Nimemsikiliza Padre Kitima, hoja zake zimejikita kwenye hofu zaidi sijaona kipengele kibaya kwenye mkataba

Mwanasheria nguli wa kiwango cha wapi? Cha hapa pasipo na mahakama, na sheria zinazochezewa na watawala, au kiwango cha kimataifa?

Hoja gani ya maana unayosema haikupanguliwa? Kuna hoja ya maana uliyoileta? Kama kuwa mwanasheria kweli ndiyo hayo uliyoandika hapa, basi uanasheria kweli una maana nyingi sana.
Bams vipi kaka?!!!

Kwa hiyo Tanzania hakuna wanasheria nguli kwa sababu tu unaamini "dola" inazichezea mahakama?!!!

Kama ndivyo tunajadili nini sasa nasi hatuko huko mataifa uliyoyasema?!!![emoji1787][emoji1787]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Nimesoma MoU kwa kurudia mara 3.
Nimegundua watanzania wengi ni wavivu wa kusoma kwa umakini.
Wanapenda zaidi kusimuliwa hata kama kuna chumvi.
Huyu msomi hakuna alichoongea cha maana saanaaa zaidi ya kuyarejea mawazo ya jumla kama ilivyo mtandaoni.
Msomi yupi ?!!!

Mwanasheria mweka uzi ?!!!

Kama ndiye ,unatanguliza choyo ,wivu na husuda kwa kushindwa hata kumpa KONGOLE kwa kizuri alichoandika na kukimbilia kujificha kuwa tuwavivu wa kusoma na ameyakusanya mitandaoni ?!!!![emoji15][emoji15][emoji15][emoji1787][emoji1787]

Duuuh hatari sana [emoji1787][emoji1787]

#MamaAnaupigaMwingi[emoji7][emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Uanasheria wako ni mashaka sana. Labda umesomea sheria, lakini siyo mwanasheria. Mwanashetia wa kweli huwa ni makini katika kusikiliza, kuchambua na kufanya hitimisho.

Padre Kitima ameeleza wazi kuwa wao viongozi wa dini siyo jukumu lao kueleza kama mkataba ni mbaya au mzuri bali wao ni sauti ya wananchi. Kwa hiyo wanaeleza yale yanayoelezwa na wananchi. Amesema kuwa wao kama viongozi wa dini wanamsikiliza kila mmoja, na walimwita waziri ili wasikie Serikali inasema nini juu ya hofu na hoja za wananchi.

Kwa hiyo kimsingi wao wametoa tahadhari zaidi kuhusiana na hofu za wananchi. Na kuhusu maoni yao kama viongozi wa dini, wameteua timu yao ya wataalam. Kutokana na hiyo timu ya wataalam, ndiyo kutakuwa na maoni ya viongozi wa dini. Kwa sasa wao kama viongozi wa dini wametoa tu maangalizo.

Kuhusiana na suala la Ngorongoro ameeleza wazi kabisa kuwa wao waliletewa malalamiko, na kuwa wao wanasikiliza malalamiko ya kila mtu, wakatuma na watu wao kuongea na waathirika.

Wewe yaelekea hata huelewi kazi na wajibu wa viongozi wa dini. Unataka waache kazi yao wafanye kazi ya uwanasheria? Mwanasheria unatakiwa kuwa makini katika kusikiliza, kuelewa content ya jambo, mazingira, na lengo la mwongeaji. Hawa ni viongozi wa dini waliomwita waziri kupata ufafanuzi wa malalamiko, mashaka na hofu za wananchi, hasa wananchi ambao hawana access ya kuifikia serikali moja kwa moja.
Huenda unamjibu mpagani sugu🤣
 
Ukuu wa wilaya hupati kabisa kabisa
Ningeweka namba zangu hapa basi ningekuwa nautaka huo ukuu wa wilaya.

Natumia fake Id na hata siku moja sijawahi reveal my true identity humu. Sasa nitaupataje huo ukuu wa wilaya?
 
Kama kweli wewe ni mwanasheria jibu hoja za WanaJF humu ambazo zimejadili IGA kwa Ibara, Vifungu, Vipengere na Randama zake, badala ya kuanzisha uzi mpya.

Kwa mfano, IGA hauna muda wa kikomo hadi DPW, kampuni ya Dubai iliyopewa "exclusive rights" (Ibara ya 5) kwenye maeneo ya ushirikiano - Appendix 1 [Ibara ya 23(1)] itakapokamilisha. Je, unaamini miradi itaisha wakati IGA umetoa fursa Tanzania na Dubai au DPW kubuni fursa zingine za ushirikiano na maendeleo hayana kikomo?

Una maoni gani kuhusu Ibara ya 19 inayohusu Serikali kurithishana makubaliano, ambayo yatakuwa mkataba rasmi, iwapo utatungiwa sheria, baada ya Bunge kuridhia? Je, IGA unastahili kupewa nguvu ya kisheria (Katiba ya JMT, Ibara ya 63(2c)?
Kwanza wewe umekuja hoja mpya.

Mimi thread yangu imejikita kwenye hoja za Padre wangu Kitima. Sio hoja zako

Sasa ngoja nirudi kwenye hoja zako
Kuhusu IGA kutokuwa na muda wa ukomo, unajua maana halisi ya hii IGA? Unajua tofauti baina ya IGA na HGA?
Huu ni mkataba unaofungua nafasi ya kuingia kwa mikataba mingine kwenye maeneo husika ( Specific areas) kwa hiyo unamaanisha IGA ingekuwa na ukomo alafu tena mkataba kuhusu eneo specific pia uwekewe ukomo? Nini logic ya kufanya hivyo?

Alafu kifungu cha 5 kisome vizuri. Exclusive right inayozungumziwa ni kuhusu ku endeleza, kusimamia na kufanya kazi eneo la mradi (project) kama ilivyoanishwa katika apendix 1. Sasa hapo shida ipo wapi? Mwekezaji kuendeleza na kusimamia eneo la mradi kuna shida gani?

Kuhusu Je ni ninaamini kama miradi itaisha wakati IGA imetoa fursa ya kubuni maeneo mengine ya uwekezaji sijaelewa hapa shida iko wapi? Labda ungedadavua vizuri zaidi? Maana kwa mujibu wa mkataba sisi tutawataarifu tu kuhusu fursa , mkataba hausemi lazima tuwape izo fursa sasa sijui shida iko wapi?

Kuhusu Serikali kurithishana mkataba sijaelewa hofu yako iko wapi? Hili ni jambo la kawaida sana kwenye mikataba ya namna hii ya sio mara ya kwanza kufanyika. Huwa linafanyika impliedly na hata likiwekwa kimaandishi sioni shida yeyote.

Nikupe mfano. Serikali yetu iliingia makubaliano na China kujengewa reli ya Tazara na ilikuwa kipindi cha Mwalimu. Makubaliano yale yameendelea kuheshimiwa na kurithiwa na awamu zingine hadi sasa .

Pia kipindi cha Magufuli tulikopa madeni mbalimbali na pamoja na Serikali ya magufuli kuondoka Serikali ya Samia imerithi hayo madeni na inaendelea kuyalipa. Sasa nieleweshe wewe hapo shida iko wapi?
 
Uanasheria wako ni mashaka sana. Labda umesomea sheria, lakini siyo mwanasheria. Mwanashetia wa kweli huwa ni makini katika kusikiliza, kuchambua na kufanya hitimisho.

Padre Kitima ameeleza wazi kuwa wao viongozi wa dini siyo jukumu lao kueleza kama mkataba ni mbaya au mzuri bali wao ni sauti ya wananchi. Kwa hiyo wanaeleza yale yanayoelezwa na wananchi. Amesema kuwa wao kama viongozi wa dini wanamsikiliza kila mmoja, na walimwita waziri ili wasikie Serikali inasema nini juu ya hofu na hoja za wananchi.

Kwa hiyo kimsingi wao wametoa tahadhari zaidi kuhusiana na hofu za wananchi. Na kuhusu maoni yao kama viongozi wa dini, wameteua timu yao ya wataalam. Kutokana na hiyo timu ya wataalam, ndiyo kutakuwa na maoni ya viongozi wa dini. Kwa sasa wao kama viongozi wa dini wametoa tu maangalizo.

Kuhusiana na suala la Ngorongoro ameeleza wazi kabisa kuwa wao waliletewa malalamiko, na kuwa wao wanasikiliza malalamiko ya kila mtu, wakatuma na watu wao kuongea na waathirika.

Wewe yaelekea hata huelewi kazi na wajibu wa viongozi wa dini. Unataka waache kazi yao wafanye kazi ya uwanasheria? Mwanasheria unatakiwa kuwa makini katika kusikiliza, kuelewa content ya jambo, mazingira, na lengo la mwongeaji. Hawa ni viongozi wa dini waliomwita waziri kupata ufafanuzi wa malalamiko, mashaka na hofu za wananchi, hasa wananchi ambao hawana access ya kuifikia serikali moja kwa moja.

Safi sana
 
Nakusikitikia sana. Mimi sio mwanasheria uchwara, ni mwanasheria kweli ndo mana nimejibu kwa hoja. Umeongea maneno mengi ila umeshindwa hata kupangua majibu ya hoja yangu yaliyotokana na uchambuzi wa mkataba wenyewe hasa kwenye mambo aliyoyaongelea Padre Kitima mwenyewe

Mwanasheria Huyu hapa, wewe ni mtu wa hovyo :

Ningeweka namba zangu hapa basi ningekuwa nautaka huo ukuu wa wilaya.

Natumia fake Id na hata siku moja sijawahi reveal my true identity humu. Sasa nitaupataje huo ukuu wa wilaya?
Uchawa acha we bado kijana mambo ya unafiki noo
 
Nakusikitikia sana. Mimi sio mwanasheria uchwara, ni mwanasheria kweli ndo mana nimejibu kwa hoja. Umeongea maneno mengi ila umeshindwa hata kupangua majibu ya hoja yangu yaliyotokana na uchambuzi wa mkataba wenyewe hasa kwenye mambo aliyoyaongelea Padre Kitima mwenyewe
Wewe huwezi kukubali kama amepangua hoja zako au la, wengine tunaona amepangua!
 
Waarabu ni washenzi hawa majangili

Wamehonga wabunge ili wauze nchi

Never let's say they won for while
 
Waarabu ni washenzi hawa majangili

Wamehonga wabunge ili wauze nchi

Never let's say they won for while
Kumbe shida ni wawekezaji kuwa waarabu?

Sijaona sehemu wabunge wameuza nchi labda utusaidiaje na kwa ushahidi? Wameuzaje?
 
Tangu mjadala wa makubaliano ya Tanzania na Dubai kuhusu masuala ya uwekezaji ikiwemo bandari uanze, hadi sasa sijaona mtu aliyesema kuhusu ubaya wowote wa kipengele cha mkataba na akakidadavua vizuri kisheria nikamuelewa.

Mimi ni mwanasheria, nimesoma mkataba, nimesoma maelezo ya Serikali kuhusu mkataba na nimesikiliza hoja wapingaji na kusema kweli sijaona hoja za wanaopinga zaidi ya kuelezea hofu zao na tahadhari zao.

Leo nimemsikiliza Padre Kitima ambaye nae pia ameelezea hofu yake kuhusu mkataba ikiwemo vifungu kadhaa. Kusema kweli hakuna alipoweza kusema kuhusu mapungufu ya kipengele chochote zaidi ya kuelezea hofu yake na kuweka tahadhari

Padre Kitima ameelezea kuhusu suala la Ardhi na kusema kweli hakuna sehemu katika mkataba paliposema mwekezaji atamilikishwa ardhi. Nilitegemea atakisema hicho kifungu na kukisoma ila nimemsikiliza zaidi nimeona nae kapiga siasa tu. Kwa nilivyokisoma kifungu cha 8 (3)(b) cha mkataba kimesema wazi haki za kutumia ardhi zitatolewa kwa mujibu wa Sheria na taratibu zetu na inajulikana kwenye sheria zetu mwekezaji hapewi haki ya kumiliki ardhi ila haki ya matumizi tu ya ardhi kwa ajili ya uwekezaji( derivative right)

kuhusu ulinzi na usalama wa bandari. hakuna kipengele chochote kwenye mkataba kilichosema mwekezaji atasimamia masuala ya ulinzi na usalama katika bandari. hata mwekezaji aliyepita tics aliyekuwa anaendesha sehemu ya bandari yetu hakuwahi kusimamia masuala ya ulinzi na usalama. Hapa pia Padre wangu Kitima ameelezea hofu tu na wala sio ubaya wa mkataba kwa kudadavua vizuri

Kuhusu Serikali kuwataarifu Dubai kuhusu fursa zingine za uwekezaji (Ibara ya 4) kusema kweli sijaona tatizo lolote kuhusu kifungu hiki. Ningeelewa kuwa kuna tatizo juu ya hichi kifungu endapo kingesema Serikali italazimika kuwapa maeneo hayo baada ya kuwataarifu. Sioni tatizo lolote kuhusu mtu kutaarifiwa tu kuhusu fursa zilizopo. Kwenye hili naona tafsiri isiyo sahihi na hofu isiyokuwepo inayolazimishwa kuwepo.

Mwisho ameelezea sehemu wawekezaji hawa walipofanikiwa na kuna sehemu amesema hawajafanikiwa. Hili sioni kama ni hoja maana mifano mizuri inaweza kuwa kwetu

Mwisho Padre Kitima amesema kuhusu Loliondo. Kusema kweli hapa naona amekuwa mwanasiasa maana sioni hoja yake kuhusu watu waliopelekwa msomera kulalamika kwa sababu hata kwa watumishi wa Umma waliopelekwa Dodoma wapo waliolalamika na kusema wanapata changamoto Dodoma! Sasa ninachojiuliza ni Je kwa wale waliolalamika inamaanisha zoezi la kuwahamishia watumishi wa serikali Dodoma halikuwa zoezi zuri lenye maslahi mazuri kwa nchi?

Mnaopinga mkataba au kuelezea mapungufu yake. Tusaidieni kuja na hoja zenye mashiko na maelezo ya uhakika. Mnapokuja na maneno ya juu juu tu bila kudadavua tunawaona na nyie ni walewale tu.
utajaribu kutetea sana hata kama ni mwanasheri kwanza tanzania hatuna wanasheria tuna wababaishaji wa sheria tu.ukweli utakuja fahamika na mtaumbuka kweupe na mtashindwa kuzificha nyuso zenu.time will tell.
 
Kumbe shida ni wawekezaji kuwa waarabu?

Sijaona sehemu wabunge wameuza nchi labda utusaidiaje na kwa ushahidi? Wameuzaje?
hakuna mtu aliyesema shida ni waarabu na kama wewe umeona hivyo basi na wewe unaenda kwa hisia tu.
 
Tangu mjadala wa makubaliano ya Tanzania na Dubai kuhusu masuala ya uwekezaji ikiwemo bandari uanze, hadi sasa sijaona mtu aliyesema kuhusu ubaya wowote wa kipengele cha mkataba na akakidadavua vizuri kisheria nikamuelewa.

Mimi ni mwanasheria, nimesoma mkataba, nimesoma maelezo ya Serikali kuhusu mkataba na nimesikiliza hoja wapingaji na kusema kweli sijaona hoja za wanaopinga zaidi ya kuelezea hofu zao na tahadhari zao.

Leo nimemsikiliza Padre Kitima ambaye nae pia ameelezea hofu yake kuhusu mkataba ikiwemo vifungu kadhaa. Kusema kweli hakuna alipoweza kusema kuhusu mapungufu ya kipengele chochote zaidi ya kuelezea hofu yake na kuweka tahadhari

Padre Kitima ameelezea kuhusu suala la Ardhi na kusema kweli hakuna sehemu katika mkataba paliposema mwekezaji atamilikishwa ardhi. Nilitegemea atakisema hicho kifungu na kukisoma ila nimemsikiliza zaidi nimeona nae kapiga siasa tu. Kwa nilivyokisoma kifungu cha 8 (3)(b) cha mkataba kimesema wazi haki za kutumia ardhi zitatolewa kwa mujibu wa Sheria na taratibu zetu na inajulikana kwenye sheria zetu mwekezaji hapewi haki ya kumiliki ardhi ila haki ya matumizi tu ya ardhi kwa ajili ya uwekezaji( derivative right)

kuhusu ulinzi na usalama wa bandari. hakuna kipengele chochote kwenye mkataba kilichosema mwekezaji atasimamia masuala ya ulinzi na usalama katika bandari. hata mwekezaji aliyepita tics aliyekuwa anaendesha sehemu ya bandari yetu hakuwahi kusimamia masuala ya ulinzi na usalama. Hapa pia Padre wangu Kitima ameelezea hofu tu na wala sio ubaya wa mkataba kwa kudadavua vizuri

Kuhusu Serikali kuwataarifu Dubai kuhusu fursa zingine za uwekezaji (Ibara ya 4) kusema kweli sijaona tatizo lolote kuhusu kifungu hiki. Ningeelewa kuwa kuna tatizo juu ya hichi kifungu endapo kingesema Serikali italazimika kuwapa maeneo hayo baada ya kuwataarifu. Sioni tatizo lolote kuhusu mtu kutaarifiwa tu kuhusu fursa zilizopo. Kwenye hili naona tafsiri isiyo sahihi na hofu isiyokuwepo inayolazimishwa kuwepo.

Mwisho ameelezea sehemu wawekezaji hawa walipofanikiwa na kuna sehemu amesema hawajafanikiwa. Hili sioni kama ni hoja maana mifano mizuri inaweza kuwa kwetu

Mwisho Padre Kitima amesema kuhusu Loliondo. Kusema kweli hapa naona amekuwa mwanasiasa maana sioni hoja yake kuhusu watu waliopelekwa msomera kulalamika kwa sababu hata kwa watumishi wa Umma waliopelekwa Dodoma wapo waliolalamika na kusema wanapata changamoto Dodoma! Sasa ninachojiuliza ni Je kwa wale waliolalamika inamaanisha zoezi la kuwahamishia watumishi wa serikali Dodoma halikuwa zoezi zuri lenye maslahi mazuri kwa nchi?

Mnaopinga mkataba au kuelezea mapungufu yake. Tusaidieni kuja na hoja zenye mashiko na maelezo ya uhakika. Mnapokuja na maneno ya juu juu tu bila kudadavua tunawaona na nyie ni walewale tu.
Uelewa wako ni mdogo sana. Kama umeshindwa kumuelewa Kitima unatia mashaka sana. Kitima ametoa facts dhidi ya propaganda na uongo wa CCM kuhusu maktaba. Mkataba huu unamadhara makubwa sana kwa taifa but huenda ukawa na faida mwa CCM ya wachache.
 
Isitoshe Dubai siyo nchi (state) hivyo haiwezi kuingia mkataba wa kimaifa (IGA - kati ya nchi na nchi). Mkataba unapaswa kuwa baina yake au DPW ns TPA.

Bunge lisiridhie kutunga sheria ya kuupa nguvu ya utekelezaji
 
Back
Top Bottom