Nimemsikiliza Mzee Butiku dakika 45 za ITV na Radio One ameongea mengi, ila haya ndiyo yameonyesha kwanini Yeye ni Hazina ya Fikra Kubwa Tanzania

Ni wapi Afrika ambapo hapakuwa na "Ujamaa" ambako walinemeka sana! Unapokuwa kama santuri mbovu, wakati mwingine mikwaruzo hiyo pia hulainika na mara moja moja kunyoosha wimbo kwa usahihi. Hii ya kwako imegota moja kwa moja, vipi?
Kama unapima kufaulu kwa Tanzania kwa kuilinganisha na nchi nyingine za kiafrika ambazo ni masikini na zilifeli kisiasa basi utakuwa na matatizo makubwa. Hivyo kwasababu nchi nyingine za Afrika hazikufauli basi jaribio la Ujamaa la Mzee Nyerere lisilaumiwe. Kiutaalamu hii tunaiita Tu QuoQue Fallacy....

NB: We start to measure the level of inequality within a state, before measuring level of inequality among states.
 
Hawa ndio chanzo kikubwa cha mkwamo tulio nao leo kama nchi.
Katika watu ambao ni hatari kwa maendeleo, ustawi na mustakabali wa taifa hili ni hawa wazee wa Cold-War.

Jaribio lao la Ujamaa lilifeli vibaya na nchi ikaangukia pua, lakini nashangaa kwanini bado tunawasikiliza tu.
 
Ghana walimtimua Nkurumah mapema na siasa zake za ujamaa uchwara wakayumba kiasi ila wakarudi kwenye mstari kama Taifa linalojielewa.
Ni wapi Afrika ambapo hapakuwa na "Ujamaa" ambako walinemeka sana! Unapokuwa kama santuri mbovu, wakati mwingine mikwaruzo hiyo pia hulainika na mara moja moja kunyoosha wimbo kwa usahihi. Hii ya kwako imegota moja kwa moja, vipi?
 
1. Tanzania bado ina Viongozi Waonevu na bahati mbaya tena wengine bado tu wanarandaranda Mitaani na sijui kwanini hawagusiki na wanaogopwa na wenye Kuwawajibisha.

2. Tunataka Katiba Mpya je, yale yaliyopo Katiba iliyoko tumeyatekeleza hata kwa 75%?

3. Taifa letu sasa lina Watu Wanafiki ambao wakiwa Vichochoroni wananung'unika ila wakiwa mbele ya Viongozi wao wananyamaza.

4. Vijana wa Leo nchini Tanzania ni Waoga watupu.

5. Viongozi wanaotishia Watu wanaowakosoa ni Wasaliti wa Katiba yetu na kamwe hawatufai.

6. Vyombo vya Habari vya Tanzania siku hizi haviibui Mambo ya Kuwaamsha Wananchi kuhusu nchi yao, bali vinaibuliwa Mambo na Watawala kwa yale wayatakayo Wao.

7. Tujitahidi sana Kuwaheshimu Viongozi ( Watawala ) wetu hata kama kuna wanaotukwaza kwani ni Sisi hawa hawa ndiyo tumewaweka Madarakani walipo na kama tukitaka Kuwakosoa basi tuwakosoe kwa Staha na huu ndiyo umekuwa ( uwe ) Ustaarabu wa Watanzania.

Ninakuombea Uhai mrefu Mzee Butiku.
Mzee anayoosha maelezo, safi sana. Hivi ushenzi aliofanya Makonda ni mtu wa kuwa uraiani?

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Katika watu ambao ni hatari kwa maendeleo, ustawi na mustakabali wa taifa hili ni hawa wazee wa Cold-War.

Jaribio lao la Ujamaa lilifeli vibaya na nchi ikaangukia pua, lakini nashangaa kwanini bado tunawasikiliza tu.
Inawezekana ujamaa ulifeli kama unavyodai. Hili ni suala linalohitaji mjadala mpana. Ulifeli kwa vigezo gani. Mfano mmoja idadi ya viwanda vilivyojengwa kipindi hicho huoni ilikuwa hatua nzuri kuelekea katika kujenga msingi wa Tanzania ya viwanda.

Pamoja na upungufu wa sera hiyo suala moja tunakubaliana. Tulifanikiwa kujenga taifa moja ambalo tofauti za kikabila, kijimbo, na kidini zilipungua na kukosa nguvu ya kutawala maisha ya watanzania. Matokeo yake amani na utulivu vimetamalaki kiasi kwamba anayetaka kufanya siasa kwa kutumia vigezo hivyo hatoboi pamoja na changamoto za katiba iliyopo.
 
Butiku,Msuya,Warioba,Msekwa hawa ni miongoni mwa wana CCM wenye uwezo wa kuongea ukweli bila kumuogopa yeyote yule.
Kongole wazee wetu japo umri wenu ushaenda.
Mungu awalinde amin.
 
Zambia hawajawahi kuwa na siasa za ujamaa ila ni taifa moja lisisilo na ukabila na lenye demokrasia imara.
Inawezekana ujamaa ulifeli kama unavyodai. Hili ni suala linalohitaji mjadala mpana. Ulifeli kwa vigezo gani. Mfano mmoja idadi ya viwanda vilivyojengwa kipindi hicho huoni ilikuwa hatua nzuri kuelekea katika kujenga msingi wa Tanzania ya viwanda.

Pamoja na upungufu wa sera hiyo suala moja tunakubaliana. Tulifanikiwa kujenga taifa moja ambalo tofauti za kikabila, kijimbo, na kidini zilipungua na kukosa nguvu ya kutawala maisha ya watanzania. Matokeo yake amani na utulivu vimetamalaki kiasi kwamba anayetaka kufanya siasa kwa kutumia vigezo hivyo hatoboi pamoja na changamoto za katiba iliyopo.
 
Huyo mzee butiku akumbuke enzi zao adhabu ilikuwa viboko tu vya mzee Kambarage😅...

Sahizi ni mambo ya kina anodi shozniga yani ukijifanya nati unachezea mjegejo😅 wa smg! Ukipona ujue kiwete kama bwana yule wa Ubeligiji
 
1. Tanzania bado ina Viongozi Waonevu na bahati mbaya tena wengine bado tu wanarandaranda Mitaani na sijui kwanini hawagusiki na wanaogopwa na wenye Kuwawajibisha.

2. Tunataka Katiba Mpya je, yale yaliyopo Katiba iliyoko tumeyatekeleza hata kwa 75%?

3. Taifa letu sasa lina Watu Wanafiki ambao wakiwa Vichochoroni wananung'unika ila wakiwa mbele ya Viongozi wao wananyamaza.

4. Vijana wa Leo nchini Tanzania ni Waoga watupu.

5. Viongozi wanaotishia Watu wanaowakosoa ni Wasaliti wa Katiba yetu na kamwe hawatufai.

6. Vyombo vya Habari vya Tanzania siku hizi haviibui Mambo ya Kuwaamsha Wananchi kuhusu nchi yao, bali vinaibuliwa Mambo na Watawala kwa yale wayatakayo Wao.

7. Tujitahidi sana Kuwaheshimu Viongozi ( Watawala ) wetu hata kama kuna wanaotukwaza kwani ni Sisi hawa hawa ndiyo tumewaweka Madarakani walipo na kama tukitaka Kuwakosoa basi tuwakosoe kwa Staha na huu ndiyo umekuwa ( uwe ) Ustaarabu wa Watanzania.

Ninakuombea Uhai mrefu Mzee Butiku.
Huyo mzee ni mjinga sana unajua,anavyokuka hela za wakfu wa mwl nyerere?

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Nisikuchoshe anzia dakika ya 40 upande madini ya huyo Mzee Butiku hasa kuhusu Tume ya uchaguzi na uchaguzi wenyewe.

Kama unapima kufaulu kwa Tanzania kwa kuilinganisha na nchi nyingine za kiafrika ambazo ni masikini na zilifeli kisiasa basi utakuwa na matatizo makubwa. Hivyo kwasababu nchi nyingine za Afrika hazikufauli basi jaribio la Ujamaa la Mzee Nyerere lisilaumiwe. Kiutaalamu hii tunaiita Tu QuoQue Fallacy....

NB: We start to measure the level of inequality within a state, before measuring level of inequality among states.
Unaona iulivyo mpuuzi?
Kwa hiyo huwezi kutoa mfano hata mmoja, lakini unataka Tanzania isilinganishwe na nchi yoyote? Hiyo Tanzania ipo sayari ya pekee ambako matatizo yanayowapata wengine yenyewe haiyapati?
Hizo "NB" hazina maana yoyote kama huwezi kujibu swala la msingi.
 
Ghana walimtimua Nkurumah mapema na siasa zake za ujamaa uchwara wakayumba kiasi ila wakarudi kwenye mstari kama Taifa linalojielewa.
Kwani Nyerere na "Ujamaa" wake aliondoka lini kwenye serikali?
Kwani Ghana wamepata ahueni kiuchumi miaka mingapi iliyopita baada ya Nkrumah?

Pamoja na hayo, huwezi kuitolea mfano Ghana kama nchi iliyofanikiwa kiuchumi.
 
Baada ya dikteta mjaama Nkurumah kuondolewa Ghana 1966 kwa mapinduzi nchi iliingia katika kipindi kirefu cha madikteta wa kijeshi kabla ya kurudi kwenye utawala wa demokrasia 1992 na tangu hapo nchi hiyo imepiga hatua kubwa katika demokrasia na uchumi ikituacha mbali sana.

Kama hutaki Ghana chukua Botswana

Mzee Butiku na Mzee Warioba wamebaki kuwa sauti za nyikani tu, hawasikilizwi na hao watawala wala hawawanyimi usingizi. Wamekuwa ni watu wa kupuuzwa tu!

Kuwaweka Warioba na Butiku kundi moja sio sahihi hata mara moja Ingawa wanatoka sehemu moja!! Warioba is principled na sio mnafiki unlike Butiku ambae anaangalia maslahi yake yanapatikana wapi!! Enzi ya Jiwe kwavile taasisi yao ilikuwa inafadhiliwa kwa kiasi na Jiwe hakuwa na ubavu wa kujitokeza na kukosoa na sasa ili ajulikane kuwa yupo ndio anaanza kupiga mayowe.

Jaji Warioba has always been consistent.
 
Baada ya dikteta mjaama Nkurumah kuondolewa Ghana 1966 kwa mapinduzi nchi iliingia katika kipindi kirefu cha madikteta wa kijeshi kabla ya kurudi kwenye utawala wa demokrasia 1992 na tangu hapo nchi hiyo imepiga hatua kubwa katika demokrasia na uchumi ikituacha mbali sana.
"Ikituacha mbali sana"? Kwa sababu ya 'Ujamaa" wa Nyerere?
Ghana nakubaliana na wewe juu ya siasa zao, wamepiga hatua nzuri kabisa, kwa vile hawana CCM huko!

Ghana wana mafuta, na pia ni vinara wa dhahabu. Hivi vimesaidia kuifanya Ghana iwe kama ilivyo sasa. Lakini hawawezi kusema uchumi wao umetengemaa zaidi kuliko wengine. Wanayo madeni ya kutisha!
 
Kama hutaki Ghana chukua Botswana
Nilikuona zamani mkuu Yoda na mfano huo. Sikutaka tu kuujibia.
Botswana walitumia vizuri mali yao ya madini ya Almas, halafu ufugaji wao wa ng'ombe ukawainua.
Wapo wangapi Botswana hadi tulinganishwe na wao, kama chungwa na chungwa na wala siyo chungwa na limao!

Siwaondolei kitu mkuu Yoda, wamejitahidi kulinda utajiri wao uwaletee manufaa wao, kuliko sisi ambao licha ya 'Ujamaa' kukwama miaka mingi nyuma hata kabla ya kuanza kutumia maliasili zetu za madini, hali yetu bado ni duni zaidi, lakini hata hivyo tunaendelea tu kulalamikia 'Ujamaa' kuwa ndio unasababisha tusifanye wanayofanya Botswana.
 
Back
Top Bottom