Mimi Kama raisi wa ma jobless pro max, nakupa heko kwa kuweza kuhitimu mafunzo.
Usi sikilize maneno ya watu, kwamba hio pesa ni ndogo, we mwenyewe nadhani una jua vyema jinsi vumbi la mtaa lilivyo zito.
Kikubwa jishikize hapo, huku uki piga kazi kwa juhudi, achana na msemo kidogo, maana hivyo vikubwa havi kuja kwa siku Moja.
Nanukuu: "Usi sikilize maneno ya watu, kwamba hio pesa ni ndogo, we mwenyewe nadhani una jua vyema jinsi vumbi la mtaa lilivyo zito".
Mwl. wa Bios? hajafanya hesabu na kubaini kwamba huo mshahara wa laki moja u'nusu ni
Tzs. elfu Tano kwa siku.
Kama Mwl. anaishi na wazazi au ndg. labda anaweza kumudu maisha. Lakini kama anajitegemea, sijui ataishije. Hebu tuone hesabu lake
🙁Theoretical):
1. Chai au kifungua kinywa asb. shs. 500/=
2. Chakula Mchana Shs 1,000/=
3. Chakula jioni shs.1,000/=
4. Umeme (
tariff 0) kwa siku shs 300/=
5. Kodi ya pango kwa siku (chumba cha 50,000 kwa mwezi)Tzs. 1,500/=
6. Maji ya kunywa (
maji chapa Uhai) Lita 1 kwa siku 500/=
7. Nishati(
Mkaa wa kupikia fungu moja) shs 200/=
Hadi hapo ukijumlisha Tshs. 5000/= kwa siku zimeisha.
Je, Anakaa karibu na shule ili atembee kwa mguu asilipe nauli?
Je, haogi au kufua nguo ili tuseme hatohitaji sabuni?
Je, Hana simu ili tuseme hatonunua vocha?
Kwa maoni yangu, Naona kwa mshahara huo; mwl. atadhalilika mahali.