KERO Nimelipia Airtel 5G, Lakini Internet Haipo — Nani Atanilipa Hasara?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kwa kweli ilikuwa inafanya vizuri kabla, mara ya mwisho nilitumia mwaka huu January. Baada ya hapo sikuwai itumia mpaka hii leo.
[Kanuni ya 25(1) [zamani Kanuni ya 8(6) katika GN Na. 112 ya 2020]:
Nukuu inaelekeza kuwa endapo laini ya simu au kifaa chochote chenye laini ya mawasiliano hakijatumika kwa mawasiliano kwa siku tisini (90) mfululizo (miezi mitatu), mtoa huduma wa mtandao analazimika kuizima/kusitisha huduma kwenye laini hiyo (shall be deactivated).

[Kighairi / Kinga ya Kisheria (Kanuni ya 25(2)):]
Kanuni inakataza mtoa huduma kuifunga laini hiyo endapo mteja atakuwa ametoa taarifa rasmi kwa maandishi kwa mtoa huduma wake kuwa laini hiyo haitatumika kwa kipindi mfululizo, mradi kipindi hicho hakizidi miezi 12 (mwaka mmoja).
===
Kwa ufupi fuata hatua hizi:

1. Piga simu - eleza wazi hitaji lako ni ukaguzi wa laini/simcard yako iwapo imezuiliwa/ imefungwa kutumia huduma
2. Fika katika ofisi za mtoa huduma - Utapatiwa simcard mpya

Tatizo: Simcard haijatumika kwa muda mrefu.
 
Kikubwa pumzi tu ndugu yangu haya mengine tuachane nayo ,ila tu leo it seems Airtel ilikuwa na shida kwenye internet
 
Nimeahawahi kutumia huduma ya Airtel Router kwa malipo hayo ya 70k kwa mwezi wanachodai wao ni unlimited internet lakini si kweli .

Wanadai kwamba kifurushi ni unlimited kwa speed kadhaa jambo ambalo kiuhalisia ni uongo.

Wanachokifanya ni kuwa wanawekea limits ya Gegabytes ukizitumia zikakribia kuisha wanakupunguzia speed ambayo haiwezi kufungua hata JF.

Niligundua hilo pale ambapo ilikuwa ikifika trh 19 - 23 ya kila mwezi speed ya internert inashuka mpaka nitakapounga kifurushi kingine cha mwezi.

Japo leo kulikuwa na shida ya kimtandao ila kama tatizo lako limeanza muda jua ni speed imepunguzwa .

Sasahivi nimehamia TTCL fiber shida yao mawayawaya mengi ila naenjoy speed na unlimited internet mpaka baasssii wao wanasema "karibu nyumbani kumenoga"
 
HUAWEI kwa jina la TTCL na then kuna TTCL ya mwisho tufafanulie kidogo hapo mkuu
 
kwahiyo TTCL imeuzwa si ndio???
 
Kwahiyo Savana hawana maajabu???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…