Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Ushauri gani unataka wakati bado tamaa zimekujaa mpaka kwenye kope za macho? Rudisha nyumba yake, rudisha kodi zake na kila ulichopewa kwa makubaliano kuwa muwe wapenzi halafu muambie huyo kijana mwenzako akupe unavyopenda au mbaki na shida zenu ndio mfurahie hayo mapenzi yenu na kijana mwenzako.
Kingine chunguza sana huyo kijana huenda kakupenda kwa kuwa una gari, kazi nzuri na nyumba ulivyopewa na mume mwenzake.
Mwisho kabisa cha mtu hakiliwi bure.
 


Mimi nahisi unashindwa kuelewa kwamba jamaa anakuchukulia kama mke wake mpaka hapo na kwa hayo aliyoyafanya, nadhani ungejiandaa kisaikolojia kuwa mke wa pili tu.

Ina changamoto zake ila sidhani kama mtu mzima angewekeza kiasi hicho kwako bila kuwa na malengo na wewe. Fahamu kwamba mara nyingi mke wa pili anaanza kama mchepuko. Mtunuku jamaa mtoto, mpe ushirikiano uyaishi maisha yako.

Leo unampenda huyo kijana kwasababu umetengenezwa ukatengenezeka ila utakapoingia tu na kumuacha mumeo ndo utajua hujui.

Vijana ni wana mambo mengi sana na utapata msongo wa mawazo bure. Mimi nadiriki kusema inawezekana mahusiano yako na huyo kijana hata yasidumu.
 
Watu komenti kama hizi sijui hawazioni [emoji1787][emoji1787][emoji1787] au wewe Mama pretty ni mwanaume
 
Utavuna ulichopanda, ulipanda vya mume wa mtu utavuna vya mume wa mtu

Usifikiri alivyokufanyia ilikuwa ni favour, alifanya hivyo vitu ili akuweke ndani ya circle yake.

Kama wewe unajielewa na uthamini utu wako, usalama wako na heshima ya ndoa yake, hiyo nyumba mrudishie na hiyo gari mrudishie..na umwambie mapenzi yaishe..akizidi kukaza peleka shtaka polisi.


Usupomrudishia vitu vyake kwa kuwa vimekukolea, basi we ni mdangaji in nature pambana na hali yako..kama akikuua tutazika tu.

Kama unadhani nimetumia maneno makali, kumbuka ukali uliojiwekea.
 
Ni nani uliyeona amefurahia hili jambo hapa? Au umekuja kutema nyongo ulizotoka nazo kwa mkeo ndugu yangu?
Kejeli na kumkandia na kumtisha na kumkatisha tamaa hujaona hilo?
Mimi sina shida na wanawake hawanisumbui kwa lolote kiasi nikose amani kwa ajili yao!
Hio ilikua jana , leo yangu ni njema baada ya kuwajueni.
 
Rudisha vitu vyake vyote ,then acha hio kazi kaanzishe biashara kigamboni
 
Good kama umejutia..
 
Mpendwa wangu kama huna kikwazo cha kuolewa mke wa pili olewa tu maana huyo bwana anaonekana anakujali, unaweza kwenda kutafuta wa peke yako naye akawa na mambo yake ya ajabu au akakuletea wenzio yakawa yaleyale

Tatizo wote wakristo.
 

Asante sana.
 
Mwambie mpenzi wako mpya haya yote ajajuwe before. All the best

Nb nakuombea huko mbele huyo mpz mpyacasije badilika maana ni maumivu mara mbili.
 

Hivyo vitu vyake sina shida navyo naweza virudisha hata leo.

Mpenzi wangu hana shida maana ni mhudumiaji mzuri tu pia. Sijawahi muomba pesa ila huwa ananipa bila kuomba. Ni mtu anajali sana na ndio maana nimesema ndio aina ya mahusiano nahitaji kwa sasa.
 

Kuzaa na mume wa mtu tena? Dhambi ya kutembea nae tu inatosha.
 
Mnaoshaur amwambir mkewe kuna wengine sisi magaid nachepuka na mke anajua na cha kufanya hana
Mm mchepuko alienda kumfata wife akamwambia akitegemea tutaachana wife akamjibu " kakae utulie najua unatembea na mme wangu na akijua umenambia wewe atakupiga akuue [emoji23] katulie kabisa binti sitak matatizo"
Huyu dem baada ya kumuoa mke wa pili ndo akanambia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…