitia fomu hizo, nilipofika kwenye kipengele cha tarehe ya kuzaliwa nikaona wote wamejaza tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa vikiwa vina fanana.

Nikafikiri, labda mmoja wao amekosea akajaza tarehe ya mwenza wake kwa bahati mbaya. Lakini walinihakikishia kuwa hawajakosea, vile walivyojaza ndivyo ilivyo.

Katika kuhakikisha juu ya jambo hilo walinionyesha na vyeti vyao vya kuzaliwa. Vyeti ambavyo walitengenezewa na wazazi wao wakati wao wakiwa bado wadogo.

Nilijaribu kufikiria kuwa huwenda vyeti hivi wangevishughulikia /kuvitengeneza wenyewe wakiwa watu wazima, labda wangeweza kuweka tarehe za kufanana ili kijitengenezea "coincidence"

Ukweli nilistaajabu.

Je, na wewe umewahi kukutana na "coincindence" ya aina hiyo? Au nyingine yoyote? Tushirikishe tafadhali.
 
Ajabu iliyonitokea kuna mwaka nilisafiri
Nikiwa lounge nikisubiri mda kuna mzee alikuwa amekaa karibu
Kwa mda ulikuwa ni mrefu sikuweza kusahau sura yake

Miaka miwili baadae sehemu ile tena nikalutana na yule mzee
Nilishtuka sana na kujiuliza je siku ziliganda? [emoji23][emoji23]
 
Rudi tena mkuu usijekuta ni sanamu
 
Back
Top Bottom