Nimemkumbuka golikipa Mosses Mkandawile

Nimemkumbuka golikipa Mosses Mkandawile

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Mosses Mkandawile alikuwa golikipa wa Simba, kipa huyu alikuwa akiwaudhi sana mashabiki wa Simba kwa namna alivyokuwa akifungwa magoli ya hovyo.

Lile goli alilofungwa Ayoub Lakred kule Ndola, Mkandawile alikuwa akifungwa zaidi ya yale, Mkandawile nilikuwa nikimshuhudia sana akifanya mazoezi pale uwanja wa Taifa B, nyuma ya uwanja wa Uhuru kulikuwa na uwanja ukiitwa Taifa B, wengi mliozaliwa miaka 2000 mkiambiwa mnatukana mara umesimuliwa.

Mkiambiwa ukweli mnabisha, mkiambiwa uongo ndio wale wale, basi ili mradi t.Sisi wengine hutudanganyi na soka la bongo, tulikuwa tunakwenda kucheki Sigara vs Pilsner, ilikuwa sio mchezo huko.

Huku kuna Idd Msigala mara Said Mrisho Zicco wa Kilosa kule sigara kulikuwa na akina Rashid Mmanga, Joseph Katuba ambaye ni marehemu, George Lucas Gazza.
 
Kama umeelewa ulichoandika wewe mwenyewe tufafanulie.
 
Kwakweli Mkandawile sikubahatika kumwona akicheza. Ila Joseph Katuba niliwahi kumwona akidakia Yanga na baadae Simba.

Wakati huo nilikuwa mwokota mpira kwenye mazoeazi ya timu kubwa na hata mechi. Enzi zile waokota mipira tulikuwa tunaitwa 'Chipukizi' maana karibia wote tulikuwa tunatokana na vijana wadogo wa CCM (Chipukizi). Na hata kwenye kuokota mipira hatukuwa na jezi za kimichezo kama leo, bali sare ya CCM (juu kijani, chini nyeusi). MSINISHANGAE, MAANA HATA YANGA WAKIFUNGA WALIKUWA WANASHANGILIA "CCM! CCM! CCM!" 😂🤣
 
Moses Mkandawire bila shaka alikuwa na asili ya Malawi yule.
 
Kwakweli Mkandawile sikubahatika kumwona akicheza. Ila Joseph Katuba niliwahi kumwona akidakia Yanga na baadae Simba.

Wakati huo nilikuwa mwokota mpira kwenye mazoeazi ya timu kubwa na hata mechi. Enzi zile waokota mipira tulikuwa tunaitwa 'Chipukizi' maana karibia wote tulikuwa tunatokana na vijana wadogo wa CCM (Chipukizi). Na hata kwenye kuokota mipira hatukuwa na jezi za kimichezo kama leo, bali sare ya CCM (juu kijani, chini nyeusi). MSINISHANGAE, MAANA HATA YANGA WAKIFUNGA WALIKUWA WANASHANGILIA "CCM! CCM! CCM!" [emoji23][emoji1787]
Nimecheka kama mazuri ila popote ulipo kula heshima yako kaka mkubwa
 
Mkandawile alianzia kuchezwa timu inaitwa Avengers, hiyo timu ilikuwa Kama tawi la Simba kwani wachezaji wengi wa Simba walipitia hapo.
Katuba alianza kuchezwa Sigara Kisha Simba baadae akamalizia mpira yanga.
Waliokufa wanaokota mpira ni skauti na Wala sio chipukizi.
 
Alex nakubaliana na ww asilimia 100, avengers ndio alitokea Mosses Mkandawile, hata marehemu All Machela
 
Alex nakubaliana na ww asilimia 100, avengers ndio alitokea Mosses Mkandawile, hata marehemu All Machela
Machela ilikuwa Temeke rangers, walikuwa wanafanya mazoezi Taifa b. Huyu jamaa alikuwa na mashuti makali na alikuwa akichezea vizuri akiwa pekupeku. Temeke Rangers ilikuwa pia Kama tawi la SIMBA. Ramadhani Lenny, Edward Chumila, Twaha Hamidu wore walitokea huko.
 
We unaongelea Temeke Squad sio Temeke Rangers, hakuna Temeke Rangers, Ramadhan Lenny na Edo wote wameishi mtaa wa njinjo pale Bulyaga Temeke, mm naongelea Avengers ilikuwa inatumia uwanja wa Taifa B, Mkandawile alikuwa akifanya mazoezi na baadae Marehemu Ally Machela
 
Back
Top Bottom