Nimempiga mtoto wa mdogo wangu, ndugu wananilaumu lakini Mama ananiunga mkono

Nimempiga mtoto wa mdogo wangu, ndugu wananilaumu lakini Mama ananiunga mkono

Mzee bora huyo. Aisee mimi mke wangu wapili si nilimkuta na mtoto wa kiume. Pumbavu zangu. Dogo alikuwa ni nunda hatari, alikuwa anamkata mama mikwara kwa kwenda mbele, anaamua yeye kila kitu na alipojichanganya eti akasema yeye ndo mwenye maamuzi ya tunachotakiwa kufanya.

Pumbavu, dogo siku moja kanitunishia misuli kama vile anataka kupigana na mimi. Nilichofanya nilimpa wiki kama tatu hivi namsoma tu taratibu. Mama yake anamuogopa dogo plus aibu. Yaani dogo alikuwa ni kufoka tu, hasikilizi chochote. Mtoto wa kiume mama miaka sita eti mama anambeba kama wa mwaka mmoja.

Nilipoanza kazi, alisoma namba. Nilijisemea eti namkaza mama yake alafu anitunishie misuli. Daadeki, leo akisikia nimekohoa anakimbia tu. Single mothers wanaharibu watoto sana.

Siku hizi dogo anajielewa freshi kweli. Ni baada ya mimi kusimamia show kama mwanaume. Ila ajabu sikuwahi kumchapa hata siku moja.
Kama hukumchapa ulimfanyaje mkuu?

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Wakati nakuwa wazaz. Wangu walikuwa wababe San bas nikiwazingua tu ukikatwa jicho aise moja kwa moja unajuwa mzee kamaind hvyo niache upuuzi wowte hapo na mgeni akiondoka nitapigwa tu hat Kama. Ni kosa dogo eti nimelia au kula chakula mbele ya wageni aise nitapigwa
 
MAKOSA 30 AMBAYO WATOTO WA ZAMANI WALIKUWA WAKILA BAKORA!!
WATOTO WA ZAMANI TULIISHI MAJUMBANI KAMA TUKO MAFUNZO YA JESHI!! UKIKUA NI FULL ADABU KUHESHIMU WATU, UTU, BUSARA NA KUJITETEGEMEA UKIWA NA UMRI MDOGO TU
1: Usiposalimia wakubwa asubuhi unapigwa
2: Usiposalimia wageni unapigwa
3: Ukinawa kabla ya wageni unapigwa
4: Ukilia bila sababu unapigwa
5: Ukinyanyuka wakati wa kula kabla ya wakubwa kuinuka unapigwa
6: Wakubwa wakiwa wamekaa wewe ukaenda kusimana pembeni unapigwa
7: Ukikaa wakubwa wamesimama unapigwa
8: Ukitumwa dukani ukachelewa kurudi unapigwa
9: Ukichelewa kurudi toka shuleni unapigwa
10. Ukiwahi kurudi shuleni unapigwa
11: Ukililia wageni wakati wanaondoka , wakitoka unapigwa
12: Kujipitisha pitisha wageni wakiwa wanakula unapigwa
13: Kujibu ovyo wakubwa unapigwa
14: Kutukana watu wazima, watoto au rika lako unapigwa
15: Ukiwa mbishi bila sababu unapigwa
16: Ukipigwa ukalia unapigwa ili unyamaze
17: Ukipigwa umenyamaza unapigwa ili ulie
18: Ukipigwa shuleni ukaenda kusema nyumbani, unapigwa
19: Ukianza kula nyama kabla ya wakubwa unapigwa
20: Ukila kwa jirani ukabainika unapigwa
21: Ukianza kunawisha wenyeji badala ya wageni mkimaliza kula unaitwa chumbani unapigwa
22: Ukianza kunawisha watoto badala ya wakubwa unapigwa
23. Ukikutana na mtu mzima ana mzigo hujampokea unapigwa
24. Ukienda kusema kama umepigwa unapigwa.
25. Mtu mzima akipita kama mnacheza hamjamshughulikia unapigwa.
26. Ukienda nyumba za watu, ukaona kitu au ukasikia story ukaileta nyumbani unapigwa
27. Ukipewa hela na mtu asiefahamika au hata anaejulikana inategemea mazingira gani unapigwa
28. Ukianza kuchagua chakula hiki nakula hiki sili unapigwa
29. Ukianza kuwa na marafiki wasioleweka makwao unapigwa
30. Mtu mkubwa akija kukuchongea nyumbani hata kama sio cha ukweli unapigwa.
YAANI YALE MAISHA! Acha kabisa.
...... Wahenga, hapo vipi???......[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Miaka 10 iliopita nimekuja dar kuanza chuo nikafikia kwa aunt yangu anawatto wawil miaka 3 na 7 aseeh walikuwa vipegesi balaaa nilipewa chumba cha uani wao wanakaa nyumba kubwa

Mwanzon nilichukulia hali ya kawaida ila kadri siku zinavyo enda nikaona wanazidi kunipanda kichwan baba yao hashind nyumban anarudi usiku saa 5 huko kila siku mama yao hivyo hivyo isipokuwa jpili anashinda home tena anajifungia chumban huko

Watto muda mwing wanashinda na dada wa kaz wanamsumbua na kumpelekesha hatari akiwapiga mama akiambiwa anakuwa mkali balaa kuna siku nipo zangu chumban nasikia yule mtto mkubwa anamuambia dada TOKA HAPA KWETU MASKINI WEWE natoka namuona anachukua viatu anamrushia nilichukua mkanda wa suruali nilimshika nilimchapa sana akatishia kusema kwa mama yake uzur mama yake anajua mm nilivyo kwel mama yake karudi ule usiku akanisemea nikatoka taratibu kuchukua mkanda nikamshika mbele ya aunt nikatandika tena nilijitahid ile semister ya kwanza wale watto wakanyooka nilibatizwa jina na kuitwa kaka mikanda mpaka sasa wanajielewa wamekuwa watu wakubwa sasa wananipenda sana na mm nawapenda pia
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Hakitaki kikamrushia remote usoni. Hapo nilitaka kunyanyuka....malaika akanizuia. Mama yake akawa tu anasema "Jamaani... Amran na hasira kama baba yake....yaani huyu mtoto" huku anajichekesha akifikicha fikicha jicho.

Nimejisemea tu wacha na iwe. Asiyefunzwa na mamaye sisi tutamfunza tu ...
Pole sana ila nasikitika kukujulisha kuwa mtoto ulimuonea hakustahili kupigwa.

Hapa ulitakiwa utandike mama mtoto makofi ya maana sana; halafu wakati huo unamwambia aongoze njia kurudi nyumbani kwake akamlete na baba yake mtoto kama kuna uwezekano. Pole sana
 
Safi kabisa ww ni km wajomba zangu yaan ulikua ukifanya ujinga kichapo utakacho pata hata kwenda kusimlia home huwezi ..sasa hivi watoto wanalelewa km mayai ....
Huyu mdogo wangu wa kike wa mwisho ana kitoto chake kina miaka 6. Weekend hii alikileta kije msalimia uncle. Mi sikuona shida kabisa. Wazo lilikuwa jema.

Shida ikawa kwenye utekelezaji. Kile ki uncle kina kera balaa... Kinakera mpaka mwisho. Kimefika home ndani ya muda mfupi kimeshaingia vyumba vyote, kimechafua kwenye friji na kimeshavunja jug la juice.

Mi niliweka pause tu kwanza kuvumilia nikiomba Mungu asaidie wageni waondoke haraka. Kikaanza kulilia remote kiangalie tamthiliya za A**m. Mimi nilishapiga marufuku pale home. Nikakikatalia ...kikaanza kulia. Mama yake anakimbembeleza....

Hakitaki kikamrushia remote usoni. Hapo nilitaka kunyanyuka....malaika akanizuia. Mama yake akawa tu anasema "Jamaani... Amran na hasira kama baba yake....yaani huyu mtoto" huku anajichekesha akifikicha fikicha jicho.

Nikainuka nikaichukua remote nikaijaribu nikaona inafanya kazi. Nikashusha pumzi kumshukuru Mungu maana nilijua pale hali ya hewa ingechafuka.

Kakawa kana mghasi sana mwanangu....uzalendo ulinishinda kalipomwambia "mshenzi weeee" hapo nilijikuta nimeamka nikakamata na kukapeleka uani. Nikavunja ua langu zuri maskini nipate fimbo. Nilikatandika sana... Heeehhh .... Si kanalia kananambia ... "Toka hapa...." Nikaona haka kametumwa kunitafutia kesi na Serikali au ustawi wa jamii....

Nikakacharaza viboko miguuni, mamaa yake akaja ...na kudai inatosha nitamuumiza mwanaye si vizuri kumchapa mtoto, inatakiwa kukaa naye kuongea naye.

Nilimwambia hilo la kukaa naye kuongea naye akafanyie huko kwao. Hapa kwa uncle katulie hasa. Mama yake ali mind. Eti....mtoto anapaswa apewe muda wa kucheza atakavyo. Nilimwambia akacheze huko ila asichezee vitu vyangu na sitaki kabisa uharibifu.

Akasema: "Kaka ndo maana wengi hatupendi kuja kwako ...mkoloni sana na hupendi watoto" alinikwaza....yaani yeye kukilea kitoto chake vile kama kimbwa koko anaona ndo mapenzi. Kitoto kina sugu, vidonda na kimekuwa cheusi, kimekauka kama kinakula cement eti ndo anakipenda nikasema wacha iwe hivyo.

Kimekaa kaa kidogo kwa utulivu kikajisahau tena ...kikajikojolea.... Mtoto wa miaka 6 anajikojoleaje? Mimi wangu ameanza kukojoa mwenyewe akiwa na miaka 2 huyu sita anakojolea carpet?

Mama yake anasema ndo alivyo yaani ...ukichelewa tu kumvua nguo anajikojolea hapendi kukaa na mkojo. NIlimwita mtoto wangu nikamwambia niitie dada. Dada alipokuja nikamwambia kanichumie fimbo.

Sister akaamua akachukue katoto kake akakapeleka kwenye gari kukaepusha na dhahama. Wakaamua kuondoka. Nikasema na iwe hivyo...alaaaah yaani kafanye ujinga nikaogope sababu ya mama yake.....sister kawaambia wadogo zangu wengine kuwa nime mnyanyasa mtoto wake. Ndugu wananisema....mama akapata taarifa.

Akanipigia simu kuwa nimefanya swadakta kile kitoto kinalelewa hovyo. Mama yake anakikiss mpaka ulimi.....anasema ndo mapenzi kwa mtoto. Mama anasema hataki hata kikamtembelee kilimtia hasara nyingi ikiwepo kudumbukiza simu yake majini.

Nimejisemea tu wacha na iwe. Asiyefunzwa na mamaye sisi tutamfunza tu ...
 
Tupe na sisi mbinu mkuu

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app

Mkuu, watoto wanawasoma sana watu wazima. Kuanzia umri wa mwaka mmoja mpaka miaka mitano ni muda wa kujenga misingi na mipaka kwa watoto. Ukichelewa kwamba bado ni mdogo eti utamnyoosha akianza kuelewa, huwezi kufanikiwa.

Sasa wangu wa kufikia, naye niliona kwa kuwa ndo anaingia kwenye maisha yangu, ilibidi nimchoree mistari mingi.

Misimamo mikali sana, kuna wakati alitaka kutunisha misuli hapo ndo nilitumia nguvu kidogo. Nilikuwa nikimshika mikono nambana kama spana, kadiri anavyopambana ndivyo navyokaza. Matokeo yake akaja kugundua hana jeuri.

Pili nikiwa nikikngea naye namlazimisha akae sakafuni kabisa na ananyoosha miguu. Kama vile yuko jela, kisaikolojia nilikua namtoa kwenye reli aliyoizoea kwamba yeye ndo wa kuamua. Kwamba maamuzi ni yeye. Nikawa namfundisha kwamba kichwa ni mimi tu!

So hakuna njia moja bali kikubwa ni saikolojia, ila muhimu zaidi ukishaamua jambo libakie kuwa lilivyo. Consistency kwa watoto ni muhimu sana. Ukiwa unabadilisha msimamo kisa mtoto amelilia kitu, basi ujue umeshafli.
 
Kuna tuko sitakaa nilisahau nikiwa shule ya msingi miaka hiyoo

Nilimsonya mwalimu nikapelekwa ofisin nikala bakora za kutosha taarifa zikafika home mama kaambiwa nikalabakora mzee kaja usiku kaambiwa nikalabakora kesho yake kuna aunt yangu mtata kinoma alikuwa akija naona kifo kifo bana alivyokuja kahadisiwa kanishushia kipigo dahh maisha ya kipindi kile ni kijesh jeshi
 
Mtoto alipinda aisee. Siku moja huwezi kuamini washkaji wamekuja kunitembelea, ile tumekaa tunapiga stori eti dogo kaanza kuwatoa kwenye kochi ili acheze.

Nilivyojaribu kumzuia nyumba ikalipuka kwa fujo za dogo. Kwa kweli huyu mwanangu wa kufikia aliharibikiwa.

Mama alimuogopa mtoto, asingeweza kwenda naye popote kwa kuogoga aibu mbele za watu. Nilichokifanya ni kujiwekea mpango kazi hatua kwa hatua, nikampa mama maelekezo. Nilivyomaliza kuweka nidhamu, nikaanza sasa kumpa mama silaha.

Yaani dogo asinisikilize tu ila mama yake pia, napo nikafanikiwa maana niliona kuna uwezekano dogo akaniheshimu ila akampuuzia mama yake na watu wengine.

Hapa nilimpa mama masharti magumu, hata nisipokuwepo dogo akileta fyongo lazima nifahamishwe, na ikiwezekana napigiwa simu dogo akisikia. Alivyoona amebanwa kila kona, alisalimu amri.

Sasa hivi nataka sasa kuingia hatua ya kujenga mahusiano ya kirafiki jambo ambalo sikutaka kufanya mwanzoni baada ya kugundua alichukulia kama mimi ni rika yake vile so ilibidi niwe mgumu, mipaka ilibidi iwepo ili kusimika nidhamu.

Nakuhakikishia, siyo kazi rahisi aisee, imenichukua karibia miaka miwili kumnyoosha dogo.

Sasa hivi mama yake anafurahi na ananitunuku vizuri hasa.
Hongera kwa kutunukiwa vizuri mkuu [emoji3][emoji3]
 
Nimecheka sana yaan umenikumbusha niliwahi kualikwa sikukuu kwenye familia flani hivi ya kishua yaani kuna kitoto cha miaka mitatu pale kinasumbua balaa halafu wenyewe wanakilea kama yai[emoji1787]
Yaani wageni wote tuliokaa kwenye sofa bale sebureni tulipakazwa michuzi katoto hakatulii mara kanakufuata kanalazimisha katoe simu yako mfukoni mpaka kanalia kwa sauti ukikapa simu kanaitupa chini kanakupanda kwenye miguu kanaanza kuvuta tai yako shingoni kakitoka hapo kanaenda jikoni kanarudi kameshika nyama kanakuja kanakushika na ile michuzi yaani sebure nzima ilikuwa ni kero yule mtoto mpaka alipokuja kusinzia jioni ya saa kumi na moja ndo tukapumua ila tulikuwa hoi mie sikuenjoy kabisa niliaga mapema nikasepa kabla hakajaamka
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] ulijua kakiamka bado nipo hapa itakuwa balaa
 
Hii ya kulilia nyama ni tabia za kishenzi. Mimi kuna jirani yangu, wanae wawili huwa hawali pasipo nyama. Mtoto akikuta mboga nyingine anamwambia kabisa mama yake yeye hali anahitaji nyama. Mtoto ana miaka 8, anayemfuatia 5.

Watoto wakisema hivi wanaenda kununuliwa kuku au samaki. Nikajaribu kutafakar haya mazingira nikashindwa kuyaelewa kabisa.
Malezi mabaya eti wanalilia nyama kaahh!ujinga mtupu,malezi ya hovyo hovyo sio mazuri kabisa ndo maana siku hizi watoto hawatembei na hawajui ndugu zaidi ya wazazi wao tu maana wanalelewa hovyo hovyo hakuna anaeweza kuwalea zaidi ya baba na mama zao

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom