Uanasheria wako ni mashaka sana. Labda umesomea sheria, lakini siyo mwanasheria. Mwanashetia wa kweli huwa ni makini katika kusikiliza, kuchambua na kufanya hitimisho.
Padre Kitima ameeleza wazi kuwa wao viongozi wa dini siyo jukumu lao kueleza kama mkataba ni mbaya au mzuri bali wao ni sauti ya wananchi. Kwa hiyo wanaeleza yale yanayoelezwa na wananchi. Amesema kuwa wao kama viongozi wa dini wanamsikiliza kila mmoja, na walimwita waziri ili wasikie Serikali inasema nini juu ya hofu na hoja za wananchi.
Kwa hiyo kimsingi wao wametoa tahadhari zaidi kuhusiana na hofu za wananchi. Na kuhusu maoni yao kama viongozi wa dini, wameteua timu yao ya wataalam. Kutokana na hiyo timu ya wataalam, ndiyo kutakuwa na maoni ya viongozi wa dini. Kwa sasa wao kama viongozi wa dini wametoa tu maangalizo.
Kuhusiana na suala la Ngorongoro ameeleza wazi kabisa kuwa wao waliletewa malalamiko, na kuwa wao wanasikiliza malalamiko ya kila mtu, wakatuma na watu wao kuongea na waathirika.
Wewe yaelekea hata huelewi kazi na wajibu wa viongozi wa dini. Unataka waache kazi yao wafanye kazi ya uwanasheria? Mwanasheria unatakiwa kuwa makini katika kusikiliza, kuelewa content ya jambo, mazingira, na lengo la mwongeaji. Hawa ni viongozi wa dini waliomwita waziri kupata ufafanuzi wa malalamiko, mashaka na hofu za wananchi, hasa wananchi ambao hawana access ya kuifikia serikali moja kwa moja.