Kikubwa Pumzi
Member
- Jul 25, 2025
- 83
- 182
Kwa kweli ilikuwa inafanya vizuri kabla, mara ya mwisho nilitumia mwaka huu January. Baada ya hapo sikuwai itumia mpaka hii leo.Tatizo la mitandao ni janga kwa taifa..
Hivi ulikua unaitumia kabla ya hapo? Au ulifanya research ni router ya mtandao upi inayofanya kazi vizuri kwa eneo lako? Binafsi natumia router ya airtel na sijawahi kupata changamoto yoyote ikitokea labda iwe bundle imeisha au wazime mtandao ..
Ila unaweza kupiga simu fanya kama unaomba uletewe fundi then mtabanana hapo hapo kwanini kwako inatokea hivyo
Ndio maana nataka nione kama naweza kushtaki ili kuondoa majibu ya mazoea.Mbona mimi nimeunga sasa iv jion hii iko powa
Ishu sio kuachana nao, ishu ni utapeli wanaofanya naamini watu wengi wanatapeliwa kwa namna hii.Achana nao njoo voda
Huawei wapo Tanzania?Kwa uzoefu wangu mtandao mzuri kwenye data kwa sasa naanza na hii Fibre ya HUAWEI japo tunadanganywa ni TTCL, anafuata VodaCom, ndiyo wanafuata Airtel, Yas na wa mwisho ni Halotel na mkia ni TTCL.
Sasa Airtel kiukweli kwenye router wamecheza lakini siyo kwenye network.
Jaribu kuangalia settings zako za router then unaweza pia kutumia chatgpt atakusaidia pia.. It was very useful to me..Kwa kweli ilikuwa inafanya vizuri kabla, mara ya mwisho nilitumia mwaka huu January. Baada ya hapo sikuwai itumia mpaka hii leo.
Nilipata kazi ilikuwa leo kutwa nzima niifanye kisha niiwasilishe jioni hii lakini mpaka sasa nimeshafeli.
Na jamaa nimeongea nao kwenye huduma kwa wateja anaongea kama kasuku amekalili maneno mwisho wa siku anasema kila mtu hapati internet.
Africa bado tunaishi kama sokwe.
Unaijua hii nchi vizuri? Yaani ukawashtaki wapi??Ndio maana nataka nione kama naweza kushtaki ili kuondoa majibu ya mazoea.
Nimekomaa nao wamenirudishia 70K yangu. Ila wamenipotezea target zangu na pesa, dude lao nalitupa kabisa.Unaijua hii nchi vizuri? Yaani ukawashtaki wapi??
Hizo gharama za uendeshaji kesi ni bora uhamie tu mtandao mwingine....
Haikuwa ishu ya settings ni wao na uzembe wao wa kiafrica.Jaribu kuangalia settings zako za router then unaweza pia kutumia chatgpt atakusaidia pia.. It was very useful to me..
Mbona mimi inapiga kazi mkuu au hilo tatizo ni location. Nimeanza kuitumia toka mwaka jana mwezi wa tatu na nailipia kila mwezi bila kukosa. Mpaka sasa sina malalamiko naoNimekomaa nao wamenirudishia 70K yangu. Ila wamenipotezea target zangu na pesa, dude lao nalitupa kabisa.
Ile ni kampuni iliyojaa uswahili sidhani kama ina watu wenye history ya kuleta matokeo chanya popote.Airtel wana customer care mbovu kuliko mtandao yote
Nasikia ni mtandao wa kizimjob ndo maana wana jeuri
Fungua page yao ya Instagram kisha soma commmets kwenye post zao alafu urudi kueleza umeona nini.Mbona mimi inapiga kazi mkuu au hilo tatizo ni location. Nimeanza kuitumia toka mwaka jana mwezi wa tatu na nailipia kila mwezi bila kukosa. Mpaka sasa sina malalamiko nao
Hivi hizi tuhuma huwa ni kweli au ni a targeted campaign against Airtel TZ ? Nimeziona sana mtandaoni.Jamani, nimelipia router ya Airtel 5G, lakini mpaka sasa sipati internet kabisa.
Nimewasiliana na 100, nikaambiwa kuna tatizo la mtandao lililowakumba watumiaji wote na kwamba internet itarudi, na kwamba siyo tatizo la kifaa wala ufundi.
Sawa, nikasema ngoja nisubiri.
Lakini cha ajabu, mpaka sasa bado sina internet. Na nilipojaribu kuuliza watu wengine wanaotumia Airtel, wanasema wao wana access internet bila shida yoyote.
Sasa hapa ndipo ninapojiuliza, Airtel mnatuonaje sisi wateja?
Hizi TSh 70,000 tunazolipa siyo kwamba tunazitoa mfukoni halafu tunacheka. Wengine tunakopa. Wengine tunazitumia kwa kazi maalum za kutafuta kipato.
Mimi kwa mfano, nimepata kazi ambayo inahitaji internet ya uhakika. Nimeweka pesa ambayo kwa kweli nilihangaika kuipata, lakini sasa nimeshindwa kufanya hiyo kazi kwa sababu internet haipo.
Naomba kuuliza watu wenye uzoefu wa mambo haya:
Mteja anaweza kulalamika wapi?
Je, ukiathirika kwa uzembe au tatizo la huduma ya kampuni ya mawasiliano, una haki ya kudai fidia? Mfano, kama ulikuwa na kazi inayokusubiri na ukashindwa kuifanya kwa sababu huduma uliyolipia haikutolewa, sheria inasemaje?
Je, ni TCRA, Fair Competition Commission (FCC), au kuna chombo kingine cha kulinda haki za mlaji?
Na kama kweli kuna tatizo la mtandao kwa watumiaji wote, kwa nini baadhi ya watu wanaendelea kutumia internet bila shida?
Kwa kweli nimeathirika sana. Sijatumia Airtel kwa muda mrefu, nikarudi kwa sababu nimepata kazi inayohitaji internet yenye uwezo wa kutosha. Nimeamua kulipia router, nimeweka pesa ambayo nimekopa, halafu huduma yenyewe haifanyi kazi.
Hivi Airtel wanaelewa kwamba kwa baadhi yetu internet siyo starehe? Ni chombo cha kazi na kipato.
Mambo kama haya ndiyo yanayofanya watu kupoteza imani na huduma za kampuni za Tanzania.
Kwa sasa mimi binafsi siwezi kumshauri mtu anunue Airtel 5G.
Bongo bado tuna safari ndefu sana kwenye customer service, integrity na kuwajibika kwa mteja. Mteja analipa pesa yake halafu akipata shida anaambiwa tu “subiri, itarudi.”
Swali langu ni moja: NIKIATHIRIKA KIFEDHA KWA SABABU YA HUDUMA NILIYOLIPIA KUTOTOLEWA, NINA HAKI GANI KISHERIA? Na ni wapi napaswa kulalamika?
Wenye uzoefu, tusaidiane hapa.