Nimeletewa Kesi: Mke wangu anatoka kimapenzi na Mume wa Mtu

Nimeletewa Kesi: Mke wangu anatoka kimapenzi na Mume wa Mtu

Ndugu zangu wana jamiiforums habari za asubuhi hii ? kwangu mimi ni mzima wa afya na nipo sawa kabisa

Sina cha kupoteza Kama mnavyoona hapo juu kwenye bandiko.

Jana jioni mida ya saa moja nikiwa kazini kwangu kuna dada ninayemfahamu kwa sura tunaishi mtaa mmoja alikuja kazini kwangu, hapo kazini kulikua na watu kadhaa wakipata huduma,

Baada ya watu wote kuondoka alinifata huyo dada akanieleza kwa uchungu mkubwa kuwa "mke wako anatembea na mme wangu mwambie mkeo aachane na mme wangu" maneno hayo aliyatamka kwa kuyarudiarudia na mpaka machozi yakamtoka

Kuna watu wakatokea pale kupata huduma yule dada akaondoka sikupata nafasi ya kuzungumza nae kiundani ili kujua mke wangu alitembea na mme wake lini, na nimeshindwa kuchukua hatua yoyote mpaka sasa nashindwa nianzie wapi, inavyoonekana mpaka dada huyu kulia kwa uchungu mbele yangu itakuwa kweli mke wangu anatoka kweli na mmewake

Ndugu zangu hili suala ni zito kweli kwangu nianzie wapi, majibu sina. Nimeamua kulileta hapa mimi kijana mwenzenu mnipe mawazo nifanye nini nimetuliza akili yangu sijakurupuka ila hatua ya kwanza nimeona nililete hapa.


Asanteni
Yuda_exalioth
Jamiiforums_Geita
Hii ni story au hadithi?!!
 
1..kuongea huku akilia kwa uchungu haimaanishi kuwa maneno yake ni kweli kwa asilimia 100,..hivyo hupaswi kuyaamini bila ushahidi....

2..uhusiano wako na mkeo ukoje mpaka sasa?..anzia hapo

3.. ikiwa ni kweli, je unazani ni nini chanzo na nini utafanya?.. swali hili lakupasa ujiulize na ujijibu wewe mwenyewe ukiwa na akili timamu bila stress wala presha ili upate jibu sahihi...

4.. kumbuka NGUVU SIO TIBA BALI HEKIMA NI DAWA....
Uzi ufungwe
 
Mtafute huyo dada ambaye ni mke wa mtu, mkae akueleze vizuri kisha kama ana ushahidi akupe na kama hana mtafute, tena ushahidi usio na shaka, ama mtege fumanizi mumfumanie kisha piga picha na video kisha wewe kaka uliyeletea hizo taarifa uamue usuke ama unyoe. Pia kumpoza huyo dada machungu na wewe kujipoza mtongoze na ummege ili iwe 1 kwa moja na sio moja bila kisha muendelee na maamuzi yenu, kama Mtaendelea na ndoa sawa kama mtaanchana pia ni sawa ila ni bora muendelee hasa kama mna watoto maana wanawake wa sasa ni mitihani unaweza ukaruka maji ukaenda kukanyaga moto kwa kupata mke mwingine ana tabia mbaya mara 2 ya huyo mkeo.
 
Muda wa kuelewa lyrics ni pale ukipigwa tukio ila hakuna tukio unainjoi mdundo kinachosemwa unapuuzia.

First impression na upendeleo vitenge unapoanza udadisi.
 
Back
Top Bottom