Hongera zako mkuu kwa kumpa malezi bora,inaonekana dogo alikuwa amepinda Kweli kweli
Mtoto alipinda aisee. Siku moja huwezi kuamini washkaji wamekuja kunitembelea, ile tumekaa tunapiga stori eti dogo kaanza kuwatoa kwenye kochi ili acheze.
Nilivyojaribu kumzuia nyumba ikalipuka kwa fujo za dogo. Kwa kweli huyu mwanangu wa kufikia aliharibikiwa.
Mama alimuogopa mtoto, asingeweza kwenda naye popote kwa kuogoga aibu mbele za watu. Nilichokifanya ni kujiwekea mpango kazi hatua kwa hatua, nikampa mama maelekezo. Nilivyomaliza kuweka nidhamu, nikaanza sasa kumpa mama silaha.
Yaani dogo asinisikilize tu ila mama yake pia, napo nikafanikiwa maana niliona kuna uwezekano dogo akaniheshimu ila akampuuzia mama yake na watu wengine.
Hapa nilimpa mama masharti magumu, hata nisipokuwepo dogo akileta fyongo lazima nifahamishwe, na ikiwezekana napigiwa simu dogo akisikia. Alivyoona amebanwa kila kona, alisalimu amri.
Sasa hivi nataka sasa kuingia hatua ya kujenga mahusiano ya kirafiki jambo ambalo sikutaka kufanya mwanzoni baada ya kugundua alichukulia kama mimi ni rika yake vile so ilibidi niwe mgumu, mipaka ilibidi iwepo ili kusimika nidhamu.
Nakuhakikishia, siyo kazi rahisi aisee, imenichukua karibia miaka miwili kumnyoosha dogo.
Sasa hivi mama yake anafurahi na ananitunuku vizuri hasa.