Nimelima ekari tano za mihogo, itakuwa tayari kwa mavuno mwezi wa Ramadhani

Tabia yenu Wanaume wa Dar wengi kupenda kula ftari la chapati ,tambi ,andazi

Na kuacha kula mazao ya mizizi kama mihogo ,magimbi, viazi nk muache hio tabia
We mwenyewe ni Kunguru wa Manzese. Ungekuwa Kunguru wa Kibondo au Simbiti ningeelewa hoja yako.
 
Tunaomba mrejesho bimkubwa
Maana mfungo ndo umeisha hv
 
Naona atakuwa bado anakokotoa hisabu ya mapato na matumizi ili aje na mrejesho ulioshiba.
Mama yetu huyu kwa msio mjua huwa ni kama motivation speaker. Utakuta anasema vitu vingii, utadhani kweli anafanya, kumbe kaja tu hapa ku-socialize. Yeye yupo zake nje ya nchi Uzunguni anakula maisha. Sasa hizi kazi za wavuja jasho ataziwezea wapi?

Unakuta siku nyingine anasema kaona fursa baada ya kwenda Ferry hivyo ataanza kukaanga dagaa na kuawauza kwenye Mwendokasi, kumbe wakati huo yupo zake Uzunguni ndani ya nyumba kawasha heater anaondoa ubaridi. Hapa kaja ku-refresh mind kutokana na loneliness iliyopo kwa Wazungu maana uzunguni ukitoka kazini kama siyo wakati wa summer ni kukaa ndani mwako na kujifungia kama kuku wa kisasa.. Ha ha haaa.
 
Madamme, niko very impressed na mapambano yako[emoji119][emoji119]
 
nmejikuta nmecheka hatar [emoji1][emoji1][emoji1]
 
Walimwibiaje?
 
Mbegu nililetewa mizigo 40 kwa 8,000 mzigo mmoja
Kwa hiyo mpaka hapo ni
Mbegu 320,000
Kulima 400,000
Palizi 200,000
JUMLA 920,000

Ofa 3,000,000
Ukikubali ofa, faida 2,080,000

Je imechukua miezi mingapi toka upande mpaka ulipopata ofa ya Tshs. 3,000,000?
Vipi hakuna gharama za wadudu waharibifu au ulinzi wa shamba dhidi ya wezi?
 
Ingia shambani usilimie hewani
 
Watu wa pwani wakisema kisamvu kitamu ,tunajiuliza sana maana iswahili chenu kigumu
(Sorry ni chombezo )
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…