Nimelima nyanya heka 1 nimepata faida ya Tsh. Milioni 9 ndani ya miezi minne

Sisemi kama jamaa ni muongo,au labda Kwa vile mgeni mbinu zake za uoteshaji mivhe ni hafifu.Mimi nalima nyanya Kwa miaka mitatu sasa,nikiotesha miche kwenye gram 25 ya nyanya dhahabu au imara napata miche elfu Tisa(9000) kwenye ekari moja unaingia miche haizidi 7000,kama kuna miche kufa au chochote hiyo miche iliyobaki utafidia(japo Mimi binafsi hua nafiwa na miche haizidi 500)
Mtoa mada anadai amepanda gram 60 za mbegu ambazo ni takribani miche elfu ishirini(20,000).
Ukumbuke gram 25 ya nyanya F1 sio chini ya 360,000.
Kwa nyanya za awali alizopanda katumia almost laki Tisa kwenye mbegu.
Kwanini upoteze hela zote hizo kwenye mbegu,miche yote hiyo 20,000 inatoshaje kwenye ekari moja?
 
Nataka kufanya kilimo Cha nyanya mkuu..naomba contact na wewe
 
Mkuu gram 20 nilizo sia nilipanda mashina 2,700/= tu baada ya kuona mbegu Ina punguana nilivyo tarajiando nikanunua mbegu zingine kama dhahabu,imara nk lengo nikukimbidhana Ili nipande Kwa Wakatiaana Ile Tanzanite F1 ilikuwa Hadi uagize Arusha.


Elimu Haina mwisho nipe mbinu zako za usiaji wa mbegu nijifunze nipo Tyr kujifunza Kwa 100% Ahsantee sana.
 
Pia umesema kuwa heka moja inachukua mashimo (mashina) 7000 unachimba Kwa umbali Gani na kwanini? Ahsantee
 
  1. Mada imetoka nje ya kilimo
  2. Maelezo ya kilimo ni juu juu
  3. Ulipo fanikiwa wewe,siyo kila mtu afanikiwe ....Wakati wewe unakimbia Dar,wengine wametobolea Dar.
  4. Siyo kila mtu lazima ajenge
 
Umepataje faida yote hiyo mkuu? Umevuna lini mbona kila Kona watu tunalia bei mbaya huku mpaka sasa hivi wengine tumetelekeza tunaandaa mbegu nyingine tu maana hela haiwez kurudi tena
Kilogram moja imedrop half price kuna mafuriko ya nyanya, kama kuna mahali soko zuri tuambizane jamani.
 
Otesha mbegu moja moja kwenye tray .nenda YouTube tafuta video za jinsi ya kusia nyanya kwenye tray.usimwage chini
 
Nataka kufanya kilimo Cha nyanya mkuu..naomba contact na wewe
Kabla hujataka kuingia kwenye kilimo hichi lazima uwe na uhakika WA maji ya kumwagilia(hela ipo kipindi cha ukame),Je Una kisima ama mto usiokauka?budget iliyokamilika ya mbegu,dawa na mbolea,chakula cha wafanyakazi Kwa miezi 4....cha Kwanza ingia YouTube,jifunze jinsi ya kusia mbegu,na kuna video nyingi Sana.Ikiwezekana nunua m begunweka hata bustani ndogo ya nyanya uwani kwako ili ujifunzie Kwa vitendo.Kilimo cha nyanya ni kigumu ila ni rahisi ukishakijulia.
 
Sawa Asante nafatlia nikijue zaidi...vipi kuhusu ukubwa wa shamba?
 
Uko wapi wapi,tenga unauzaje?
Huku chato mganza mkuu huwa tunauza kwa kilo ila sometimes kama bei ikidrop kama hivi now crate inaenda kwa 20k shamba ila ni crate ile kubwa special ya plastic
 
Kamwe huwezi msikia Azam au GSM akisema nimefanya hilo nimepata hiko, njoono tufanye
Hakika hata Mimi sio Azam Wala GSM mkuu.

Mimi naitwa Nikifa MkeWangu Asiolewe ndo jina langu. Hao uliwataja nawasikia tu Wala sijawahi kuwaona Kwa macho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…