Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Ekari tano kulima ilinigharimu laki nne, nilipata vijana wanne kwa makubaliano unawapa sehemu ya kulala, wanatembea na kapu lao ndani wana sufuria. Wanaamaka asubuhi wanakwenda kulima mpaka saa tano wamemaliza. Wakirudi wanapika chakula chao wenyewe. Iliwachukua siku tatu kumaliza ekari tano na kila mtu alishika laki yake mkononi.
Tulipanda mwezi November, palizi tumemaliza wiki iliyopita. Palizi ilichukua laki mbili. Kuna wanunuazi wameomba kuchukua shamba kwa milioni tatu. Hili bado sijaafikiana nao. Ninataka kuuza rejareja kwa watakao hitaji ya iftar.
Shamba liko katika barabara kuu kwahiyo changamoto ya usafiri sina. Faida nyingine ni kula kisamvu, baada ya palizi tumeanza kula kisamvu na kitamu sana.