Nimemchoka mwanaume huyu lakini nampenda nifanyeje?

hamna cha kushauri hapo, ni wazi hapo ukiwa naye ndani ndo hata maendeleo hutayaona, anakupotezea muda hafai labda kama na ww upo hivyo vinginevyo utakuwa unampa nafasi ya bure. toka kwenye vimbweta mpaka leo mtu hajabadilika....when a woman loves!!!!!!:disapointed:
 

Haya,..
Huyu wakiona atakuwa haombi hela tu,ila akikosa atakuwa anabeba sahani anaenda kuuza,...
Naomba tu awe analeta ushuhuda hapa kama ata "LAZIMISHA KUFUNGA NAE NDOA"
 
Ukimuacha ndio atakuwa cha pombe zaidi, na hivi ni mwanajeshi kuna hatari kuwa anaweza kukudhuru

Jaribu kumtafutia saikolojisti amsaidie.

hiyo labda familia yake imtafutie, mbona kuchoshana mapema sana.
 

Mimi ni mtu mzima, na ndoa ya muda mrefu na watoto wakubwa. Nakushauri achana naye kabisa. Hutajenga maisha au kuwa na maendele0 ukiwa na huyu bwana kama mume. Piga u=turn imediately binti. Yaani huyu boyfriend wako hajui kesho, yeye ni leo tu. Kama utaamua kumzalia au kufunga ndoa basi ukubali kuendesha nyumba as a single parent while you are two in the house. Una kazi yako, tulia, Mungu atakupa mume bora.
 
shukuru hujaolewa naye bado! uchumba tuu FIKILIA ZAIDI!
 
Dada yangu addiction ni kitu kibaya sana hasa ya pombe, kama msomi wa kiwango cha chuo hajaweza ku- drink responsibly mpaka leo basi hata hiyo elimu yake ni kazi bure, siwezi kukushauri umuache mpenzi wako lakini kuwa makini, maana ku change ni issue, niliwahi kuwa na mpenzi aliyebobea kwenye kilauri kama huyo wako, mwenyewe nilichemsha, nikamuacha aendelee maisha yake. siku hizi hata mwili wangu unaanza kurudi, looh usiombe.
 

Hana mapenzi ya dhati anakupenda kwa sababu unauwezo wa kumsaidia anapokuwa na shida
mapenzi ni kusaidiana lakini huyu amezidi.
umejitahidi kumbadilisha habadiliki
achana nae huyo sio ubavu wako muombe Mungu atakupa ubavu wako
atakuja kukosa wa kumlea kama ulivyomlia atatia adabu na atabadilika
 
Daahha
huyo anahitaji professional help
kwa sababu ni alchoholic..
akipata good treatment na akienda
Rihab tabadilika..
 
Jamaniieeeeeeeeeeeee watu hubadilika. Kwa ukweli ni kero sana kukaa na mtu wa aina hii!
Mfano mimi kua wakati nilikuwa nikiamka nafikiria safari baridi saa 12 asubuhi. Yaani sifikirii kitu chochote. Hali hii iliendelea na zaidi nilipooa wakwe wakamnunulia binti ya yao. Sikujua kijiko wala uma ni nini. Kitanda chenyewe nilinunua baada ya kuoa. Usiniulize nilikuwa nalala wapi!
Mke wangu alivumilia haka katabia ka ulevi. Tulipopata mtoto wa kwanza wakwe wakamtunza mke wangu kwa miezi 3 hivi. Nilipomchukua mke wangu na kuanza kuishi naye na mtoto wetu, taratiibu akili ikaanza kuja! Kwanza nikapigwa stop no sigara kuvuta nyumbani! Ikawa nikija kwanza niende nikaoge ndo nimkaribie mtoto kutoa harufu ya sigara. Taratiibu nikaanza kuzoea nikaacha sigara nikabakia na pombe. Niandikapo hapa nina miaka nane tangu niache sigara na sasa huwa nakunywa bia mbili tu na mara nyingine napitiza hata mwezi bila kunywa. Ilifikia mahali njikipewa dawa ambazo siruhusiwi kunywa pombe situmii na hata nikitumia simalizi dozi! Siku ya kwanza tu jioni yake naanza kunywa!
Hiyo ni kwa baadhi ya watu,,,, ila kusema ukweli kubadilika ni mtu mwenyewe.
 
Acha upuuzi kua, macho unayo lakini huoni.. masikio unayo lakini husikii :bored: sasa unataka tukusaidie nini wakati kila kitu ushaona kila kitu mwenyewe!! Kwani umeambiwa wanaume wameisha?????:disapointed:

sijui hata alikwend achuoni kufanya nini huyu binti, ikiwa hata kuamua jambo kama hili linalohusu mustakabali wa maisha yake hawezi. Tena jamaa kawa mjeshi asubiri kubamizwa tu.
 


Halafu sasa ulale na mtu aliyekunywa pombe wewe hujanywa kha!!!! Usingizi hauji kabisa yaani pombe mbaya lakini mmmhhhh
 
Mi nadhani suala la kunywa pombe linaweza kuzuilika iwapo mnywaji akiamua na kama unywaji wake si wa kuwa forced na mapepo, otherwise akiombewa anweza kupona. Kwani kuna watu wengi nimewashuhudia wakiacha kunywa kwa kuamua wenyewe na wakafanikiwa. Tatizo mimi ninaloliona ni huyo boyfriend wako kuonesha mapenzi wakati kaishiwa fedha, mi nawasiwasi kama huyo boyfriend wako anakupenda kwa dhati, isijekuwa anakupenda kwa sababu unampa hela. Mi nakushauri umchunguze vizuri huyo boyfriend wako kama kweli yupo serious, kama yupo serious jaribu kumsaidia kuachana na pombe otherwise unapoteza muda wako tu....
 
Huyu jama kama every penny anayopata inaishia kwenye pombe hebu Nyambura jaribu kufikiria yafuatayo
1.Mkiwa na familia Je, hauwezi kujikuta wewe ndio unalea familia peke yako jamaa yeye hela itakuwa inaishia kwenye pombe tu.

2.Jamaa anatumia another trick ya kuzaa na wewe sababu anajua utakuwa una huruma kwake kwa kuwa ni baba wa mtoto

3.Kama hiyo abia haijabadilika tokea uko naye chuo kuna dalili zozote za yeye kubadilika sasa hivi

4.Ukiwa na familia inahitaji mtu kutuliza kichwa na sio kwa mambo hayo anayoyafanya sasa hivi

5.Kabla ya kuingia kwenye commitment yoyote ile inapaswa uhakikishe jamaa amebadilika kabisa tena ikiwezekana hata hiyo pombe awe ameacha kabisa.

6.Kitu kingine ambacho kinanishangaza huyu jamaa huwa analia ili umuonee huruma au iweje kama ndiyo hivyo inabidi ubadilike maana anatumia weakness yako ya kumuonea yeye huruma every now and then

7.You need to be strong na kufanya maamuzi sahihi ukikosea it will mess you up and cost you for the rest of your life.

Ni hayo tu
TF.
 

Yego..Ushauri wangu ni huu,ni kweli kwa fikra za haraka haraka huyo jamaa hafai...pili hujasema kama umewahi kumpeleka kwa watumishiwi wa Mungu (wachungaji,mapadri,mashehe,)..Tafadhali fanya hivyo..pia weka msimamo wako wazi,usimwambie anywe kiasi,hii kitu kiasi ni tata..huenda hiyo kiasi ndo kwake yeye inamfanya bwiii,MWISHO; NAOMBA UMSAIDIE,MAWAZO YA BINAADAM INCLUDING HAWA WA JF WANAANGALIA UPANDE MMOJA WA SHILINGI..USIMWACHE HUYO JAMAA HADI UHAKIKISHE OPTIONS ZOTE ZIMEGONGA MWAMBA..1. ITISHA KIKAO NA WAZAZI/FAMILIA YAKE (BILA SHAKA WANAKUTAMBUA), 2. TAFUTA WATU WA MAKAMO,MKALISHENI CHINI WAKATI ULE AKIWA NA PESA,,FANYA BIDII UMPATE WAKATI HUO..3. MPELEKE KANISANI..AMINI AMINI NAKWAMBIA AKIEPUKANA NA BALAA HILO UTAPATA THAWABU KWA MUNGU,PIA UTAKUWA UMEMWOKOA( UMETIMIZA UKRISTO WAKO/UISLAM..) ASANTE
 
sijui hata alikwend achuoni kufanya nini huyu binti, ikiwa hata kuamua jambo kama hili linalohusu mustakabali wa maisha yake hawezi. Tena jamaa kawa mjeshi asubiri kubamizwa tu.

Umeona mkuu watu wengine mpaka wanaudhi, kweli kusoma sio kuelimika... sasa huyu mleta mada anatofauti gani na wale watoto walotoka shule za kata mwaka jana????:bored:
 
Umeona mkuu watu wengine mpaka wanaudhi, kweli kusoma sio kuelimika... sasa huyu mleta mada anatofauti gani na wale watoto walotoka shule za kata mwaka jana????:bored:

Kwenye mapenzi hakuna Kisomo, hata uwe na PHD utafanya mambo ambayo mtoto wa shule hiyo ya kata atashanga
 
huyo jamaa hawezi kusaidiwa mpaka yeye mwenyewe ajikubali kuwa ana matatizo ya ulevi wa kupindukia.tatizo na wewe unamlea maana anajua akianguka,wewe ndio unamuokota kwa kumpa hizo hela.jaribu kumwambia siku hizi sina,natengeneza maisha,na ujaribu kumwambia,kama unanipenda,jaribu kuacha ulevi,maana miaka inaenda.muulize tukiwa na mtoto haya ndio maisha?
 
kama hujui kusoma basi hata picha hujui kuangalia
 
Ningumu sana kwa hiyo tabia kuibadilisha, ingekuwa suala ni pombe tu ningesema vumilia kama unampenda, ila kwenye suala la kukuomba pesa!!! hapo kama mwanaume ameshindwa kuelewa majukumu yake.
Na hata badilika kwa hilo, kosa ni pale utakapoamua kufunga naye ndoa, nipo utayaona makucha yake yote.
Tell him openly, and give him time to act on your words.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…