Nimeletewa Kesi: Mke wangu anatoka kimapenzi na Mume wa Mtu

Nawasihi washikilie hapohapo 😀😀hojazao Zina mashiko ni Utapeli 🤣🤣Sasa unafunga ndoa miak miwil unamuacha mume sawa humtaki ndo ubebe na kitanda mwenzio alale wapi🤣🤣
😂😂 Hili balaa ndoa utapeli, ndo dhuluma , ndoa wanachukua samani za ndani 😂
 
MAMBO YA MSINGI YA KUYAFAHAMU KABLA YA KUINGIA KWENYE NDOA:

1. Sherehe ya Harusi ni ya siku moja tu, na Ndoa ni ya maisha yote.

2. Mwanamume/Mwanamke aliyezoea kuchepuka kabla ya Ndoa, ataendelea kuchepuka hata baada ya Ndoa.

3.Upole na ukimya si kiashiria cha tabia njema.

4. Ukikitaka ambacho hakijawahi milikiwa na mtu yeyote, ni lazima ufanye jambo ambalo halijawahi fanywa na mtu yeyote.

5. Mungu akitaka kukubariki hukuletea mtu, na Shetani akitaka kukuangamiza hukuletea mtu.

6. Bora uishi mwenyewe kuliko kuoa ama kuolewa na mtu asiye sahihi.

7. Aina tatu za wanaume wakuepukwa:
(a) Walevi
(b) Wazinzi
(c) Wagomvi.

Aina tano za wanawake wa kuepukwa;
(a) Walevi
(b) Wazinzi
(c) Wachawi
(d) Wagomvi
(e) Wasio tii

8 .Kuolewa na Mchekeshaji hakutakufanya uwe na Ndoa yenye furaha.

9. Maneno matatu yanayojenga amani katika Ndoa:
(a) Nakupenda.
(b) Samahani.
(c) Asante.

10. Kupiga punyeto kwa mwanaume na kujichua kwa mwanamke ni kuharibu mwili wako mwenyewe.

11. Kuoana kabla ya kuwa marafiki ni kama gari bila mafuta, hamuwezi kufika popote.

12. Mafanikio ya Ndoa siku zote ni pembe tatu:
Mungu mmoja
Mume mmoja
Mke mmoja.

13. Furaha ya kudumu maishani hutegemea na chaguo lako la mwenzi katika Ndoa.

14. Usioe/kuolewa na pesa au mali. Oa/Olewa na mtu. Pesa/Mali hufilisika lakini utu hudumu milele.

15. Uchumba uliovunjika ni bora zaidi kuliko Ndoa isiyo na amani wala furaha.

16. Usiweke kipaumbele chako kwa muonekano mzuri wa mwanamke. Hakuna mwanamke mbaya, bali anahitaji kupendezeshwa.

17. Mapenzi si upofu. Upofu ni kuoa ama kuolewa na mwanamume/mwanamke kwa sababu tu anakidhi haja zako kingono.

18. Ukiwa rafiki mwema, utawavutia marafiki wema. Vivyo hivyo kwa marafiki wabaya.

19. Asili ya mikono inayojali ni moyo unaojali.

20. Iepuke Ndoa mbaya kabla haijaanza.

MUNGU AKUBARIKI ILI UPATE CHAGUO SAHIHI.
 
Kwakweli ni shida
Kunarafikiyngu Jana wameachana na mkewe mke kasomba vitu vyote vya ndani ndoa Ina miak 2 na ni ya kanisani nimemuonea huruma sana
Kataa Ndoa Wana hoja wakat mwingine
Duh! Nn sababu ya kuachana, usaliti?
 
exalioth usihangaike mtafute yule dada aliyesema hivyoo baada ya hapo mwambie naomba namba za mumeo , akikupa mwombe mkeo simu halafu piga hiyo namba au text au piga uone amemsavuje au amejibu message imeandikwaje halfu screen shots watumie wazee wako nawake halafu unaomba ushauri . Nifanyaje
 
Kwakweli sijauliza niliomba aongee wayamalize akasema kaongea nae Zaid ya miez 4kaomba samahani zote kambeleza miez 4 wanaishi kama kaka na dada ni kupika na kula tu mwisho kaamua amuche aondoke kama anavotaka
Unafkir atakuja Kuoa huyo.
 
kuwa makini huo ni mkakati wa kukutoa relini .
Tuliza Moyo, tuliza akili huyo dada na mkeo kuna vitu vyako wanahitaji kwako halafu wewe ni kikwazo.

Be very carefully Mwanaume Kamili.
Tena usithubutu kumshirikisha mkeo.
Cha kufanya mchunguze kwa umakini mkubwa sana nyendo za mke wako dhidi na huyo mume wa huyo dada,
Lakini pia mchunguze kwa makini sana mawasilino na nyendo za mkeo na huyo mke wa mtu aliekuja kushtaki.
Utakachogundua , kitakupa mahali pakuanzia kuiconfront hii issue.
Na utaisolve swiftly but also softly
 
Ubarikiwe, Nimepata kitu hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…