Nimempiga mtoto wa mdogo wangu, ndugu wananilaumu lakini Mama ananiunga mkono

Nimempiga mtoto wa mdogo wangu, ndugu wananilaumu lakini Mama ananiunga mkono

Huyu mdogo wangu wa kike wa mwisho ana kitoto chake kina miaka 6. Weekend hii alikileta kije msalimia uncle. Mi sikuona shida kabisa. Wazo lilikuwa jema.
kitoto = mtoto
chake = wake
kina = ana
alikileta = alimleta
kije = aje
shida imeanzia hapo kwa jinsi ulivyomuelezea huyo mtoto wa miaka 6.
 
Malezi ya watoto siku hizi yamekuwa shida sana watoto wanadekezwa kupitiliza mpaka inakuwa kero.
 
nimekupenda bure, hapo umemsaidia sana mama ake bila kujua

acha wakulaumu ila umefanya vyema.
 
Nililetewa mtoto wa sista nikae nae ameenda kozi ,kalikua kakojozi kameacha,kalikua hakajui hata kula kanalishwa mwenye kanakula sasa hivi tena anakula mpk wanamshangaaa,anacheza vzr na ananenepa.Mama ake haamini mtoto wa miaka 6 hajui chochote!

Kuna wazazi wanalea watoto kama hakuna kesho!!Mimi binafsi malezi ya kudekezq kizembe sinaga ,kuna Siku tumeenda kwenye sherehe kuna mtoto akawa analilia nyama jikoni wakawa wanamchekeq na wakampa..nilikaa kimya lakini nkasema moyoni angekua wangu angeimba aleluya!!!
Unanifaa sana wewe!!
 
Usimnenee mtoto wa mtu hivyo.
Halafu. Nini kitatokea?. Vitoto vingine vinalelewa vibaya sana. Kimojawapo ni hicho. Naamini hata wewe una malezi hayo ya digtal. Mtoto miaka 6 anajikojolea
 
Malezi ya wengi ni ya tamthiliya.........kuna shida sana Kwasasa
 
Mzee bora huyo. Aisee mimi mke wangu wapili si nilimkuta na mtoto wa kiume. Pumbavu zangu. Dogo alikuwa ni nunda hatari, alikuwa anamkata mama mikwara kwa kwenda mbele, anaamua yeye kila kitu na alipojichanganya eti akasema yeye ndo mwenye maamuzi ya tunachotakiwa kufanya.

Pumbavu, dogo siku moja kanitunishia misuli kama vile anataka kupigana na mimi. Nilichofanya nilimpa wiki kama tatu hivi namsoma tu taratibu. Mama yake anamuogopa dogo plus aibu. Yaani dogo alikuwa ni kufoka tu, hasikilizi chochote. Mtoto wa kiume mama miaka sita eti mama anambeba kama wa mwaka mmoja.

Nilipoanza kazi, alisoma namba. Nilijisemea eti namkaza mama yake alafu anitunishie misuli. Daadeki, leo akisikia nimekohoa anakimbia tu. Single mothers wanaharibu watoto sana.

Siku hizi dogo anajielewa freshi kweli. Ni baada ya mimi kusimamia show kama mwanaume. Ila ajabu sikuwahi kumchapa hata siku moja.
Ulifanyaje tupeane maujuzi....mitoto ya siku hizi kichomi sana
 
Hata kama umekwazika bado unatakiwa kuulinda utu wa mtu na heshima yake, sio "kile kitoto" ni "yule mtoto". Mtoto bado ni mtu na kuwa mtundu au kukosa adabu hakumuondolei heshima ya utu wake

Mkuu haya matukio ya hivi yapo karibu kila nyumba, kila mtu akiyaleta humu asijui patakuwaje. Hongera kwa kuwajibika kuwapa nidhamu watoto wenu na ndio jukumu lako kama mtu mzima, usilalamike pambana.
Mimi nimesoma lugha. Na hakuna neno hata moja nililokosea. Kile kitoto.
 
Back
Top Bottom