Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

1: uko tiyari kuachia nyumba?
2: uko tiyari kuachia gari?
3: uko tiyari kuikosa hiyo kazi?
4;hako ka serengeti boy kana chochote au kamekupendea mali za jamaa?

Kama yote hayo uko tiyari muweke wazi ondoka bila chochote.

Ila nakuhakikishia hako ka serengeti baada ya miezi 2 tu katakuacha maana hutokuwa na chochote.

Kuanzia hapo utakuwa nagundu hata mme wa kukuoa hutompata.

Utaishia kulala na vitoto ambavyo unavizidi umri, na vitakuzalisha vikutekeleze.

Mimi nimekuelewa ila ujinga uloufanya ni kumruhusu akawekeza kwako wakati humpendi.

Dada kuna siku utapauka utakumbuka hii comment. Unakwenda kukosa kila kitu kisa hicho kivulana ulichokipata na wenda hakina kitu labda smartphone na laptop.

Dada duniani huwezi pata vyote, bora ukose upendo lakini unahudumiwa.

Nani kakudanganya hako kavulana katakupa raha kuliko huyo baba?

Ondoka ila jiandae kupauka, nimeona walofanya kama wewe wanatamani kurudisha siku nyuma.

Ukipenda jibu maswali hapo juu.

Ni heri kwake aachie vyote vya bwanaake, aondoke hana ki2. Muhimu uhai wake
 
Yaani ningekuwa na uhakika kuwa nikivirudusha basi tutaachana kwa amani ningevirudisha tangu jana. Ila kuna kauli zake tata amekuwa akiziongea tangu nilipoanza kumwambia wazazi wanataka niolewe ndizo zinanipa wasiwasi.
simamia msimamo wako ukimaliza kumrudishia vitu vyake nenda kituo cha polisi toa taarifa na hata siku moja asikuite muonane eti tuongee au kufanya urafiki maana haya ni maisha yako ukiendeea kuishi kama hivi mpaka lini??
 
Thread Tele Humu Watu Wanakufa Kisa Mapenzi Nawe Umeanza
Rudisha
Gari Alilokununulia
Nyumba Aliyokujengea
Kodi Anayolipa

Halafu Huyo Unayempenda Mkaanze Upya
Hapo Umenasa Mwenyewe, Huna Namna
Exactly niliwaza hvyo hvyo arudishe hvyo vitu vyote akaanze upya kuya jenga
 
Habari wanajamii forum, ni matumaini yangu kuwa mko salama. Ama la, basi Mungu awafanyie wepesi.

Ndugu zangu nahitaji msaada wa mawazo yenu sana. Ninapitia sijui niseme ni wakati mgumu au ni ujinga wa kujitakia. Niko kwenye mahusiano na mume wa mtu sasa yapata miaka mitatu. Imefikia hatua nimechoka na nahitaji kujing’atua ila nakosa njia nzuri ya kuachana nae. Am not even proud with what i did so if you judge me i’ll understand.

Huyu mtu tangu nafahamiana nae ameyabadilisha sana maisha yangu maana ana mchango mkubwa sana. Alinisaidia kupata kazi nzuri na kuachana na kakazi kangu nilikokuwa nafanya, alinihamisha na kunipangishia sehemu nzuri zaidi. Baadae alininunulia gari nami nikawa natembea nimekaa, pia amenijengea nyumba iliyo kwa jina langu ila kwakuwa ipo nje ya mji nimeipangisha nakula kodi ila bado analipia kodi hapa ninapoishi.

Mahusiano yalipoanza sikufikiria hata yangechukua miezi 6, ila sasa ni miaka mitatu+. Ni mwanaume anayejali sana ila ana wivu balaa. Ni mara kadhaa amekuwa akinitishia kuwa akigundua ninamsaliti atanikata shingo. Sasa huwa najiuliza huyu ni mume wa mtu, anatarajia kweli niwe na yeye tu ili iweje?

Sasa nimechoka jamani, natamani niwe na mpenzi wangu na sio mume wa mtu. Kuna huyu kijana nimeanza nae mahusiano sasa ni miezi 5, kusema kweli nampenda na ninaona kabisa nae ananipenda. Haya ndio aina ya mahusiano niyatakayo. Nimekuwa nikitafuta visingizio kuwa asije kwangu maana sio maadili ila ukweli ni kuwa naogopa mlipa kodi akijua atanitoa roho.

Huyu mume wa mtu nishamtafutia visingizio ili tuachane ila inashindikana. Natamani yeye ndio aanze ili asije kuwa na kinyongo. Ila kuna wakati najipa moyo kuwa nimwambie tu tuachane lakini nikikumbuka aliwahi kunikunja nusura anipige alipokuta msg asizozielewa kwenye simu nahisi kutetemeka. Aliwahi kunionyesha silaha anayomiliki, nilipomuuliza ni ya nini akasema hata mimi nikimletea ujinga ananifyatua. Japo ulikuwa utani ila niliogopa kusema kweli.

Balaa zaidi recently ameanza kung’ang’ania nimzalie. Nimekuwa nikijifanya mimba hazishiki ila kusema kweli natumia dawa zisishike maana siko tayari kuzaa nae. Kwanza nahisi kama suffocation maana ananibana sana. Kwangu anakuja tu muda wowote akijisikia, na ole wangu asinikute nyumbani ni tatizo kubwa. Kila ninachofanya anahitaji apate taarifa kwanza, yaani kama mkewe vile jamani.

Nimejaribu kuelezea haya ili angalau muelewe ni kwanini nahitaji msaada wa mawazo yenu ili nijikwamue kwenye hili shimo nililojichimbia. Nipeni ushauri naachanaje na huyu mwanaume bila kuleta madhara kwangu.
Haya DeepPond uje utolee ufafanuzi tu mkuu naona yule malaya kaja kukuanzishia uzi!
 
Mwisho wa siku inakuja kutokea kama ya mleta mada!
Kwa ufupi Mwanamke changamoto zake ni kubwa sana, unaweza kusema unakwepa hili kwa Mwanamke huyu unaenda kukutana na lingine gumu kwa Mwanamke yule.
Tuseme tu mmeturahisishia sana wanaume kutangulia mbele za haki kwa kweli
bro kama ni hivo si utulie tu nahuyo ulienae kinachokupeleka nje ya ndoa ninini ? Baki njia kuu
 
Kuna kitu kipo ndani yetu wanaume ambacho hamnacho nyie wanawake nacho ni kupenda.
Tunauwezo wa kupenda Mwanamke zaidi ya mmoja na kuheshimu wote kwa nafasi zao.
Kwenu wanawake ni changamoto kidogo kuwa na upendo kwa wanaume wawili.

Sisi tunaweza kutamani ukajua tumependa kumbe la!
Tunaweza kupenda ukajua tumetamani.
Kipimo cha mwanaume anayependa ni ile kujali na kuhudumia, fikiri mtu ama make na pengine ana familia lakini bado amejitoa kukujali na kukuhudumia na kukulinda.
Hapo hajakutamani bali amekupenda.

Na kama unavyojua maswala ya kupenda huenda mpaka ndani ya moyo na nafsi na akili na matokeo huonekana kwenye mwili.

Sasa mtu kama huyo kumtoka sio rahisi sana maana mchakato wake ni kuanzia ndani ya nafsi mpaka aje akubali atakua amesumbuka sana na pengine kupoteza vingi wakati akichakata kuondoka kwake moyoni mwake.

Kwa sisi wengine tunaweza kuvumilia kipindi kigumu kama hiko kwa tumaini ya kwamba yatapita tu lakini tutabakiwa na majereha makubwa sana moyoni.

Wengine kwa kweli hawana uwezo wa kuvumilia hali hiyo, wanafanya maamuzi magumu yenye gharama kubwa mpaka ya uhai, na vile umesema ana bunduki, jiadhari sana.


Unaweza ukafanya jambo hilo bila athari kubwa iwapo unatumia busara na akili kubwa na hoja za nguvu.

Kuna dawati la jinsia,kuna viongozi wa dini, kuna wanasheria,kuna watu wa heshima kwako na kwake, na pia nyie wawili mkikaa mkiambina ukweli naamini kabisa mtafika mwafaka ulio bora.

Binafsi nakuombea na kukutakia yote mema,naamini kidogo unapitia pagumu lakini wakati mmoja utafika na utakuwa na heri na furaha na amani.
mkuu ikumbukwe uliapa kumpenda mkeo kwa hali yoyote ile sasa iweje leo ukereke na hali yake utoke nje ya ndoa??
Naamiini unafuatilia Sana misingejanhaika ya dini sasa unakwama Wapi mpaka unamcheat mkeo na kupoteza resources kibao ambazo ungeipatia/ ungeihudumia familia yako unapoteza kwa hawara wa nje??
unafiki katika ndoa utatupeleka pabaya sana wanandoa!
 
Ni kweli wanatofautiana na mchepuko kiuwezo lakini yeye sio mnyonge kama mnavyomfikiria. Ni mtu namfahamu vizuri tu kwa muda sasa. Labda apretend kuhusu kunipenda ila kuhusu mali anazo zake na ni mpambanaji sana.
Kua na Mali Ni suala jingine, na moyo wa kuhudumia Ni suala jingine.

Kuna Watu wanamali Sana ila Ni mabahili Hadi kwenye afya zao wenyewe.

Muda always Ni mwamuz mzur[emoji4]
 
Back
Top Bottom