katoto kazuri
JF-Expert Member
- Feb 10, 2018
- 6,124
- 5,745
Nimekumiss wangu sana zamani tulipokuwa tunaandikiana barua za upendo kama hizi,
Uhali gani mpenzi ,
Tokea mchana sijakuona ,
Umeshindaje,,,,, wangu .
Moyo wangu ulikuwa mzigo na wasiwasi wangu ni hadi nikuone wewe,moyo wangu ni mwepesi pale nilipokuona wewe , mzigo uliokuwa moyoni umeutua baada ya kusikia sauti yako .
Busu lako ndio faraja yangu, ukinikumbatia mwili wangu huchangamka na kuwa maridadi shuleni nafurahia masomo na mara ingine nakutaja wewe.
Je wakumbuka nilivyoadhibiwa kisa wewe??
Je unakumbuka nilikubali adhabu ya kuchimba kisiki kisa mwalimu alifuma barua yetu.
Katoto kazuri nakupenda sana natamani uwe mke wangu ukubwani.
Nishirikiane nawewe kulea watoto wetu kwa furaha .
Una Macho ya kurembua na kudunduliza mpenzi wewe unanipaga raha sana napagawa.
Marashi yako yananifanya niote niko bustanini nawewe tukisikia harufu za maua mbalimbali yaliyomo bustanini.
Cheko lako lanipa raha pale nisikiapo lanifariji kiasi cha mimi kuendelea kusikia sauti yako.
Kwani sauti yako ni nyoronyoro na humtoa nyoka pangoni.
Katoto kazuri nakupenda sana.....
I love u chukua ua hilo ndani ya hii barua kila unusapo ujue nakupenda .
Je yako ilikuwaje??
Tuambie kwa maana nimemmis sana huyu kaka aisee alikuwa one of the kind .......😍😘😘😘😘🤩🤩 Musah
Dedication hii kwake jamani