Nimemsikiliza Padre Kitima. Hoja zake zimejikita kwenye hofu zaidi. Sijaoona kipengele kibaya kwenye mkataba

Kila jambo tunalifanya kwa sababu ya HOFU.

1. Tunalima kwa sababu ya HOFU ya kukosa chakula
2. Tunavaa Condom kwa HOFU ya kupata maambukizi
3. tunafanya DNA test kwa HOFU ya kubambikiwa watoto
4. Tuna majeshi kwa HOFU ya Usalama wetu
5. Tunasali/tunaswali kwa HOFU ya adhabu huko Ahela.
6. Tunajenga madaraja kwa HOFU ya kusombwa na Maji.
7. Tunajenga Msingi Imara wa nyumba kwa HOFU ya nyumba kuanguka
8. Tumezuia Watoto wadogo kwenda Bweni kwa HOFU ya Kulawitiwa
9. Tunavuna Maji kwa HOFU ya kukosa maji
10. Tunalinda Rasilimali zetu kwa HOFU ya kunyang'anywa na Wakoloni Mamboleo
11. HOFU NDO MSINGI WA KILA KITU. Waarabu wana kwao
 
Nimefanya uchambuzi wangu kuthibitisha kuwa ni hofu tu na kwenye mkataba hakuna shida. Weka uchambuzi wako kuonesha mkataba una shida. Hili ni jukwaa huru
 
Wewe huna akili au unatokea zanzibar
 
Mimi sifanyi mambo yangu kwa sababu ya hofu.
 
Ni namna ya kuwasilisha hasa kwa watumishi wa kanisa. Anajaribu kumantain neutrality.
Angefanya ufafanuzi kuonesha makosa at least tungeona hoja yake iko wapi? Kwa watanzania wengi wasiopenda kusoma wanaweza muona ana hoja kweli ila kumbe kuihalisia hakuna hoja ya msingi
 
Asitwambie kitu huyu mwanasheria!
Wasiwasi ndiyo akili shehe.
Na akili za kuambiwa changanya na zako
 
This time Serikali imeweka wazi,hapo awali hiyo unayosema ilikuwa wazi?
Serikali imeweka wazi na imeelezea faida zake,kinachoinekana ni hasara ziko kwenye hisia kuliko uhalisia..

Hoja ya sijui ukijifunga hakuna kuvunja mkataba imejibiwa
Bandari kuuzwa imejibiwa
Usalama wamejibu
N.k.nk Sasa shida Iko wapi?

My Take
Kila siku nawaambia ogopa sana Wajamaa Huwa ni watu wa hovyo sana,wanaongozwa Kwa vitu vya hiasia,Imani na hofu za kipuuzi bila hoja..
 
Uko sahihi kabisa. Ninachokiona ni hisia hasi na kujihami zaidi kuliko uhalisia
Serikali imejibu hoja zote Sasa shida Iko wapi? Na uzuri Kila kitu kumewekwa Bungeni..

Mengine yamesalia ni hisia za kipuuzi na wapuuzi wanatumia kujitafutia umaarufu wa Kisiasa.
 
Naona umejijengea hofu.

Huu mkataba ni wa Watanzania. Unajadili hoja ya mtu anayehoji contents za mkataba.

Ulipaswa kuja na hoja zenye mashiko kuliko hadithi za abunuwasi hapa kumjibu mtoa hoja.

Hebu tupe mfano mzuri mmoja wa mkataba wa ubinafsishaji yaani ukodishaji au upangishaji baina ya serikali na wageni uliowahi kufanikiwa.

Pia kumbuka hoja kuwa serikali imeshindwa kusimamia na hao wageni watapandisha tija ili kuchangia bajeti ya nchi kwa 67%, leta elimu hapa kwa nini na hasa maeneo gani tumeshindwa kusimamia.

Serikali inapofika mahala inasema jambo hili au lile wameshindwa maana yake ni kwamba CCM imeshindwa hivyo badala ya kung'ang'ania kwa mitutu madarakani wawapishe wengine waendelee pale walipoishia.

Naomba kufahamu, hivi Kibajaji au Msukuma wana utaalam gani wa kudeal na mikataba?

Kwa mtazamo wangu ni kwamba, kama serikali iliupeleka Bungeni Mkataba huo kwahoja za jumla na hakuna kifungu kwa kifungu kilichojadiliwa na kupitishwa, maana yake ni kwamba wewe na wenzako mnaoupigia chapuo mkataba hamjui hata nini mnasimamia zaidi ya kutetea chama
 
Wewe umemsiliza wap mbona tofauti na maelezo yako, Father Kitima yupo smart sana na kuelezea kwa ufasaha
 
Sheria ipi imerumika kuuweka wazi?
Au ni utashi wa Hangaya?

Ndugu sikiliza.
Shida siyo kukodisha, kupangisha wala kushirikiana. Tatizo ni contents za mkataba. Tatizo ni proccess za kufikia utekelezaji wake.

Kila mwenye akili timamu anahitaji kuona mabadiliko ya kiutendaji yenye tija. Unazinanga serikali zilizopita kuwa hazikuwa na uwazi lakini hizo serikali zilikuwa za chama gani? Huu uwazi unaoongelewa leo umeletwa kwa sheria gani?

Wapuuzi na wapumbavu ndiyo huamini kuwa akishakuwa kiongozi basi anakuwa mwenye akili kuliko anaowaongoza.
 
Hivi we hujaona vyama vya siasa vinavyoupinga mkataba huo? Au huna macho. Hujaona bunge linavyomshambulia mbowe karibu nusu ya mijadala ya nibowe. Hujaona lisu anavyosema mkataba wa hovyo kiwahi kutokea. Hujasikia mange kimambi anavyotusemea na kusema wewe. Au hujua mana ya vyama vya siasa na makundo ya kiraia. Au makundi ya kiraia kwako ni mapadre tu
 
Tatizo lako kwa kitima ni kwa sababu yeye ni father Kitima.Lakini ukweli hata sisi wanataaluma wenzako tunaona tatizo kwenye mkataba sio tu kwenye vipengele bali kuanzia kwenye recitals,parties,terms na conclusion.Nilisikitika sana kuona wataalamu hawakufanya homework Yao vizuri kabla ya kukimbia nao bungeni.
 
Hamjui mnachotaka,isipowekwa wazi mnauliza ,iliwekwa wazi mnauliza , upuuzi mtupu..

Pili Contents zimefanya nini? Kwa mfano content ipi kwako ni shida?
 


Hivi unaweza kuzipangua hizi facts? Huyu mtu anaongea kwa uwazi kabisa ameshikilia huo Mkataba? Na kama anapotosha wamchukulie hatua :

 
upuuzi mtupu..

Pili Contents zimefanya nini? Kwa mfano content ipi kwako ni shida?
Kwanza elewa kuwa am not questioning kwa faida yangu. Nina wanangu pia watakuwepo wajukuu mbeleni.

Najua wewe tayari umeshajiwekea mazingira ya wanao na vitukuu.


Umeuliza content. Be smart utueleze kuwa mkataba uliovujishwa ndo huo au huko ndani mna mkataba wenu?


Weka mkataba hapa ulio sahihi nikuoneshe contents ambazo zinaenda kuigharimu nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…