Tajiri wa matajiri
Senior Member
- Apr 17, 2024
- 166
- 649
Nimemfumania zaidi ya mara 3 na kumsamehe. Tuna mtoto mmoja, lakini bado hataki nimuoe.
Nina miaka 37 na niko kwenye mahusiano na huyu dada kwa miaka 12 sasa. Yeye ana miaka 35, ni mwanamke ambaye nampenda sana, lakini katika kipindi chote cha mahusiano nimepitia mambo mengi sana kiasi kwamba nimefika mahali nimeshakatishwa tamaa. Kipindi tulipoanza mahusiano nilimkuta akiwa na mwanaume mwingine, alikuwa akim*piga sana na kumdhalilisha, na mara nyingi alikuwa akimfanyia vitendo vya ajabu hadi kumuingilia kinyume na maumbile.
Kipindi hicho, alikuwa rafiki yangu, alikuwa ananiambia kila kitu. Nilimuonea huruma nikaingia naye kwenye mahusiano, nikamsaidia hadi akaachana na yule mwanaume na tukawa tuko vizuri. Baada ya mwaka mmoja, kuna siku yule mwanaume alinipigia simu na kuniambia nimwache mwanamke wake, alinidhihaki sana na kibaya zaidi alikuwa anatumia simu ya mwanamke wangu. Alimpa simu mwanamke wangu na akaniambia hanitaki tena kashaniacha.
Niliumizwa sana lakini baada ya mwezi mmoja alinitafuta na kuniomba msamaha akisema haitajirudia tena. Alidai kuwa alikutana na mwanaume huyo akampa lifti na wakajikuta wameanza tena mapenzi. Nilimsamehe na tukakaa kwenye mahusiano kwa miaka miwili hadi nilipokuja kumfumania na mwanaume mwingine. Huyu mwanaume alikuwa baba mtu mzima na nilimfumania mpenzi wangu akimtumia picha za uchi, akijichezea. Nilipomuuliza aliniambia ni tamaa tu na kwamba yule baba hana nguvu yoyote ya kumkufanya chochote, ana kisukari. Nilimwambia sipendi, nikamuacha lakini baadae akaja kunambia kuwa ana mimba yangu.
Kweli tulipima na ikathibitika kuwa ana mimba. Nilidhani kuwa akizaa atabadilika, hivyo nilimsamehe tukaanza upya. Hata hivyo, mambo yalikuwa mabaya kipindi cha ujauzito, alikuwa hanitaki, ananiomba pesa lakini hataki tuonane. Hadi mtoto alipofikisha miaka miwili, alikuwa haruhusu hata nimwone mwanangu. Nilienda kwao na kuongea na mama yake, wakamkalisisha kikao, akaniruhusu kumuona mtoto, lakini maisha yaliendelea vilevile. Nilimwambia kuwa tuna mtoto, kwa nini tusifunge ndoa, akanijibu kuwa umri bado.
Baadaye nilikuja kugundua kuwa amerudiana na X wake ambaye sasa ni mume wa mtu na niligundua baada ya mke wa huyo mwanaume kunitafuta na kunitumia ushahidi wa picha zao wakifanya mapenzi na meseji wanazochat. Nilipomwambia akaanza kunitukana sana, akaniambia hanitaki tulee mtoto na mambo ya mapenzi basi. Wakati huo nilikubali kwani na mimi nilikuwa tayari nimeshaingia kwenye mahusiano mengine.
Nilipata mwanamke mwingine ambaye alikuwa ananijali, ananionyesha upendo na alikuwa kila kitu kwangu. Nilienda kwao kujitambulisha, nikatoa mahari lakini X wangu aliposikia nataka kuoa, alimtafuta huyo mwanamke na kum*tukana sana akimwambia huyo ni mume wangu. Alirudi kwangu kwa lazima, akahamishia vitu vyake mpaka sasa tunaishi pamoja.
Ni miezi 9 sasa, nililazimika kumwacha yule mchumba wangu lakini tatizo ni kuwa huyu mwanamke kila nikimwambia kuhusu ndoa ananiambia bado. Umri umeenda, sijui nifanye nini. Je, ni mtu anayenipenda kweli au? Miezi 9 hii sijawahi kumfumania tena ila suala la ndoa ndio hataki, naomba ushauri wako!