Wee bwana huyu mrembo wa mjini kazoea raha za huku mujini huko kwengine ataona shida tuuHapana, sijipigii pasi. Ni utani tu, anaweza kwenda popote na inaonesha ni mzoefu wa kusafiri. Kama anaishi Arusha akienda kujificha Mtwara au Songea au hata Mbeya ataishi kwa amani. Siwezi kumshauri Kubaki sehemu ambayo haridhiki.
Hapana amechoka kuwa mtumwa na anahitaji kuwa huru na mtu atakayelala na kuamka naye. So Ms Saaly sell the house Tena hakikisha kuanzia dalali mpaka mnunuzi wawe ni wageni maeneo hayo wasije vujisha kwa Mzee baba ukalambwa Shaba. The day umepata malipo ndipo acha kazi Ile ya masaa 24.
On the same day or the day after, get away leaving everything else behind including your dear friends, I mean everything; car, contacts, some personal belongings. Tanzania ni kubwa hii na Africa ni Moja. If you will pocket 20m it's enough to start afresh somewhere else in Tz or EAC.
Wapenzi kuuana ni real, take care.
Ukishauza niambie nikufiche!!
Sahii kabisa,
Hizo Ni mbwembwe za penzi jipya kwasababu anajua mwanamke wa class ya juu asionekane marioo
Ila uwezo wa kuhudumia Kama mwanzo ndo asahau kabisa[emoji4]
Mtafute instagram na facebook kwa jina la Idi makengo,atakupa utaratibu utaongea nae.Nampata wapi?
Hebu acheni hayo mambo bwana, nae bidada arudishiwe vyake na muda wake alioupoteza kwa jamaa basi.
Mimi nakuambia, utapata maushauri mengi hapa, ila ushauri ambao hautakudhuru ni huu, maana yatayeye atakuona mzembe na ataona kama vile yeye ndo kakuacha, pia na mali zake ataona hauko nazo umezipoteza, kumbe akili nyingi.
Sent from my itel P32 using JamiiForums mobile app
Basi kama na huyu wa huyu yupo kama wewe,hapo utata!
Ni kweli mtu akijiona 'mnyonge' basi anaenda kutafuta 'nguvu' popote zinapopatikanaNiliwahi kumuuliza hivi mkeo akijua itakuwaje? Akaniambia akijua ndio vizuri ili tusifiche fiche sasa maana hana cha kufanya. Tatizo moyo wa mtu kichaka, sio wanawake wote ni wanyonge unaweza pigwa tukio la hatari.
Hawa viumbe ni wabinafsi sana ni wa kuishi nao kwa akili sana. Kuna mdau kasema hapo chukua mkopo then jifanye huwezi kuulipa ili akuone duwanzi akuache. Nami naungana nae maana naona kama ukilianzisha wewe utapigwa na kitu kizito.Wanavyosema ni kama mimi sina ninachopoteza katika hili.
Sasa kwa yote hayo alokufanyia mbona tayari ni mumeo!? Hapana mie sikushauri umuache unaweza pata laana! Hapo tafteni tu namna muyarasmishe hayo mahusiano na uhesabike ni mke mdogo!Habari wanajamii forum, ni matumaini yangu kuwa mko salama. Ama la, basi Mungu awafanyie wepesi.
Ndugu zangu nahitaji msaada wa mawazo yenu sana. Ninapitia sijui niseme ni wakati mgumu au ni ujinga wa kujitakia. Niko kwenye mahusiano na mume wa mtu sasa yapata miaka mitatu. Imefikia hatua nimechoka na nahitaji kujing’atua ila nakosa njia nzuri ya kuachana nae. Am not even proud with what i did so if you judge me i’ll understand.
Huyu mtu tangu nafahamiana nae ameyabadilisha sana maisha yangu maana ana mchango mkubwa sana. Alinisaidia kupata kazi nzuri na kuachana na kakazi kangu nilikokuwa nafanya, alinihamisha na kunipangishia sehemu nzuri zaidi. Baadae alininunulia gari nami nikawa natembea nimekaa, pia amenijengea nyumba iliyo kwa jina langu ila kwakuwa ipo nje ya mji nimeipangisha nakula kodi ila bado analipia kodi hapa ninapoishi.
Mahusiano yalipoanza sikufikiria hata yangechukua miezi 6, ila sasa ni miaka mitatu+. Ni mwanaume anayejali sana ila ana wivu balaa. Ni mara kadhaa amekuwa akinitishia kuwa akigundua ninamsaliti atanikata shingo. Sasa huwa najiuliza huyu ni mume wa mtu, anatarajia kweli niwe na yeye tu ili iweje?
Sasa nimechoka jamani, natamani niwe na mpenzi wangu na sio mume wa mtu. Kuna huyu kijana nimeanza nae mahusiano sasa ni miezi 5, kusema kweli nampenda na ninaona kabisa nae ananipenda. Haya ndio aina ya mahusiano niyatakayo. Nimekuwa nikitafuta visingizio kuwa asije kwangu maana sio maadili ila ukweli ni kuwa naogopa mlipa kodi akijua atanitoa roho.
Huyu mume wa mtu nishamtafutia visingizio ili tuachane ila inashindikana. Natamani yeye ndio aanze ili asije kuwa na kinyongo. Ila kuna wakati najipa moyo kuwa nimwambie tu tuachane lakini nikikumbuka aliwahi kunikunja nusura anipige alipokuta msg asizozielewa kwenye simu nahisi kutetemeka. Aliwahi kunionyesha silaha anayomiliki, nilipomuuliza ni ya nini akasema hata mimi nikimletea ujinga ananifyatua. Japo ulikuwa utani ila niliogopa kusema kweli.
Balaa zaidi recently ameanza kung’ang’ania nimzalie. Nimekuwa nikijifanya mimba hazishiki ila kusema kweli natumia dawa zisishike maana siko tayari kuzaa nae. Kwanza nahisi kama suffocation maana ananibana sana. Kwangu anakuja tu muda wowote akijisikia, na ole wangu asinikute nyumbani ni tatizo kubwa. Kila ninachofanya anahitaji apate taarifa kwanza, yaani kama mkewe vile jamani.
Nimejaribu kuelezea haya ili angalau muelewe ni kwanini nahitaji msaada wa mawazo yenu ili nijikwamue kwenye hili shimo nililojichimbia. Nipeni ushauri naachanaje na huyu mwanaume bila kuleta madhara kwangu.
Yeah uko sahihi mkuu. Huenda jamaa anatamani amuoe ila anashindwa kutokana na tabia zake.Kuoa Ni mchakato mkuu,
Kama Anatabia mbovumbovu Ni mwanaume gani mpumbavu atathubutu kuweka ndani Moja kwa moja.
Mtafute instagram na facebook kwa jina la Idi makengo,atakupa utaratibu utaongea nae.
Na pia utasoma mikasa ya watu wengine naamini utajifunza pia.
Ngoja tuongeze sauti basi,Wapendwa badala mnipe ushauri mnaniongezea magazijuto kweli? Najua i messed up big time and an not proud. Nisaidieni najikwamuaje hapa.
Ushauri mzuri ila mleta mada hajasema kuwa hampendi ila shida iliyopo ni kwasababu ya kuwa kwenye mahusiano na Mume wa mtu.Gunia 4 za mkaa zinakuhusu wewe
PS. Kaa nae umueleze ukweli juu ya maamuzi yako na sio uamue tu kumuacha. Najua unahofia anaweza kukunyanganya materials alizokupa! Bora umwambie kuhusu future yako ili yeye aamue kukuacha na achukue mali au akuachie AU akufanye mke wa pili....Wengi tu wameolewa na watu wasiowapenda
Hayo ndio madhara ya kumpenda mtu kutokana na Status/materials aliyonayo na sio kutoka ndani ya Roho yako🚶🚶🚶
Sasa kwa yote hayo alokufanyia mbona tayari ni mumeo!? Hapana mie sikushauri umuache unaweza pata laana! Hapo tafteni tu namna muyarasmishe hayo mahusiano na uhesabike ni mke mdogo!
nina hakika hata ukipata mume huyo jamaa hutaachana nae, mtaachana kwa muda tu!
Mfalme Sulemani alikuwa na wake wangapi? Yeye hakuwa na dini? Mfalme Daudi alikuwa na wake wangapi? Yeye hakuwa na dini? Haya, Ibrahimu ambaye wewe mwenyewe unamuita baba wa Imani alikuwa na wake wangapi? Yeye hakuwa na dini? Au wewe Mungu wako ni bora zaidi ya Mungu wa Ibrahimu, Yacobo na Isaka?Dini hairuhusu mke wa pili.
Hebu muelekeze anaanzaje anzaje???Tafuta namba ya mke wake kajisemee