Nimemshauri mwanangu akimaliza tu masomo awe polisi

Nimemshauri mwanangu akimaliza tu masomo awe polisi

Mkuu watu wananeemeka, na uhakika wa maisha na usalama mwanzo mwisho, hakuna hata wa kuwagusa wewe na famikia yako yate, unataka nini zaidi ya hilo
unaneemeka kupitia manung'uniko ya watu unaona ni sawa?
 
Acheni masihara jamani, polisi wanaishi kwa raha sana inchi hii,
Nimeipenda sana hii kazi, mwanangu nakuusia tena, ukifuzu tu fanya kazi ya upolisi
Ila kumbuka pia kuwa maadili anayotakiwa kuwa nayo Polisi, ni sawa na yale anayotakiwa kuwa nayo Mtumishi wa Mungu kwenye nyumba ya Ibada; usahau hilo tafadhali
 
Kuna familia moja hapa Wilayani baba ni polisi mama ana kijibar hapa mtaani basi naye ni kama polisi vile kisa baba polisi sasa ole wako ulewe uzingue utajikuta kituoni, mtoto naye siku zingine anakaa bar majibu ya hovyooo kisa mtoto wa polisi basi naye polisi. Kifupi familia yote mapolisi naona na wewe umependa uwe baba wa polisi. Hongera
Usinikumbushe wkt tunasoma tulisoma na mtoto wa mkuu mmoja wa polosi. Sasa yeye enzi zile kila kitu chake anasema kanunua Mariedo.
Sasa kuna watu wengine wakawa wananunua hivyo hivyo Kariakoo na Mtumbani huko. Wakija wanamponda. Sasa yeye akisikia moto unawaka wanagombana.
Wakigombona anawaletea kigofu aisee miye asubihi nikisikia habari ya kigofu namwangalia yule dada kwa macho ya kuogopa sana.
Bora tulimaliza bwana aliwanyoosha sana wenzie na kigofu kile, mtoto wa polisi na yeye polisi aisee.
 
Kwa hapa nchini, hata police akiwa mwanao usimwamini wala usijiweke wazi sana kwake. Akiona kuna dalili ya pesa kwako anawasontea wahuni wenzake uliwa kichwa halafu huko mbelembele anakinga mikono anakatiwa chake.
Namwachia radhi
 
Back
Top Bottom