Nimemchoka mwanaume huyu lakini nampenda nifanyeje?

Dada yangu siwezi kukuambia umuache japo ni wajibu wako kufanya hivyo...huyo ameshindwa kujilea sembuse kulea familia..uliona wapi mtu anamaliza mshahara kwa wiki mbili, siku zote yeye ni ombaomba..tafadhali kuwa strong katika hili na ufanye unachotakiwa kukifanya...mzalie uone moto...kwani atatumia kigezo cha wewe kuwa mzazi mwenzie kumiliki kila kitu, kama uhuru, akiba zako, hata kujaribu kukuaribia hata ajira ...sikutanii tumeshayaona kama hayo....kwenye maisha unapaswa ujipende wewe mwenyewe kwanza na hata unapopenda wengine unapaswa uwapende kama unavyojipenda na ninachokiona mimi kwako ni kuwa HAUJIPENDI KABISA..maisha sio uwanja wa mazoezi...kama unabisha fanya jaribio la kuzaa naye uone...SIKUTISHI
 
Naweza kukupa ushauri nje ya hapa?
Mi nimemsikia anaseama lazima uende na nauli yako na kinywaji juu yako. Mimi kama kaka yake nimemshauri asitoe tena nauli kwa vibuzi! Hata huyu mtarajiwa anataka mtoto wa bure ili naye alipiwe nauli ya kwenda kazini tunatangaza huduma kusitishwa kwa muda till next time!
 
Mshukuru Mungu umeweza kumsoma na kumuelewa mapema,usijitafutie majuto kwa kuendelea kuwa nae.Jiondoe hapo mdada.Piga goti Mungu akuoneshe na akupatie ambaye wewe ni ubavu wake
 
<p>
kuna mtu amewasaidia wengi.. no. yake ni 0712183282
</p>
<p>&nbsp;</p>


mhh tatiana huyo mtu anasaidiaje hao watu kimaombi au kiushauri? namimi labda nimpelekee matatizo yangu
 
<p> </p>
<p>&nbsp;</p>

wanaume wa sampuli hiyo wako kibao wanaitwa 'vimeo' hawafai utateseka mpaka ukome nakushauri temana nae upesi weka mtazamo kwa wanaume wenye akili shosti bora umeshtuka mapema.
Maana hilo sio bomu ni tetemeko kimbia
 
Utapewa ushauri kibao hapa tena wa maana but at the end of the day we sikiliza moyo wako tu!
 
kuhusu suala la ndoa ni vyema ukamshirikisha Mungu kwa maana labda atabadilika mkishaoana ila cha muhimu ni kutokubali kubeba ujauzito kabla ya ndoa takatifu, ukihitaji msaada zaid nipigie au nitumie msg kwene # 0785343853, Mungu akusaidie katika kufanya maamuz ya busara!
 
Msaidie mwenzio kama unampenda kwa dhati. kwanza mpe masharti kama anakupenda atakusikia, akipata hiyo pesa akupe mfanye mipango ya future kama kununua thamani za ndani na mambo mengine, yeye unampa tu pesa kidogo ya matumizi. Pia mwambie awe anaenda kanisani itasaidia kiasi fulani kusikia neno la Mungu anawez pata hofu fulani ya Mungu
 
nimuulize huyu dada; je unampendea nini huyo BF wako? maana tuwe makini na kusema unampenda mtu kumbe unakuwa UMEMZOEA TU kwasababu mmekuwa pamoja siku nyingi. ninamfano wa demu mmoja(mtoto wa kishua) alimpenda houseboy wao na wazazi walimkataza akakataa na kutishia kujiua. hapa ninachojifunza ni mazoea tu ya kuwa pa1 kimazingira/kimapenzi nk. so, kwa maelezo ya dada hapo juu ni kwamba mzigo umemelemea na hata hawezi kujisifu kwa wenzake kuhusu boifrendi wake (asiyemsaidia, asiyejipenda, unfocused etc). una nini cha kujivunia kwa huyo BF?
ushauri;
1. vumilia (maana kunawengine mmezaliwa mama huruma)-jifariji kwa kumuombea, kumpa ushauri.
2. quit na hutakuwa na cha kujutia
hakuna option nyingine
lastly, AMEKUZOEA SANA INAONEKANA NA ANAJUA WEWE NI MSAADA (POCKET MONEY)
remember; ndoa ndoano na challenges ni nyingi na wengine hupatia BP ndoani but on the other side of the coin ukipata chaguo zuri, ni peponi kila siku
 
unatoa number ya nini?? andika ujumbe kijana (masterhuds) wengi tupate somo.
 
You cannot change anybody especially a man...only God. Advise...its you to change. Believe me it works.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…