Nimemsikiliza Padre Kitima. Hoja zake zimejikita kwenye hofu zaidi. Sijaoona kipengele kibaya kwenye mkataba

Yeye alikuwa rais na ndio mwenye access na hiyo mikataba, na alitamka hilo hadharani. Kwanini hukujitokeza umuombe mkataba?
Kwani Rais sio binadamu kama wewe? Hawezi kuongopa? hawezi kuwa na hisia? Umeshawai kunisikia nikisema kweli gesi ya mtwara imeuzwa?
Bila uthibitisho hayo ni maneno tu ambayo mtu yeyote anaweza kuyaongea.
 
Tangu mjadala wa makubaliano ya Tanzania na Dubai kuhusu masuala ya uwekezaji ikiwemo bandari uanze, hadi sasa sijaona mtu aliyesema kuhusu ubaya wowote wa kipengele cha mkataba na akakidadavua vizuri kisheria nikamuelewa.

Mimi ni mwanasheria, nimesoma mkataba, nimesoma maelezo ya Serikali kuhusu mkataba kusema kweli sijaona hoja za wanaopinga zaidi ya kuelezea hofu zao na tahadhari zao.

Leo nimemsikiliza Padre Kitima ambaye nae pia ameelezea hofu yake kuhusu mkataba ikiwemo vifungu kadhaa. Kusema kweli hakuna alipoweza kusema kuhusu mapungufu ya kipengele chochote zaidi ya kuelezea hofu yake na kuweka tahadhari

Padre Kitima ameelezea kuhusu suala la Ardhi na kusema kweli hakuna sehemu katika mkataba paliposema mwekezaji atamilikishwa ardhi. Nilitegemea atakisema hicho kifungu na kukisoma ila nimemsikiliza zaidi nimeona nae kapiga siasa tu. Kwa nilivyokisoma kifungu cha 8 (3)(b) cha mkataba kimesema wazi haki za kutumia ardhi zitatolewa kwa mujibu wa Sheria na taratibu zetu na inajulikana kwenye sheria zetu mwekezaji hapewi haki ya kumiliki ardhi ila haki ya matumizi tu ya ardhi kwa ajili ya uwekezaji( derivative right)

kuhusu ulinzi na usalama wa bandari. hakuna kipengele chochote kwenye mkataba kilichosema mwekezaji atasimamia masuala ya ulinzi na usalama katika bandari. hata mwekezaji aliyepita tics aliyekuwa anaendesha sehemu ya bandari yetu hakuwahi kusimamia masuala ya ulinzi na usalama. Hapa pia Padre wangu Kitima ameelezea hofu tu na wala sio ubaya wa mkataba kwa kudadavua vizuri

Kuhusu Serikali kuwataarifu Dubai kuhusu fursa zingine za uwekezaji (Ibara ya 4) kusema kweli sijaona tatizo lolote kuhusu kifungu hiki. Ningeelewa kuwa kuna tatizo juu ya hichi kifungu endapo kingesema Serikali italazimika kuwapa maeneo hayo baada ya kuwataarifu. Sioni tatizo lolote kuhusu mtu kutaarifiwa tu kuhusu fursa zilizopo. Kwenye hili naona tafsiri isiyo sahihi na hofu isiyokuwepo inayolazimishwa kuwepo.

Mwisho ameelezea sehemu wawekezaji hawa walipofanikiwa na kuna sehemu amesema hawajafanikiwa. Hili sioni kama ni hoja maana mifano mizuri inaweza kuwa kwetu

Mwisho Padre Kitima amesema kuhusu Loliondo. Kusema kweli hapa naona amekuwa mwanasiasa maana sioni hoja yake kuhusu watu waliopelekwa msomera kulalamika kwa sababu hata kwa watumishi wa Umma waliopelekwa Dodoma wapo waliolalamika na kusema wanapata changamoto Dodoma! Sasa ninachojiuliza ni Je kwa wale waliolalamika inamaanisha zoezi la kuwahamishia watumishi wa serikali Dodoma halikuwa zoezi zuri lenye maslahi mazuri kwa nchi?
Hata kwenye gesi mlisema hivyo hivyo, Leo mmebakia kukopa madeni. Wadanganyeni wengine.
 
Afaddhalli viongozi wa dini wameketi chini na angalau kuthubutu kudadavua na kuishauri serikali kwa uchache kuhusu Bandari, better wameungana na miongoni mwa waTz kuonyesha hofu. Vyama vya Siasa na taasisisi za kiraia vipo kimya haijulikani wanaunga mkono ama wanapinga. Sijui, labda wanajipanga. Kwa style hii 2025 njia ni nyeupe na nyepesi mno kwa Mama kurejea Mamlakani. Na 2030, vilevile yeyote atakae simamishwa na ruling party atashinda kwa kishindo kwasabb atakua mpya while opposition still watakua ni walewale wagombea Urais wa miaka yote.
Wewe unawaza uchaguzi tu. Siasa haziendi hivyo. Unawaza 2030 wakati hata hujui mwezi ujao utakuwaje?.
 
Kila siku Huwa nawaambia Wajamaa ni watu wajinga sana na msingi wa mambo Yao Huwa ni hisia hasi na kujihami mda wote,wanachoogopa Wala hakieleweki
Wanaogopa tangu historia mbaya ya serikali. Mkataba wa NBC, Mkataba wa Netsolutions na Tanesco, Mkataba wa TRL na Serikali, mkataba wa bomba la gesi, IPTL etc yote hayo yalishindikana. Lazima wanachi wawe na hofu. Wewe Kama huna hofu utakuwa mnafiki au chawa.
 
Hizi taharuki kuhusu mkataba zimezagaa Nchi nzima,naona Wananchi wengi sasa wanapata habari zao twitter.

Alamsiki
 
Hata watetezi wa uuzwaji wa gas yetu huko Mtwara walikuwa wanakuja na utetezi na mbwembwe kama hizi zako. Leo hii imefahamika gas sio yetu, umemuona yoyote katika waliouza gas ile wakijitokeza kutetea uhuni ule?
Nikikumbuka stori za gesi ya mtwara nachoka kabisa. Watu wasio na hatia walipoteza maisha wilayani Masasi wakati wa maandamano ya kupinga gesi kusafirishwa kwenda Dar.Siasa hizi
 
Unaandika vijimaneno viwili vitatu unaita uchambuzi

Halafu unasema hujaona chochote.

Hapo kwa njaa zako unapigia mahesabu mahela ya waarabu watakayo kuita wakupe.
 
Mwisho ameelezea sehemu wawekezaji hawa walipofanikiwa na kuna sehemu amesema hawajafanikiwa. Hili sioni kama ni hoja maana mifano mizuri inaweza kuwa kwetu

Mwisho Padre Kitima amesema kuhusu Loliondo. Kusema kweli hapa naona amekuwa mwanasiasa maana sioni hoja yake kuhusu watu waliopelekwa msomera kulalamika kwa sababu hata kwa watumishi wa Umma waliopelekwa Dodoma wapo waliolalamika na kusema wanapata changamoto Dodoma! Sasa ninachojiuliza ni Je kwa wale waliolalamika inamaanisha zoezi la kuwahamishia watumishi wa serikali Dodoma halikuwa zoezi zuri lenye maslahi mazuri kwa nchi?
Wewe unadai ni mwanasheria na unakuwa na fikra za aina hii kama ulivyoeleza hapa?

God have mercy upon us!

Hayo mengine uliyoandika huko juu, kama unadhani ni "hofu" tu ya Padre; sasa wewe tusemeje kwa unavyojiaminisha kutokuwa na hafu juu ya mkataba huo? Wewe ndiye utakuwa unasimamia utekelezaji wake?

Hakuna lolote la maana katika andiko zima uliloweka hapa, ila ni mwendelezo tu wa fikra potofu ambazoimekuwa kama ni jadi yako.
 
Tangu mjadala wa makubaliano ya Tanzania na Dubai kuhusu masuala ya uwekezaji ikiwemo bandari uanze, hadi sasa sijaona mtu aliyesema kuhusu ubaya wowote wa kipengele cha mkataba na akakidadavua vizuri kisheria nikamuelewa.

Mimi ni mwanasheria, nimesoma mkataba, nimesoma maelezo ya Serikali kuhusu mkataba kusema kweli sijaona hoja za wanaopinga zaidi ya kuelezea hofu zao na tahadhari zao.

Leo nimemsikiliza Padre Kitima ambaye nae pia ameelezea hofu yake kuhusu mkataba ikiwemo vifungu kadhaa. Kusema kweli hakuna alipoweza kusema kuhusu mapungufu ya kipengele chochote zaidi ya kuelezea hofu yake na kuweka tahadhari

Padre Kitima ameelezea kuhusu suala la Ardhi na kusema kweli hakuna sehemu katika mkataba paliposema mwekezaji atamilikishwa ardhi. Nilitegemea atakisema hicho kifungu na kukisoma ila nimemsikiliza zaidi nimeona nae kapiga siasa tu. Kwa nilivyokisoma kifungu cha 8 (3)(b) cha mkataba kimesema wazi haki za kutumia ardhi zitatolewa kwa mujibu wa Sheria na taratibu zetu na inajulikana kwenye sheria zetu mwekezaji hapewi haki ya kumiliki ardhi ila haki ya matumizi tu ya ardhi kwa ajili ya uwekezaji( derivative right)

kuhusu ulinzi na usalama wa bandari. hakuna kipengele chochote kwenye mkataba kilichosema mwekezaji atasimamia masuala ya ulinzi na usalama katika bandari. hata mwekezaji aliyepita tics aliyekuwa anaendesha sehemu ya bandari yetu hakuwahi kusimamia masuala ya ulinzi na usalama. Hapa pia Padre wangu Kitima ameelezea hofu tu na wala sio ubaya wa mkataba kwa kudadavua vizuri

Kuhusu Serikali kuwataarifu Dubai kuhusu fursa zingine za uwekezaji (Ibara ya 4) kusema kweli sijaona tatizo lolote kuhusu kifungu hiki. Ningeelewa kuwa kuna tatizo juu ya hichi kifungu endapo kingesema Serikali italazimika kuwapa maeneo hayo baada ya kuwataarifu. Sioni tatizo lolote kuhusu mtu kutaarifiwa tu kuhusu fursa zilizopo. Kwenye hili naona tafsiri isiyo sahihi na hofu isiyokuwepo inayolazimishwa kuwepo.

Mwisho ameelezea sehemu wawekezaji hawa walipofanikiwa na kuna sehemu amesema hawajafanikiwa. Hili sioni kama ni hoja maana mifano mizuri inaweza kuwa kwetu

Mwisho Padre Kitima amesema kuhusu Loliondo. Kusema kweli hapa naona amekuwa mwanasiasa maana sioni hoja yake kuhusu watu waliopelekwa msomera kulalamika kwa sababu hata kwa watumishi wa Umma waliopelekwa Dodoma wapo waliolalamika na kusema wanapata changamoto Dodoma! Sasa ninachojiuliza ni Je kwa wale waliolalamika inamaanisha zoezi la kuwahamishia watumishi wa serikali Dodoma halikuwa zoezi zuri lenye maslahi mazuri kwa nchi?
Ni namna ya kuwasilisha hasa kwa watumishi wa kanisa. Anajaribu kumantain neutrality.
 
Back
Top Bottom