ulitaka kumuacha mkiwa chuo lakini kwa huruma ukaendelea nae ili asiache chuo. Mlipomaliza chuo mkapangwa mikoa tofauti, kilichokufanya uendelee nae ni kitu gani tena? yaani mko mikoa tofauti lakini bado uhusiano unaendelea tena na mtu usompenda. unalo hilo, umelikoroga, linywe kaka yetu kwa roho moja. alikusitiri sana mkiwa chuo usihangaike hapa na pale. kwanza unajikanyaga hata hujui unataka nini, mara simtaki, mimba isitolewe, hutaki kuzaa watoto na mama tofauti, sasa ili usizae watoto wa mama tofauti, muoe.
usisahau kutuchangisha michango ya harusi.