Mzee Kitinku
Member
- Sep 23, 2026
- 54
- 191
Hii hadithi ya kufikisha ya binti mmoja anayeitwa "Angel"
Jana nikiwa hapa Jijini Mbeya kwenye shughuli zangu za kila siku nikakutana na Binti mmoja ambaye nimempa Jina la Angel.
Binti huyu alikuwa anazinguka mtaani akisajili line za simu kama njia Moja wapo ya kuzipata kipato chake Cha kila siku.
Katika maongezi yetu, alinisimulia mkasa wake kutokana na tukio la baada ya uchaguzi wa mwaka Jana. Binti huyu alieleza kuwa, yeye aliolewa na aliyekuwa marehemu mmewe na walibahatika kupata watoto wawili wa kiume. Mtoto Mkubwa ana miaka 4 na mdogo ana mwaka na miezi 6 sasa.
Anaeleza kuwa , waliishi vizuri na mmewe kwenye ndoa Yao na mme alikuwa ndio anapambana kwa ajili ya kuilisha na kuitunza familia yake iliyokuwa na amani na furaha.
Hadi ilipofikia TAREHE 30/10/2025 ndio maisha yalinadilika rasmi kwake na kwa watoto wake naye kuwa mjane akiwa na umri mdogo baada ya mmewe kuuawa kwa Risasi alipotoka nyumbani kwenda nje dukani kufuata majitaji Yao ya Kila siku.
Anasimulia, hakuamini aliposikia mlio wa Risasi na alipochungulia nje akamkuta mme wake akiwa amelala kwenye damu huku ubongo wake ukiwa umepasuliwa na kumwagika nje kutokana na kupigwa Risasi.
Anaendelea kuhadithia kuwa, ni picha na tukio linalomuumiza na kumtesa kila siku kwani bado picha ile ipo Moyoni make na hajui atalisahauje.
Maisha yakabadilika na haikuwa na jinsi na akiangalia ana watoto wawili wanamtegemea huku yeye akiwa ndio Baba Yao na mama Yao na sasa anapambana kwenye kusajili laini za simu ili apate ugali wa watoto wake.
Mungu amsaidie binti huyu. Ni story mrefu na ya kusikiyisha nimeamua kuifupisha.