Nimemnyang'anya 'beki tatu' simu, je nimekosea?

Nimemnyang'anya 'beki tatu' simu, je nimekosea?

umefanya sawa,kila nyumba inamasharti yake!
 
It seems members wengi (wakiume) house-girls ni "chakula yao" - Kwa kutumia posts hizo hapo juu

Narudi Kaunta!
 
Mfanyie maombi atokwe na mapepo ...........mwambie Go... And Sin No MoreJohn 8:3-11
 
[/COLOR]Mkuu nilikuuliza maswali 4 lakini hujayajibu,kama simu ni kwa mawasiliano ya kujenga basi ungemjenga kwanza beki tatu wako juu ya matumizi bora ya simu pasi na kumnyang'anya.
Kwenye red:Inaonekana beki tatu wako kuchukuliwa inakuuma sana,kunani mwenzetu???

Mbona nilikwambia nilishamuimbia hayo yote uliyouliza, huenda huna uzoefu wa kukaa na hawa beki tatu mkuu. Kama una familia na watoto nadhani ungeweza ku imagine hatari iliyopo mbele ya watoto. Ni kubwa zaidi ya hilo la simu. Hebu imagine unarudi kutoka kazini then unakuta mtoto wako wa miaka miwili au mitatu anaangalia ponographic films na kivula usichokijua pamoja na beki tatu nadhani unaweza kupata picha hapo. Na haya yanatokea, huwa hawajali sana hawa beki tatu na kuna jamaa yangu ilishamtokea hii ingawa nashukuru haijanitokea mimi.

Ushauri wangu kwenu usikalie kimya jambo lolote lisilo la kawaida ukilihisi au kulisikia from your neighbours. Watch out mkuu, ila ukikua utajua tu
 
sai bure kuna namna, labda umekazimikia bhana, kuwa muwazi tu, ulirudi home ukamalize ishu kufika ukakuta kidume kingine ila kwasababu wewe una mamlaka ukaamua kutumia mamlaka yako juu yake vibaya....sawa bhana ila jua na yeye ni binadamu kama wewe hizo ni pilika[pilika za maisha tu
 
Hawa wasichana wa kazi nao balaa tu, mimi ilishanitokea hiyo, tena wa kwangu hakuwa hata na simu, alikuwa anapika wanakula wanafanya mambo yao humohumo ndani, nilichofanya siku hiyo niliyomshika nilimrudisha kwao siku hiyo hiyo, kwa umri wa huyo wa kwako (25yrs) ni mdada mkubwa huyo chakufanya mrudishie simu yake ila ukae nae chini uongee nae umwambie tabia ya kuleta wanaume ndani sio nzuri na umwambie hali halisi ya dunia ilivyo magonjwa n.k lakini mpe uhuru angalau jumapili moja unamruhusu anatoka out kidogo kama ataenda kukutana na vidume vyake huko ni yeye mwenyewe
 
nilishamuimbia nyimbo zote unazozijua wewe kuhusiana na hii kitu. Na ndiyo maana wikiend yeye huwa anapata off ya kwenda mjini kutembea nikiamini huko ndo angemalizia hizo hamu zake. Nadhani amenogewa au huenda hao bf wake hawana uwezo wa kwenda guest ndiyo maana wanakuja kumalizana naye kwangu. Unajua kwako wewe unaona sawa beki tatu akifanyia mapenzi ndani ya nyumba yako ila mimi nadhani hiyo si sawa kabisa, binadamu tuko tofauti na ktk hili tumetofautiana
hujanielewa mkuu!! Hakuna anaesema ama anmbae angependa nyumbani kwake kugeuzwe dangulo!! Nnachokizungumzia mm ni ww kumnyanganya simu kama adhabu ! Kakushindwa kitabia mrudishe kwao tafuta mwingine! Lakini sio kumpiga na kufanya umfanyiayo!
 
umemkosea heshima.hebu fikilia wewe boss wako akunyang'anye simu utajiskiaje.kama umemchoka mrudishe kwao kuliko kumnyanyasa kwa vitu vodogo vidogo.kwani nyie ndo mtamuoa?.au hamtaki awe na malafiki.kwani yeye mfungwa?.acheni ukilitimba.mia

yaelekea limekugusa sana hili mkuu ndio eneo la mawindo yako nini..................

Wote mnaomsakama huyu mnatambua kuwa pamoja ni kuwa mfanayakazi lakini akishakuwa ndani ya nyumba anahesabiwa kama mtoto wa familia? hebu chukulia ni binti yako....................ungechukua hatua zipi
 
Yuko mama mtanzania kafungwa jela juzi Uingereza kwa sababu ya mambo haya haya ya kunyanyasa mtumishi wa ndani.
Ndugu zangu u hausgel ni ajira kama zilivyo ajira nyingine,hivyo zina miiko yake kwa mwajiri na mwajiriwa.Nchi hii sijawahi kusikia ajira inayosema mwajiri akae na simu ya mwajiriwa hadi atakapoenda likizo.Wajuzi wa sheria za kazi jamani nisaidieni.
by the way Mkuu mrusha uzi,huyo hausgel unamlipa sh ngapi kwa mwezi?
 
  • Thanks
Reactions: bht
hujanielewa mkuu!! Hakuna anaesema ama anmbae angependa nyumbani kwake kugeuzwe dangulo!! Nnachokizungumzia mm ni ww kumnyanganya simu kama adhabu ! Kakushindwa kitabia mrudishe kwao tafuta mwingine! Lakini sio kumpiga na kufanya umfanyiayo!

Baba siku zote anakuwa na huruma na hg,
kama baba yuko hivi mama atafanyaje,
but ngojea mavuno yako na utayaona.
 
Hivi Rebecca tayari ameshafungwa, kesi yake niliisikia

Yuko mama mtanzania kafungwa jela juzi Uingereza kwa sababu ya mambo haya haya ya kunyanyasa mtumishi wa ndani.
Ndugu zangu u hausgel ni ajira kama zilivyo ajira nyingine,hivyo zina miiko yake kwa mwajiri na mwajiriwa.Nchi hii sijawahi kusikia ajira inayosema mwajiri akae na simu ya mwajiriwa hadi atakapoenda likizo.Wajuzi wa sheria za kazi jamani nisaidieni.
by the way Mkuu mrusha uzi,huyo hausgel unamlipa sh ngapi kwa mwezi?
 
Umefanya vyema kuwatimua hao Vijana, wengine wanakuwaga wezi, wanaweza kuchora raketi ya wizi, Ila Simu mrudishie na umpige Marufuku kuleta watu nyumbani kwako.Akirudia mrudishe kwao.

Ukipata muda ongea naye vizuri kuhusu hathari za ngono isiyo na mpango,Pia kubeba Mimba zisizo na Mpango Na akuelewe kuwa sio tabia nzuri kuingiza wanaume ndani.Na kuhusu Simu Wakati mwingine inaweza tokea dharura na yeye hana mawasiliano na wewe itakuwaje sasa?
 
mkuu kitendo ulichofanya si sahihi ... mtake radhi huyo binti na kuwa mbali naye .. cha msingi mwambie mkeo aongee nae amweleweshe nini kinatakiwa na asisahau kutumia makaratasi ... maana iko siku atakuja kumweleza mkeo unamtongoza
 
  • Thanks
Reactions: bht
hyom ishu seriouz hatukatai ana haki ya ku do na hao vidume wake lakini sio kwako,ni risk sana aseee,wizi,na hata kukla angekuwa anakula nao utashangaa unga haukai stooo mara sukari imeisha,tumbafu sao
 
yuko kwa age ya 25yrs

sasa mbona unamfuga kama mnyama? binti mkubwa kabisa huyo.
unadhani yeye hana mahitaji ya kimwili kama binadamu mwingine yeyote? mrudishie simu yake na mpe uhuru wake akafanyie mambo yake kwingine. mwambie tu hutaki afanyie kwako. sasa asiwasiliane na mtu wake kwani hana haki ya kupenda na kupendwa? una mapango wa kumfanya mke wa pili?

acha kabisa ndyoko, mm nikikupata kama wewe namsaidia binti kukufungulia mashtaka!!!

sikujua ukiwa msaidizi wa nyumbani unaforsake some of your rights as a human being!!!!!!!!!
 
hujanielewa mkuu!! Hakuna anaesema ama anmbae angependa nyumbani kwake kugeuzwe dangulo!! Nnachokizungumzia mm ni ww kumnyanganya simu kama adhabu ! Kakushindwa kitabia mrudishe kwao tafuta mwingine! Lakini sio kumpiga na kufanya umfanyiayo!

kama ulisoma vizuri ni kile kidume ndo nilikichapa makofi sio beki tatu
 
Yuko mama mtanzania kafungwa jela juzi Uingereza kwa sababu ya mambo haya haya ya kunyanyasa mtumishi wa ndani.
Ndugu zangu u hausgel ni ajira kama zilivyo ajira nyingine,hivyo zina miiko yake kwa mwajiri na mwajiriwa.Nchi hii sijawahi kusikia ajira inayosema mwajiri akae na simu ya mwajiriwa hadi atakapoenda likizo.Wajuzi wa sheria za kazi jamani nisaidieni.
by the way Mkuu mrusha uzi,huyo hausgel unamlipa sh ngapi kwa mwezi?

Namlipa 50,000 kwa mwezi. vipi nimuongezee?
 
hyom ishu seriouz hatukatai ana haki ya ku do na hao vidume wake lakini sio kwako,ni risk sana aseee,wizi,na hata kukla angekuwa anakula nao utashangaa unga haukai stooo mara sukari imeisha,tumbafu sao

Mkuu hayo yote nili ya consider na ndiyo hatari kubwa nnayoiona mbele yangu. Ntawaambia uamuzi ntakaoufanya. Kwa kuwa anaenda likizo next month, nadhani ntafanya maamuzi wakati huo huo anaoenda kwao. Ngoja kwanza nimlie timing ya kuchinja kobe nione kama amejirekebisha
 
Back
Top Bottom