Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Habari wanajamii forum, ni matumaini yangu kuwa mko salama. Ama la, basi Mungu awafanyie wepesi.

Ndugu zangu nahitaji msaada wa mawazo yenu sana. Ninapitia sijui niseme ni wakati mgumu au ni ujinga wa kujitakia. Niko kwenye mahusiano na mume wa mtu sasa yapata miaka mitatu. Imefikia hatua nimechoka na nahitaji kujing’atua ila nakosa njia nzuri ya kuachana nae. Am not even proud with what i did so if you judge me i’ll understand.

Huyu mtu tangu nafahamiana nae ameyabadilisha sana maisha yangu maana ana mchango mkubwa sana. Alinisaidia kupata kazi nzuri na kuachana na kakazi kangu nilikokuwa nafanya, alinihamisha na kunipangishia sehemu nzuri zaidi. Baadae alininunulia gari nami nikawa natembea nimekaa, pia amenijengea nyumba iliyo kwa jina langu ila kwakuwa ipo nje ya mji nimeipangisha nakula kodi ila bado analipia kodi hapa ninapoishi.

Mahusiano yalipoanza sikufikiria hata yangechukua miezi 6, ila sasa ni miaka mitatu+. Ni mwanaume anayejali sana ila ana wivu balaa. Ni mara kadhaa amekuwa akinitishia kuwa akigundua ninamsaliti atanikata shingo. Sasa huwa najiuliza huyu ni mume wa mtu, anatarajia kweli niwe na yeye tu ili iweje?

Sasa nimechoka jamani, natamani niwe na mpenzi wangu na sio mume wa mtu. Kuna huyu kijana nimeanza nae mahusiano sasa ni miezi 5, kusema kweli nampenda na ninaona kabisa nae ananipenda. Haya ndio aina ya mahusiano niyatakayo. Nimekuwa nikitafuta visingizio kuwa asije kwangu maana sio maadili ila ukweli ni kuwa naogopa mlipa kodi akijua atanitoa roho.

Huyu mume wa mtu nishamtafutia visingizio ili tuachane ila inashindikana. Natamani yeye ndio aanze ili asije kuwa na kinyongo. Ila kuna wakati najipa moyo kuwa nimwambie tu tuachane lakini nikikumbuka aliwahi kunikunja nusura anipige alipokuta msg asizozielewa kwenye simu nahisi kutetemeka. Aliwahi kunionyesha silaha anayomiliki, nilipomuuliza ni ya nini akasema hata mimi nikimletea ujinga ananifyatua. Japo ulikuwa utani ila niliogopa kusema kweli.

Balaa zaidi recently ameanza kung’ang’ania nimzalie. Nimekuwa nikijifanya mimba hazishiki ila kusema kweli natumia dawa zisishike maana siko tayari kuzaa nae. Kwanza nahisi kama suffocation maana ananibana sana. Kwangu anakuja tu muda wowote akijisikia, na ole wangu asinikute nyumbani ni tatizo kubwa. Kila ninachofanya anahitaji apate taarifa kwanza, yaani kama mkewe vile jamani.

Nimejaribu kuelezea haya ili angalau muelewe ni kwanini nahitaji msaada wa mawazo yenu ili nijikwamue kwenye hili shimo nililojichimbia. Nipeni ushauri naachanaje na huyu mwanaume bila kuleta madhara kwangu.
Kwa mimi navojijua nikifanyiwa hivyo naua. Na huyo hawara yako kakupa favour zote hizo alafu umkimbie tu kirahisi hivyo ..ukishamuacha yeye na mali zake karipoti polisi uombe ulinzi
 
Holy spirit
 
Mkuu DeepPond kama tafadhari muache kwa amani binti wa watu, ona anavopata shida jaman daaah.

We binti tamaa zimekuponza, pole sana.
Watu wa hivo ni kweli ukimzingua hataona shida kukupoteza na unahatarisha maisha ya hako kamjaa kako pia akijua atakafyatua kweli.

Ushauri mzuri ni kukomaa na hiyo style yako coz kila kitu kakupa yeye hapo ulipo hata uhai wako kaushikilia sasa.

Kama una ujasiri mwambie unatamani kuitwa mke, walau basi akuoe mke wa pili. Lakini kama unajiamin zaid mwambie akuruhusu uolewe ila mahusiano yenu yataendelea kama kawaida kwasababu huko nampwilimbwinde kwenu wazaz wanasumbua wanataka ndoa na wajukuu uwapatie ndoani na sio kuzaa tu bila ndoa.
 
Mimi pia na mke mdogo( enzi alikuwa mchepuko akisoma chuo nikampangia na kumpa gari na biashara alipomaliza chuo nikamjengea then et anataka aniache nilimfata mamake nikamwambia nitawaua ukoo mzima)
Wakat natoa hela mtoto anasoma na kuishi vzr dar why hawakumzuia sahiz ndo wanawaza aolewe? Never
Ilibid waongee nae vzr akakubali nikamuoa mke wa pili ndo kesi ikaisha
 
Kuna wakati huwa nafikiria kumrudishia gari na hati ya nyumba na viwanja alivyoninunulia kisha nimwambie tuachane. Ila nahofu atavipokea bila kinyongo?

BTW Sina hata huo uzuri na hilo tako unalofikiria ninalo. Ni wa kawaida sana.
Kama unaweza tafuta no ya uyo mke wake alafu umtumie pics zenu( wewe pamoja na mmewe) kwa kutumia new no afu usikilizie 🤣🤣🤣🤣
 
Mkuu DeepPond kama tafadhari muache kwa amani binti wa watu, ona anavopata shida jaman daaah.

We binti tamaa zimekuponza, pole sana.
Watu wa hivo ni kweli ukimzingua hataona shida kukupoteza na unahatarisha maisha ya hako kamjaa kako pia akijua atakafyatua kweli.

Ushauri mzuri ni kukomaa na hiyo style yako coz kila kitu kakupa yeye hapo ulipo hata uhai wako kaushikilia sasa.

Kama una ujasiri mwambie unatamani kuitwa mke, walau basi akuoe mke wa pili. Lakini kama unajiamin zaid mwambie akuruhusu uolewe ila mahusiano yenu yataendelea kama kawaida kwasababu huko nampwilimbwinde kwenu wazaz wanasumbua wanataka ndoa na wajukuu uwapatie ndoani na sio kuzaa tu bila ndoa.
Duh![emoji848]
 
Mimi pia na mke mdogo( enzi alikuwa mchepuko akisoma chuo nikampangia na kumpa gari na biashara alipomaliza chuo nikamjengea then et anataka aniache nilimfata mamake nikamwambia nitawaua ukoo mzima)
Wakat natoa hela mtoto anasoma na kuishi vzr dar why hawakumzuia sahiz ndo wanawaza aolewe? Never
Ilibid waongee nae vzr akakubali nikamuoa mke wa pili ndo kesi ikaisha
Daah mzee umetisha sana🙌🏽🙌🏽Kwahyo ulitaka kufyeka familia nzima
 
Kwenye nyumba na gari hapo pagumu Sana kupotezea ila kazi kidogo binafsi ningeweza kusamehe, ushauri wangu rudisha nyumba na gari baada ya hapo muombe muachane ili uanze upya
 
Habari wanajamii forum, ni matumaini yangu kuwa mko salama. Ama la, basi Mungu awafanyie wepesi.

Ndugu zangu nahitaji msaada wa mawazo yenu sana. Ninapitia sijui niseme ni wakati mgumu au ni ujinga wa kujitakia. Niko kwenye mahusiano na mume wa mtu sasa yapata miaka mitatu. Imefikia hatua nimechoka na nahitaji kujing’atua ila nakosa njia nzuri ya kuachana nae. Am not even proud with what i did so if you judge me i’ll understand.

Huyu mtu tangu nafahamiana nae ameyabadilisha sana maisha yangu maana ana mchango mkubwa sana. Alinisaidia kupata kazi nzuri na kuachana na kakazi kangu nilikokuwa nafanya, alinihamisha na kunipangishia sehemu nzuri zaidi. Baadae alininunulia gari nami nikawa natembea nimekaa, pia amenijengea nyumba iliyo kwa jina langu ila kwakuwa ipo nje ya mji nimeipangisha nakula kodi ila bado analipia kodi hapa ninapoishi.

Mahusiano yalipoanza sikufikiria hata yangechukua miezi 6, ila sasa ni miaka mitatu+. Ni mwanaume anayejali sana ila ana wivu balaa. Ni mara kadhaa amekuwa akinitishia kuwa akigundua ninamsaliti atanikata shingo. Sasa huwa najiuliza huyu ni mume wa mtu, anatarajia kweli niwe na yeye tu ili iweje?

Sasa nimechoka jamani, natamani niwe na mpenzi wangu na sio mume wa mtu. Kuna huyu kijana nimeanza nae mahusiano sasa ni miezi 5, kusema kweli nampenda na ninaona kabisa nae ananipenda. Haya ndio aina ya mahusiano niyatakayo. Nimekuwa nikitafuta visingizio kuwa asije kwangu maana sio maadili ila ukweli ni kuwa naogopa mlipa kodi akijua atanitoa roho.

Huyu mume wa mtu nishamtafutia visingizio ili tuachane ila inashindikana. Natamani yeye ndio aanze ili asije kuwa na kinyongo. Ila kuna wakati najipa moyo kuwa nimwambie tu tuachane lakini nikikumbuka aliwahi kunikunja nusura anipige alipokuta msg asizozielewa kwenye simu nahisi kutetemeka. Aliwahi kunionyesha silaha anayomiliki, nilipomuuliza ni ya nini akasema hata mimi nikimletea ujinga ananifyatua. Japo ulikuwa utani ila niliogopa kusema kweli.

Balaa zaidi recently ameanza kung’ang’ania nimzalie. Nimekuwa nikijifanya mimba hazishiki ila kusema kweli natumia dawa zisishike maana siko tayari kuzaa nae. Kwanza nahisi kama suffocation maana ananibana sana. Kwangu anakuja tu muda wowote akijisikia, na ole wangu asinikute nyumbani ni tatizo kubwa. Kila ninachofanya anahitaji apate taarifa kwanza, yaani kama mkewe vile jamani.

Nimejaribu kuelezea haya ili angalau muelewe ni kwanini nahitaji msaada wa mawazo yenu ili nijikwamue kwenye hili shimo nililojichimbia. Nipeni ushauri naachanaje na huyu mwanaume bila kuleta madhara kwangu.
Kwa nini usiolewe mke wa pili? Hivi unaujua uchungu wa kumchuna vyote hivyo halafu umuache? Hivi hujawahi kusikia matukio ya watu kuuana kwa sababu ya wivu wa kimapenzi? Fikiria kabla ya kutenda. Huo ndio ushauri wangu.
 
Hii story ya mtoa mada inaweza kunigusa kwa namna mbili.

1. inashabihiana Sana na ya jamaa yangu mmoja wa karibu sana, (yule wa sheli)
Isipokua Mambo kadhaa
- kwenye suala la nyumba na kuipangisha,ila ile nyumba docs ziliandikwa kwa jina lake jamaa na sio la mwanamke (NIKIWA SHAHIDI).
-kwenye suala la umri wa mahusiano, Ni miaka 3 na nusu na sio miaka 3.

Ila kila kitu kilichobaki Ni 100% true, suala la bastola Ni kweli anayo, ilo la kumtishia Sijui jamaa hajawai nambia khs kumtishia.

2. Inashabihiana Sana na ya kwangu,
Isipokua Mambo kadhaa
-kwenye suala la nyumba, ya kwangu bado Ni pagale sijaimalizia nmempangishia TU nyumba.
-kwenye suala la Gari, sijamnunulia gari Ila tangu wiki ilopita jumamosi Kuna Gari ya mtu nmeazima (kilitime) nmempa awe anatumia kwa muda.
Ila sio yangu Wala sijamwambia nmemnunulia yeye. NMEMPA TU ATUMIE bila MAELEZO yoyote.
-Kwenye suala la mimba, Hilo Mimi ndo Sitaki kuzaa nae TU. Kama anatumia madawa labda kimya kimya sijui Mimi.

Ila kila kitu kilichobaki Ni 100% true, hasa ilo suala la kumtishia bastola na suala la umri wa mahusiano Pamoja na sarakasi nyingine zote alizoeleza.

KWAIYO MPK SASA NIKO DILEMA,
MPAKA PALE NTAKAPOJIRIDHISHA HII STORY BAADA YA UCHUNGUZ WA KINA KUANZIA IYO KESHO[emoji848]
 
Back
Top Bottom