Nimekutana na Wanandoa wenye tarehe ya kuzaliwa inayofanana

Nimekutana na Wanandoa wenye tarehe ya kuzaliwa inayofanana

Hii huwa inatokea kwa mambo mengi sana. Binafsi imenitokea kwa mazingira matukio na matamshi

Nimewahi kuokota hela (sh mia) sehemu ileile kiasi kilekile mkao wake ardhini uleule safari ni ileile nilikuwa nikienda shule asubuhi asubuhi sana

Kwenye mazungumzo si mara moja unakuta tunazungumza jambo na washkaji lakini kuna vipande vya mazungumzo vinajirudia kwa namna ileile ya siku nyingine kabla

Nafikaga baadhi ya sehemu halafu nashangaa kukuta eneo fulani linafanana kila kitu na eneo lingine la nyumbani mfano nimewahi kwenda sehemu fulani nikakuta barabara fulani kama ya kwetu mbaya zaidi mpaka kwenye kona kulikuwa na kibanda cha mangi na penyewe nikakuta mtu kama yule yule japo walitofautiana kiasi fulani

Maajabu ya kujirudia yapo na yanashangaza sana
 
Siku kadhaa zilizopita, kuna wanandoa wawili walikuja kupata huduma ofisi ninayofanyia kazi. Katika huduma hiyo kuna fomu walitakiwa kujaza kila mmoja, na kulikuwa na k kipengele cha kuzaja tarehe ya kuzaliwa.

Baada ya kuzipitia fomu hizo, nilipofika kwenye kipengele cha tarehe ya kuzaliwa nikaona wote wamejaza tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa vikiwa vina fanana.

Nikafikiri, labda mmoja wao amekosea akajaza tarehe ya mwenza wake kwa bahati mbaya. Lakini walinihakikishia kuwa hawajakosea, vile walivyojaza ndivyo ilivyo.

Katika kuhakikisha juu ya jambo hilo walinionyesha na vyeti vyao vya kuzaliwa. Vyeti ambavyo walitengenezewa na wazazi wao wakati wao wakiwa bado wadogo.

Nilijaribu kufikiria kuwa huwenda vyeti hivi wangevishughulikia /kuvitengeneza wenyewe wakiwa watu wazima, labda wangeweza kuweka tarehe za kufanana ili kijitengenezea "coincidence"

Ukweli nilistaajabu.

Je, na wewe umewahi kukutana na "coincindence" ya aina hiyo? Au nyingine yoyote? Tushirikishe tafadhali.
Mimi na mume wangu tumefanana mwaka wa kuzaliwa ila mwezi na tarehe tumepisha siku 32 tu
 
Back
Top Bottom