Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Habari wanajamii forum, ni matumaini yangu kuwa mko salama. Ama la, basi Mungu awafanyie wepesi.

Ndugu zangu nahitaji msaada wa mawazo yenu sana. Ninapitia sijui niseme ni wakati mgumu au ni ujinga wa kujitakia. Niko kwenye mahusiano na mume wa mtu sasa yapata miaka mitatu. Imefikia hatua nimechoka na nahitaji kujing’atua ila nakosa njia nzuri ya kuachana nae. Am not even proud with what i did so if you judge me i’ll understand.

Huyu mtu tangu nafahamiana nae ameyabadilisha sana maisha yangu maana ana mchango mkubwa sana. Alinisaidia kupata kazi nzuri na kuachana na kakazi kangu nilikokuwa nafanya, alinihamisha na kunipangishia sehemu nzuri zaidi. Baadae alininunulia gari nami nikawa natembea nimekaa, pia amenijengea nyumba iliyo kwa jina langu ila kwakuwa ipo nje ya mji nimeipangisha nakula kodi ila bado analipia kodi hapa ninapoishi.

Mahusiano yalipoanza sikufikiria hata yangechukua miezi 6, ila sasa ni miaka mitatu+. Ni mwanaume anayejali sana ila ana wivu balaa. Ni mara kadhaa amekuwa akinitishia kuwa akigundua ninamsaliti atanikata shingo. Sasa huwa najiuliza huyu ni mume wa mtu, anatarajia kweli niwe na yeye tu ili iweje?

Sasa nimechoka jamani, natamani niwe na mpenzi wangu na sio mume wa mtu. Kuna huyu kijana nimeanza nae mahusiano sasa ni miezi 5, kusema kweli nampenda na ninaona kabisa nae ananipenda. Haya ndio aina ya mahusiano niyatakayo. Nimekuwa nikitafuta visingizio kuwa asije kwangu maana sio maadili ila ukweli ni kuwa naogopa mlipa kodi akijua atanitoa roho.

Huyu mume wa mtu nishamtafutia visingizio ili tuachane ila inashindikana. Natamani yeye ndio aanze ili asije kuwa na kinyongo. Ila kuna wakati najipa moyo kuwa nimwambie tu tuachane lakini nikikumbuka aliwahi kunikunja nusura anipige alipokuta msg asizozielewa kwenye simu nahisi kutetemeka. Aliwahi kunionyesha silaha anayomiliki, nilipomuuliza ni ya nini akasema hata mimi nikimletea ujinga ananifyatua. Japo ulikuwa utani ila niliogopa kusema kweli.

Balaa zaidi recently ameanza kung’ang’ania nimzalie. Nimekuwa nikijifanya mimba hazishiki ila kusema kweli natumia dawa zisishike maana siko tayari kuzaa nae. Kwanza nahisi kama suffocation maana ananibana sana. Kwangu anakuja tu muda wowote akijisikia, na ole wangu asinikute nyumbani ni tatizo kubwa. Kila ninachofanya anahitaji apate taarifa kwanza, yaani kama mkewe vile jamani.

Nimejaribu kuelezea haya ili angalau muelewe ni kwanini nahitaji msaada wa mawazo yenu ili nijikwamue kwenye hili shimo nililojichimbia. Nipeni ushauri naachanaje na huyu mwanaume bila kuleta madhara kwangu.
Rudisha hiyo Nyumba aliyokujengea then anza kujilipia kodi mwenyewe..
 
Ujengewe nyumba
Gari ununuliwe..
Kazi nzuri utafutiwe ..


Halafu unasema anaku suffocate?

Tukusaidie umuache vipi?

Huyo Kijana umemwambia kuhusu kodi?


Why usirudishe nyumba na gari kwanza uone huyo Kijana mpya atakupenda vipi?

Ukiuliwa wala usimlaumu mtu
Huna akili
[emoji28][emoji28][emoji28] Anatafuta kifo kirahisi sana...!
 
Maneno mazur Sana Ayo luckyline[emoji4][emoji106]
Wewe nae anza kujiandaa😂😂 vip hujaanza kuwekeza kwa hao wapenzi wako?,mara mchepuko mara mdogo mtu, ka gegedo kako kako moto kweriiii kweriiiiy😂😂.

Sijui ndoa zina nini, kuna kaka alinambia kuwa mwanaume akitaka kufa mapema akose mchepuko. Eti ndoa ngumu.
 
Sasa unataka Jamaa akulipie kodi.

Huyo huyo Jamaa uendelee kutembelea gari lake.

Huyohuyo Jamaa,uendelee kula hela ya Kozi alojenga kwa jina lako.

Alafu kuja kwako umpangie mashariti???

HIVI MBONA MNAKUAGA WAPUMBAVU HIVO???


UKIULIWA INAKUAJE ????.



Haya basi katika kumchana ukweli, mwambie, Chukua Gari lako, Hela ya kodi ya nyumba yako hii hapa nanyumba chukua,


Rudisha kila KILICHO chake ,alafu uendelee nahako kajamaa kako.


Muwe MNAKUA na Akili basi.,,, Wakati Ana kutongoza hukujua ni Mume wa MTU??




Ulivyo FISI unataka Jamaa akuache, nanyumba pia, nagari ,viendelee kua kwako kwakua Tayari una kakazi kakupata hela yakula??.


NIAMIN..HAUNA AKILI HATA KIDOGO.
 
Wewe nae anza kujiandaa[emoji23][emoji23] vip hujaanza kuwekeza kwa hao wapenzi wako?,mara mchepuko mara mdogo mtu, ka gegedo kako kako moto kweriiii kweriiiiy[emoji23][emoji23].

Sijui ndoa zina nini, kuna kaka alinambia kuwa mwanaume akitaka kufa mapema akose mchepuko. Eti ndoa ngumu.
Sio uongo ndugu yangu ndoa ni ngumu kwa kiasi chake, naongelea hili nikiwa kama mhanga!
 
Yani wakati anakufanyia yote hayo upo umetulia unafraid,saizi unataka umbwage??
Kama uko serious kweli,mwambie umrudishie vitu vyake thenumuache.

Ndo mana now days uhalifu umezidi sababu ya mapenzi.
 
Ujengewe nyumba
Gari ununuliwe..
Kazi nzuri utafutiwe ..


Halafu unasema anaku suffocate?

Tukusaidie umuache vipi?

Huyo Kijana umemwambia kuhusu kodi?


Why usirudishe nyumba na gari kwanza uone huyo Kijana mpya atakupenda vipi?

Ukiuliwa wala usimlaumu mtu
Huna akili
Nakazia hapa
Tena ikiwezekana mchume mali kisha wekeza pembeni
Kisha jitoe
 
kwahiyo unamshauri dada wa watu kufa sio. Akifanya hivo ajue wazi kabisa anakufa muda wowote afanye na maandalizi tuu. Na sasaivi watu wanavouana ni hatare.
Hawezi kufa...

Anamtishia hivyo sababu anajua hajaolewa ila akiolewa hana mamlaka nae tena...
 
Yaani hapa suala la kuwa na kinyongo kwa kweli lazima ata ingekuwa wewe mtu ame invest time emotions na money and u exect asiwe na kinyongo.
Solution nyingine tafuta kazi nje ya nchi ama nenda kasome nje ya nchi huku ukimwachia hizo mali zote

Hii sio fair hata kidogo.
 
Ndo aina ya wanawake tulokua nao, shukran ya punda Ni mateke.

Ila Ni mwanaume mpumbavu pekee ndo atakayeruhusu huo upuuzi wake utokee[emoji4]
Wanawake nao sometimes wanapitia magumu, kuna rafiki yangu alikuwa na mme wa mtu wameachana juzi kwa mwenyekiti maana police ilishindikana.

Pia kabla ya police nilikuwa nasuluhisha kila siku.
Mme wa mtu alikuwa anamuhudumia hadi sisi tunaona wivu, sema huyu dada alitumia akili hakutaka kukubali kujengewa, sijui gari vyote alikwepa na kizuri mwanaume ndo alikuwa akija kwa dada, tuko fensi moja so hayo yote niliyaona kwa macho yangu.

Mimi nikamuita dada nikamuuliza mbona huyu mwanaume anakudekeza huduma zote anakupa hadi sisi majirani tunaona wivu nini shida, kwa nini unachepuka?

Huyo dada alilia akafunguka,

" mimi nimechoka ndani ya miaka 4 niko kifungoni na huyu baba nateseka mimi, hajawahi nifanyia chochote, hata shuka halijawahi lowa hata kidogo.

Usimuone huo urefu, kalea kitambi kadudu kamebaki kadogo sana, na mimi nilivyomnene kanaishia mapajani, nilikuwa namvumilia kwa sababu ananihudumia ila kwa sasa nimechoka.

Kuna biashara tuliwekeza wote namrudishia mtaji wake ila mimi siwezi tena, ana wivu, ananifata kazini, nikitoka out ananisaka mji mzima tukifika ndani hana anachonifanyia, nimechoka mimi, staki tena mgongo unaniuma , bado kunionea wivu kunipiga na mkanda, staki mimi akapiga ukunga."

Dada alivyoenda police wakasema hawataki kesi za wapenzi, akaenda kwa mwenyekiti wakaita wajumbe, mwanaume akasema hawezi kumwacha kirahisi eti kawekeza
kwake, dada kasema hela yote ya mtaji nitampa ila tuachane nipumue.mwanaume akagoma.

Kwenye huo mgogoro mwanaume alitoa vitisho vya kumuua dada kwa sms akaituma kwa mama dada,so siku hiyo kwa mwenyekiti dada kaonesha hiyo sms. Dada kamwambia mwenyekiti kuwa huyo mwanaume atamuua wagawame walichowekeza mbele ya mwenyekiti.mwanaume kagoma.

hiyo ishu ya kushindwa kufanya kazi kitandani hakuisema kwa mwenyekiti.

Sasa mwenyekiti akaamua kuwa mwanaume aondoke pale maana dada alikuwaga akipanga hapo before.aondoke hapo arudi kwake mpaka baada ya wiki. Wakirudi kila mtu aje na anachodai wakabidhiane kwa mwenyekiti.

Dada kaomba asindikizwe mwanaume atowe vitu vyake, maana na ufunguo mwanaume alizigomea dada akawa analala hotelini. Walipofika ndani akatoa vitu kiduchu nguo zote zikabaki, dada kasema avumilie mpaka huo muda waachane kwa amani.

Dada kamwambia mlinzi asiruhusu kuingia getini, lakini pia mwenyekiti aliandika barua ya kumtaka mwanaume asikanyage hapa mpaka siku walopewa kupata suluhu.

Mwanaume akaondoka, wakaanza jibizana kwenye simu mdada kamwambia alivyonchoka gegedo halifanyi kazi, mwanaume akasala kuwa kapata mabwana wengine, ni kweli dada alikuwa kapata mtu.

Baada ya wiki mwanaume hakurudi kwa mwenyekiti, dada akaandaa mtaji alopewa akapeleka kwa mwenyekiti, wakamsubiri mwanaume hakuja hadi leo.

Dada katoa nguo za mwanaume kaziweka kwenye salufeti ziko hapo coridoni. Ni mwezi sasa mwanaume hajarudi. Tunasikia alienda kwa mganga amroge asiachike.

Nb huyu mwanaume ana familia yake mkewe waliachana anaishi na wanae tu. Mwanaume alitaka amuoe huyu dada akagoma akawa akimpotezea coz alijua hawez ingia nae ndoa.

Za chini chini zinasema mke wa huyu mwanaume aliondoka sababu ya mapungufu ya kitandani ya mwanaume, kwamba siku moja alizidiwa akachepuka alipigwa akaondoka ndani yupo uchi hadi leo hajawahi rudi.

Mwanaume kosa vingine ila sio nguvu za kiume

So mleta mada kuwa makini rudisha kila kitu ishi maisha yako.
 
Mimi pia na mke mdogo( enzi alikuwa mchepuko akisoma chuo nikampangia na kumpa gari na biashara alipomaliza chuo nikamjengea then et anataka aniache nilimfata mamake nikamwambia nitawaua ukoo mzima)
Wakat natoa hela mtoto anasoma na kuishi vzr dar why hawakumzuia sahiz ndo wanawaza aolewe? Never
Ilibid waongee nae vzr akakubali nikamuoa mke wa pili ndo kesi ikaisha
Hii ba ngoosha !!!! Yan haya maswala hata kama roho ya kishetani huna inajiapload yenyewe, ye binti aombe ndoa kwa uyo kiongozi, ila ingekuwa kule ucgagani machame bibie angemtanguliza mbele za haki jamaa chapu tu
 
Back
Top Bottom