puker
JF-Expert Member
- Nov 22, 2018
- 1,001
- 2,010
Habarini ndugu zangu. Niende Moja kwa Moja kwenye mada. Maisha ya mwanadamu ni mjumuisho wa vitu vingi sana, tunapambana Kila kukicha kuhakikisha tunakuwa Bora zaidi ya tulivyokuwa Jana.
Lakini kwa sasa kwangu hii imekuwa tofauti. Najua wengi tunapitia changamoto lakini tunapambana na kuzishinda.
Kwenye maisha yangu, nimekuwa nikipambana kama wafanyavyo wengine lakini changamoto ninazopitia kwa sasa hazihusiana kabisa na mali... Bali ni mahusiano kwa wanaonizunguka, nimekuwa mtu wa kuumizwa, kutopewa thamani na kusalitiwa kwa wale wote nilio waamini na kuwapenda.
Sina furaha Wala sioni tumaini, sioni umuhimu Tena wa Mimi kuwepo katika ulimwengu huu.
Maisha yangu mwenyewe yamekuwa ni maumivu tosha, nikiri wazi najichukia Mimi, historia yangu na Kila kitu kinachonizunguka, moyo wangu umekufa ganzi.. hauhisi chochote Tena.
Nimewahi kufikiria kujiua lakini naingiwa na hofu na uoga mkubwa sana, nakiogopa kifo.
Kitu ambacho naona kwangu ni nafuu na ninaweza kukifanya kikaniweka sawa katika hili.
Natamani kubadilisha Kila kitu kwenye maisha yangu, sio mali , nguo , ndugu marafiki na majamaa.
Yani kiufupi sihitaji kuwa na chochote kitakachonipa historia ya nyuma, hata Jina langu silihitaji Tena hata huu mwonekano wangu ubadilike natamani kwenda mbali sana Kila kitu kiwe kipya nianze upya nahisi Nitakuwa na Amani na nitapata nguvu ya kupambania furaha na ubora wangu Tena .
Sijui haya yote ni kwa namna Gani yanawezekana lakini natamani niache Kila kitu nitokomee mbali na nisionekane Tena kwenye Dunia yangu ya zamani.
Nawaombeni ushauri ndugu zangu nawezaje kulifanikisha hili.
Natangulisha shukrani🙏