Nimekutana na Watanzania waliosoma Ulaya, hawana kumbukumbu nyingi za social life, ni wengi wapo kama hawa?

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Kutokana na mazingira nayofanyia kazi zangu kuwa karibu na taasisi flani inayo husika na walengwa, nimeweza kujuana na baadhi yao waliosoma majuu sanasana wale wa ulaya ambao kwa sasa wapo Bongo.

Wengi wana mengi ya kushare hasa kwenye suala zima la elimu jinsi walivyoweza kupata sponsorship, kuchagua vyuo, kupata visa, n.k

Lakini kwenye Social life nje ya darasani wengi hawana mengi ya kushare, yani ile social life hasa ya vijana tunayopenda ya kuchangamana kwenda sehemu unacheza mpira au basketball, kudate watoto wa majuu, kwenda kwenye events kama matamasha, n.k.
 
Basi kosa ni la traffic wa angani ,sidhani Kama mapishi ya Nyama yanaweza kuunguza mchanga

Au Ni Simba wa yuda nahis Ni gori la offside na on-site

Basi hili nalo mkalitazame akina Kassim
 
Ukisikia tabia za Kiswahili moja wapo ni kama za huyu mtoa posti. Sasa mtu akwambie socia life lake huko nje ili iweje Kwa mfano. Acha umbea Fanya yako.

Unataka kumaanisha huko nje hao jamaa walikuwa wanaishi nje ya jamii? Kwenye jamii sehemu yeyote Ile kuna watu wanaopenda kujichanganya na wasiopenda kujichanganya.

Halafu usipendepende kufatilia maisha binafsi ya watu. Wamekuona ni zoba ndio maana hawajakusimulia.

Mtu yeyote mwenye akili zake timamu hawezi kushare hovyo personal life yake masual kama dating, outing etc ni private issues.
 
Wazungu wenyewe hawana mambo ya kuchangamana sana, mostly wanaishi in isolation. Kukiwa na get together event na yenyewe inapangiwa muda, nusu saa au saa moja kila mtu anatawanyika kivyake. Hizo bata za vigodoro hadi majogoo ni hukohuko ulimwengu wa tatu.
 

Umeona ehh
Mtoa posti hajui kama hao vija wako reserved maana nchi nyingi za ulaya zina condition ya “your reponsible for your own actions “
Alafu kuna laws chungu nzima ukikosea kidogo yaani utajamba cheche!
Msichana ukikaa naye vibaya umesha pigwa rape charges
Ukiendesha gari umelewa yaani ukikamatwa ni heri ungekaa nyumbani ukaacha masomo walahi [emoji35]
 
Wazungu wa nchi gani kaka??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…