Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,931
- 24,816
Huyu mdogo wangu wa kike wa mwisho ana kitoto chake kina miaka 6. Weekend hii alikileta kije msalimia uncle. Mi sikuona shida kabisa. Wazo lilikuwa jema.
Shida ikawa kwenye utekelezaji. Kile ki uncle kina kera balaa... Kinakera mpaka mwisho. Kimefika home ndani ya muda mfupi kimeshaingia vyumba vyote, kimechafua kwenye friji na kimeshavunja jug la juice.
Mi niliweka pause tu kwanza kuvumilia nikiomba Mungu asaidie wageni waondoke haraka. Kikaanza kulilia remote kiangalie tamthiliya za A**m. Mimi nilishapiga marufuku pale home. Nikakikatalia ...kikaanza kulia. Mama yake anakimbembeleza....
Hakitaki kikamrushia remote usoni. Hapo nilitaka kunyanyuka....malaika akanizuia. Mama yake akawa tu anasema "Jamaani... Amran na hasira kama baba yake....yaani huyu mtoto" huku anajichekesha akifikicha fikicha jicho.
Nikainuka nikaichukua remote nikaijaribu nikaona inafanya kazi. Nikashusha pumzi kumshukuru Mungu maana nilijua pale hali ya hewa ingechafuka.
Kakawa kana mghasi sana mwanangu....uzalendo ulinishinda kalipomwambia "mshenzi weeee" hapo nilijikuta nimeamka nikakamata na kukapeleka uani. Nikavunja ua langu zuri maskini nipate fimbo. Nilikatandika sana... Heeehhh .... Si kanalia kananambia ... "Toka hapa...." Nikaona haka kametumwa kunitafutia kesi na Serikali au ustawi wa jamii....
Nikakacharaza viboko miguuni, mamaa yake akaja ...na kudai inatosha nitamuumiza mwanaye si vizuri kumchapa mtoto, inatakiwa kukaa naye kuongea naye.
Nilimwambia hilo la kukaa naye kuongea naye akafanyie huko kwao. Hapa kwa uncle katulie hasa. Mama yake ali mind. Eti....mtoto anapaswa apewe muda wa kucheza atakavyo. Nilimwambia akacheze huko ila asichezee vitu vyangu na sitaki kabisa uharibifu.
Akasema: "Kaka ndo maana wengi hatupendi kuja kwako ...mkoloni sana na hupendi watoto" alinikwaza....yaani yeye kukilea kitoto chake vile kama kimbwa koko anaona ndo mapenzi. Kitoto kina sugu, vidonda na kimekuwa cheusi, kimekauka kama kinakula cement eti ndo anakipenda nikasema wacha iwe hivyo.
Kimekaa kaa kidogo kwa utulivu kikajisahau tena ...kikajikojolea.... Mtoto wa miaka 6 anajikojoleaje? Mimi wangu ameanza kukojoa mwenyewe akiwa na miaka 2 huyu sita anakojolea carpet?
Mama yake anasema ndo alivyo yaani ...ukichelewa tu kumvua nguo anajikojolea hapendi kukaa na mkojo. NIlimwita mtoto wangu nikamwambia niitie dada. Dada alipokuja nikamwambia kanichumie fimbo.
Sister akaamua akachukue katoto kake akakapeleka kwenye gari kukaepusha na dhahama. Wakaamua kuondoka. Nikasema na iwe hivyo...alaaaah yaani kafanye ujinga nikaogope sababu ya mama yake.....sister kawaambia wadogo zangu wengine kuwa nime mnyanyasa mtoto wake. Ndugu wananisema....mama akapata taarifa.
Akanipigia simu kuwa nimefanya swadakta kile kitoto kinalelewa hovyo. Mama yake anakikiss mpaka ulimi.....anasema ndo mapenzi kwa mtoto. Mama anasema hataki hata kikamtembelee kilimtia hasara nyingi ikiwepo kudumbukiza simu yake majini.
Nimejisemea tu wacha na iwe. Asiyefunzwa na mamaye sisi tutamfunza tu ...