Nimelima parachichi hekari 14 lakini kwa mara ya kwanza nimepata viparachichi vidogo sana

Naam nilikuja na Mtaalamu toka njombe, akaja huku songea na yeye ndio alifanya budding na kila kitu
Alipima udongo?
Mtaalamu kweli wa kusomea ambaye anajua mbegu sahihi kwa maeneo tofauti?
Sababu namfahamu jamaa anajiita mtaalamu wa miti ya matunda anafanya budding (grafting) ya mimea. Anasafiri mikoani kwa kukodiwa ila hajagusa hata darasa la kwanza na hajui kusoma na kuandika.
Wataalamu wa mtindo wa huyu jamaa yangu hawawezi kufanya proper judgement ya aina ya mbegu na aina ya udongo husika baada ya vipimo.
 
Iyo mbegu ni hybrid na sungwi si unaona mengine yana rangi ya blue
 
Kui convert nadharia kuwa hela nacho kipengele
 
mshaurini kama inahitajika mbolea au chochote,
 
Nimelima na kupanda miparachichi heka 14 mwaka ndio zimezaa lakini ninapata wasiwasi mana ni vinekuwa vidogo sana kiasi kwamba nahisi haviwezi ingia sokoni, je wataalamu ndio huwa hivi kwa mara ya kwanza?
Weka picha
 
Kuna wadau nilisikia wanaongea kwamba, maua wa kwanza unatakiwa kupukutisha yote mmea usiweke matunda uendelee kukomaa kwanza( mfano ni kuepuka mimba kwenye umri mdogo), uzao unaofuta ndio wenyewe.
 
Mnajua sana kukatishana tamaa πŸ˜‚πŸ˜©
 
Nimelima na kupanda miparachichi heka 14 mwaka ndio zimezaa lakini ninapata wasiwasi mana ni vinekuwa vidogo sana kiasi kwamba nahisi haviwezi ingia sokoni, je wataalamu ndio huwa hivi kwa mara ya kwanza?
Eti ''hekali''.
 
Its about Facts wewe jipe moyo.

Kujipa matumaini hakulete mafanikio.....laza ufanye kitu
Parachichi is a big business na watu wengi tuu wanapiga pesa za kueleweka, lakini kama kawaida ya maisha, wakulima waliofeli nao ni sehemu ya kilimo cha parachichi, jipange
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…