MAKOSA 30 AMBAYO WATOTO WA ZAMANI WALIKUWA WAKILA BAKORA!!
WATOTO WA ZAMANI TULIISHI MAJUMBANI KAMA TUKO MAFUNZO YA JESHI!! UKIKUA NI FULL ADABU KUHESHIMU WATU, UTU, BUSARA NA KUJITETEGEMEA UKIWA NA UMRI MDOGO TU
1: Usiposalimia wakubwa asubuhi unapigwa
2: Usiposalimia wageni unapigwa
3: Ukinawa kabla ya wageni unapigwa
4: Ukilia bila sababu unapigwa
5: Ukinyanyuka wakati wa kula kabla ya wakubwa kuinuka unapigwa
6: Wakubwa wakiwa wamekaa wewe ukaenda kusimana pembeni unapigwa
7: Ukikaa wakubwa wamesimama unapigwa
8: Ukitumwa dukani ukachelewa kurudi unapigwa
9: Ukichelewa kurudi toka shuleni unapigwa
10. Ukiwahi kurudi shuleni unapigwa
11: Ukililia wageni wakati wanaondoka , wakitoka unapigwa
12: Kujipitisha pitisha wageni wakiwa wanakula unapigwa
13: Kujibu ovyo wakubwa unapigwa
14: Kutukana watu wazima, watoto au rika lako unapigwa
15: Ukiwa mbishi bila sababu unapigwa
16: Ukipigwa ukalia unapigwa ili unyamaze
17: Ukipigwa umenyamaza unapigwa ili ulie
18: Ukipigwa shuleni ukaenda kusema nyumbani, unapigwa
19: Ukianza kula nyama kabla ya wakubwa unapigwa
20: Ukila kwa jirani ukabainika unapigwa
21: Ukianza kunawisha wenyeji badala ya wageni mkimaliza kula unaitwa chumbani unapigwa
22: Ukianza kunawisha watoto badala ya wakubwa unapigwa
23. Ukikutana na mtu mzima ana mzigo hujampokea unapigwa
24. Ukienda kusema kama umepigwa unapigwa.
25. Mtu mzima akipita kama mnacheza hamjamshughulikia unapigwa.
26. Ukienda nyumba za watu, ukaona kitu au ukasikia story ukaileta nyumbani unapigwa
27. Ukipewa hela na mtu asiefahamika au hata anaejulikana inategemea mazingira gani unapigwa
28. Ukianza kuchagua chakula hiki nakula hiki sili unapigwa
29. Ukianza kuwa na marafiki wasioleweka makwao unapigwa
30. Mtu mkubwa akija kukuchongea nyumbani hata kama sio cha ukweli unapigwa.
YAANI YALE MAISHA! Acha kabisa.
...... Wahenga, hapo vipi???......[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]