Nimemsikiliza Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) na mipango ya kuinua uwekezaji hakika nimefarijika sana

Kama ni hivyo, kwa nini DPW na TICTS zinagombea bandari ya Dar es salaam bila kuhusisha TIC? 😲
 
Wabongo vichwa maji sana! Makelele mengi vitendo zero!
 
Hakika, anastahili kuwa mahali alipo
 
Wawekezaji wa ndani wameshindwa kuwapa nishati ya uhakika umeme, ndio wataweza kuwavutia Wawekezaji wa nje waje kuwekeza?

NCHI YA AJABU KUWAHI TOKEA.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
Nchi hii imetoka mbali. Lazima tujifunze kureconize hata hatua chache kuelekea nyingi ambazo serikali imefanya. Kumbuka idadi ya watu waliounganishiwa umeme si sawa na Ile ya enzi za Mkapa pia matumizi yameongezeka na hivyo kuongeza changamoto ambayo kimsingi hatua zinaendelea kuchukuliwa siku hadi siku. Mwisho jielekeze katika kujikumbusha kuwa maendeleo ni mchakato.
 
Hakuna aliekataa, ila kwanini tunadanganywa kilasiku kuwa umeme utakuwa Stable na mwisho wa siku hamna kitu zaidi ya mgao.?

UKWELI NI JAMBO JEMA KWA WANANCHI, WATUAMBIE UKWELI.
 
Hakuna aliekataa, ila kwanini tunadanganywa kilasiku kuwa umeme utakuwa Stable na mwisho wa siku hamna kitu zaidi ya mgao.?

UKWELI NI JAMBO JEMA KWA WANANCHI, WATUAMBIE UKWELI.
Serikali ina namna yake ya kufanya mambo yake. Tuipe muda kwani naamini hakuna kiongozi anafurahia mgao wa umeme na mateso dhidi ya wananchi wake. Juzi tu mh Rais ametoka kuelezea mchakato wa til 4 ambazo ameanza kuzitoa katika wizara ya nishati ili kukabiliana changamoto ya upatikanaji wa umeme
 
Umeelewa lakini nilichokiandika Mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…