Jamaniieeeeeeeeeeeee watu hubadilika. Kwa ukweli ni kero sana kukaa na mtu wa aina hii!
Mfano mimi kua wakati nilikuwa nikiamka nafikiria safari baridi saa 12 asubuhi. Yaani sifikirii kitu chochote. Hali hii iliendelea na zaidi nilipooa wakwe wakamnunulia binti ya yao. Sikujua kijiko wala uma ni nini. Kitanda chenyewe nilinunua baada ya kuoa. Usiniulize nilikuwa nalala wapi!
Mke wangu alivumilia haka katabia ka ulevi. Tulipopata mtoto wa kwanza wakwe wakamtunza mke wangu kwa miezi 3 hivi. Nilipomchukua mke wangu na kuanza kuishi naye na mtoto wetu, taratiibu akili ikaanza kuja! Kwanza nikapigwa stop no sigara kuvuta nyumbani! Ikawa nikija kwanza niende nikaoge ndo nimkaribie mtoto kutoa harufu ya sigara. Taratiibu nikaanza kuzoea nikaacha sigara nikabakia na pombe. Niandikapo hapa nina miaka nane tangu niache sigara na sasa huwa nakunywa bia mbili tu na mara nyingine napitiza hata mwezi bila kunywa. Ilifikia mahali njikipewa dawa ambazo siruhusiwi kunywa pombe situmii na hata nikitumia simalizi dozi! Siku ya kwanza tu jioni yake naanza kunywa!
Hiyo ni kwa baadhi ya watu,,,, ila kusema ukweli kubadilika ni mtu mwenyewe.