Nimemmiss sana, Hayati John Pombe Magufuli

Watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri Na wanyonge ndio wanammis mwendazake
 
Ume miss zile habari za kuopolewa miili ya watu kwenye viroba ndiyo maana huna hamu tena ya kuangalia taarifa ya habari!
 
Umesema ukweli kabisa.magufuli ndiyo rais ambaye alitufaa watz wengi ukiwatoa mafisadi kama kikwete walichukia sana.kipindi hicho mtanzania yeyote alianza kusikiliza taarifa ya habari kufatilia miradi mingi aliyokuwa akizindua ya kuwanufaisha wtz.Tofauti na Sasa Kila kitu Kiko hovyo chini ya huyu mama Yao.
 
Umuhimu wa mtu akiondoka
 
Fanya kazi...penda familia yako kwanza...dunia ni mapito....nchi inaendeshwa kwa mifumo..hata huyo makonda aboreshe taasisi iwe imara...peke yake hatoweza
Who is makonda mpaka aboreshe mifumo,RC ni karani tu bora mbunge ni mfanya maamuzi sio rc
 
Hayupo tena ni udongo Tu sasa..
Usiweke matumain Kwa wanadamu wanakufa ...
 
Yule jamaa alikuwa na amsha amsha ya kipekee.. Leo kafungua hiki kesho kaanzisha mradi huu. Hujakaa sawa katumbuliwa mtu mara kule katenguliwa yule.. Kidogo mashirika yamepeleka gawio la faida Dah..

Kwangu Mimi atabaki kama Nabii aliyekuja Tanzania kutufundisha jinsi Rais anavyotakiwa kufanya kazi.. Akamaliza miaka yake mitano huyooo kaenda zake.. Kazi kwetu.. Tufate aliyotufundisha au turudi kulekule.. Bahati mbaya sana tumeamua kurudi kulekule..

Moyoni mwangu Magufuli hajafa.. Anaishi milele.. Nimebakisha picha yake tu kwenye screen saver za simu zangu na Computer angalau nimuone kila siku..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…