Nimelima nyanya heka 1 nimepata faida ya Tsh. Milioni 9 ndani ya miezi minne

Asante kwa kutoa fursa ya kuulizwa...

Mimi nahitaji kulima mkoa wa katavi, hao wateja wa rwanda kenya na uganda hufika huko?
 
Hongera sana mkuu,maneno Yako mazuri
 
Lakini umepoteza mda mwingi kuwananga vijana wanaokula maisha yao ya dar na simu ghali
Uzi ulikuwa nyanya ila ukabadilika mengine
Sasa jaribu kuongeza nyama kwenye nyanya
 
Kilimo hakipo hivyo acha uongo
 
Well said
 
Upo sawa mkuu sahivi nategemea kupanda cabbage heka3 4 wiki ijayo jtatu vijana wanaingia mzigoni kupanda. Mbegu Iko tyr
Usisambae sana mapema
Kama nyama zinalipa jikite kwenye nyanya tu

Usifanye diversity mapema concentrate kwenye hiyo nyanya inalipa

Nyanza imeonyesha faida ya milioni 9 faida kwa mwezi endelea na Nyanya tu kwa miaka mitano mfukulizo kabla ku divesfy expand ekari za Nyanya ni mapema mno kufanya diversification kama Nyanya inalipa fanya diversification after five years kama profit ya nyanya iko consistent for all those five years

Ku diversity kwenye business huhitaji utulivu wa akili za kibiashara don't rush

Hata uki diversify hiyo new business ipe at least five years huku una nyanya na huku una hiyo new business ukiziangalia zote before diversifying kwenye product ingine ya tatu

Usione akina Azam wana Products nyingi Azam food,Azam Marine,Azam Media na Azam Sport nk diversification haiendi mbio kama fast food kukaangiwa chips kuku chap chap

Diversification ni serious business consideration
 
Acha ushamba kilimo kinacholipa ni milungi na bangi pekee robo heka ya milungi unalamba 2.5 milion wakati umeilima kwa 150000 so janjaluka
 
Kwa faida ya wanataka kulima

SHAMBA.

Mimi shamba ni la nyumbani ni Bure Pamoja na mbolea samadi ilikuwa Bure pia.

Uaandaji pamoja na kulimiwa ni Bure pia Kuna ng'ombe kwetu na jembe la kukokotwq na ng'ombe (pirau)

MBEGU :-Nilinunua mbegu ya nyanya kutoka Epinavi nitaweka picha zao na mawasiliano Yao hapa chini.

Awali niliambiwa gram 50 kama ingeota vizuri ingetisha kupanda Heka1 yote.

Hivyo nilinunua gram40 ya mbegu aina ya Tanzanite F1
Nikanunua gm10 Dhahabu F1
Nikanunua gm10 imara f1

Bado hazikutosha Kwa heka moja
Hivyo nilitafuta Kwa mkulima mwenzangu Ambae aliniambia yeye ana mbegu inaitwa Onex kama sijakosea na aliikamua tu sio pure.

Kwa vile nilitaka kupanda na zisipishane nikanunua kwake jamaa na kupandikiza

Mnamo trh7/3/2024 nikianza uhamishaji wa Miche kutoka kitaluni na Hadi trh 13 zoezi la upandaji liliisha.

Palizi nilitumia vijana wangu wa kazi ambao wapo4 tu

MBOLEA YA VIWANDANI:-nimeweka mara5 na Kila kuweka nilikuwa natumia mifuko2 au 2 kasoro.

(Hapa mbolea zinatofautiana kulingana na umri wa nyanya)

VIUA TILIFU/KUVU:-Nimetumia kadiri inavyohitajika Sina idadi sahihi.

VIFAA :-Majembe,solo nk pia.

MAVUNO RASIMI NA MAKUBWA :-
Mchumo wa kwanza tray 47 garde1
Grade2 try4
Mchumo wa 2 box 63¹
Grade2 box9
mchumo wa3 grd1 try54
Chenga13

BEI:- Awamu ya 1 niliuza grad1 Kwa 45k chenga32k

Awamu ya pili grd1 niliuza Kwa 53 chenga42 nyanya ilipanda bei

Awamu ya 3 bei grd1 48k
Chenga25k.

Kwa ujumla wake nilipata Tsh8,800,000 na Hela kadhaa mesahau

Baada hapo nikianza kuuza Kwa bajaji
Na kwenye matenga hapa Sasa ni changanyikeni tu maana sikuwa shambani na kupigwa nilipigwa na vijana pia sikuwa na jinsi kutokana na kubanwa na kazi na hata kuandika idadi nilishindwa.

Mara kadhaa mzee wangu ndo alihusika na mauzi akiwapo shambani

Na pesa ilikuwa unatumiwa kulingana na mauzi maana ilikuwa Kila siku natumiwa Hela ambayo Kwa ujumla ni nilipata 5,378,000/= maana msg nilikuwa sifuti.

Ukija jumlisha zote Ni Tsh 14,178,000/=

Wafanyakazi ni4 Kila mmoja 500k Jumla 2,000,000/= zilibaki ni dhana za vilimo madawa na mbegu nk.
 

Attachments

  • IMG_20240419_173003_744.jpg
    992.2 KB · Views: 38
  • IMG_20240510_074036_916.jpg
    485.7 KB · Views: 43
  • IMG_20240509_142915_223.jpg
    2.5 MB · Views: 41
  • IMG_20240622_172444_112.jpg
    2.7 MB · Views: 38
Ushauri wako makini sana nimeupokea mkuu.

Hapa nilipo **** shida maji hivo nilienda kukodi shamba sehemu yenye mkondo wa ziwa Victoria ndo nikapata hizo Hela 4 Tena Kwa shart kuwa ifikapo mwezi wa11 kusiwe na zao lolote maana ndo wanategemea kulima mahindi nk. Ndio maana nikaona kuliko kukaa na vijana wangu wa kazi Bure ni Bora nilime cabbage mkuu.

Baada ya hapo narudi hapa kwenye shamba la nyanya Tena na hii nitapata faida zaidi ya hiyo na uhakika maana masika nyanya Huwa unaweka sana ukizingatia tu matunzo stahili.

Shukran sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…