Nimelima ekari tano za mihogo, itakuwa tayari kwa mavuno mwezi wa Ramadhani

Chondechonde usiwauzie wajanja wa mjini sitasahau walimliza dada mmoja mjane aliamua auze ili apate ada ya watoto, kilichomtokea si yeye hata Mimi sitosahau, jamaa walikuja na Fuso wakaanza kuvuna mihogo Fuso halijai heka ya kwanza, ya pili, ya tatu na mihogo imeishia nusu ya gari, mwisho dada wa watu akawaambia basi acheni wakang'ang'ania kuvuna mwisho akawaambia na hela yenu msinipe nikama nimewalimia ninyi. Sio hadithi hii ilitokea chanika miaka ya nyuma 2006, nadhani Sasa watakuwa wameongeza utaalam zaidi wa kuwaibia wakulima.
 
Patana nao au chukua hellaa hii biashara ina tabia ya kushuka bei kadri muda wa mavuno unvyoendelea

Sent from my VTR-L29 using JamiiForums mobile app
 
Hongera sana kwa uthubutu mkuu, napenda kufaham hii laki nne ilijumlisha na hela ya mbegu? Na vipi gharama za kupanda zlikuaje?
 
Hongera sn kwa uthubutu mkuu, napenda kufaham hii laki nne ilijumlisha na hela ya mbegu? Na vipi gharama za kupanda zlikuaje?
Mbegu nililetewa mizigo 40 kwa 8,000 mzigo mmoja
 
Ingekuwa enzi za mwendazake huu ndio ungekuwa mwanzo wa kutekwa na yale majamaa
 
Kuna pahala umesema unachuma KISAMVU... huwa nafahamu Muhugo ulochumwa KISAMVU hufanya MUHOGO kuwa Mchungu na sehemu zingine haufungi kabisaa
 
Tumebakisha less than 3 weeks heading into HOLY MONTH OF RAMADHANI... nashindwa kukuhakikishia km Mihogo yk itakuwa tayari coz sijajua umepanda mbegu gani
 
Kuna pahala umesema unachuma KISAMVU... huwa nafahamu Muhugo ulochumwa KISAMVU hufanya MUHOGO kuwa Mchungu na sehemu zingine haufungi kabisaa
Sijalifaniya uchunguzi hili, lakini ninakumbuka tulipanda miti ya mipira special kwa kuchuma kisamvu miaka mingi iliyopita.
 
Kuna pahala umesema unachuma KISAMVU... huwa nafahamu Muhugo ulochumwa KISAMVU hufanya MUHOGO kuwa Mchungu na sehemu zingine haufungi kabisaa
Inategemea na mchumaji mkuu, kisamvu cha mihogo kwa usalama zaidi inatakiwa achume mwanaume,
Hata kunde na mazao mengineyo ya mboga inatakiwa achume mwanaume, usiruhusu hata siku moja achume mwanamke au binti maana huwezi juwa yupo kwenye hali gani

Ila kisamvu cha mihogo ni kitamu asikwambie mtu
 
Daaaah.
Dada Sky Eclat njoo tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…