Nimemsikiliza vizuri Askofu Gwajima, nina maswali machache juu ya nadharia yake

Nimemsikiliza vizuri Askofu Gwajima, nina maswali machache juu ya nadharia yake

meliyasumu

Member
Joined
Jul 20, 2021
Posts
16
Reaction score
9
Nimesikiliza kwa umakini sana juu ya mambo aliyoyasema mchungaji Gwajima. Nina maswali machache sana juu ya nadharia yake juu ya korona na namna alivyosema na kuaminisha watu:

1. Yeye ni mtumishi wa Mungu na anaamini Mungu ni alfa na omega na hashindwi na chochote, sasa kama ni hivyo kwanini anasema tu wasichanje wakati angeweza kuwaambia hata ukichanja hutakufa maana Mungu hashindwi na chochote na mimi kama mtumishi nawaaminisha kwa kuwa nimetumwa ma Mungu.

2. Mungu anasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa kwanini yeye anatoa maneno tu haji na ushahidi wa kimaabara juu ya ukweli wa anayoyaamini?

3. Anasema ana taasisi marekani je yeye anawezaje kwenda kwenye hiyo taasisi yake iliyo marekani kama hana chanjo? Maana baada ya kuibuka kwa korona hauwezi kwenda marekani bila chanjo sasa kwanini yeye anashawishi waamini wake wasichanjwe?

4.Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi ni chache nazo nimejaa taabu anataka kutuaminisha kuwa tusipochajwa tutaishi zaidi?

5. Kuwa na msimamo wa unaloliamini ni jambo jema sana lakini kwanini msimamo wako ndio uwe muongozo kwa waumini wako wote?

6.Unasema unajua madhara negative yatakayotokea baada ya kuchanja je alijiuliza yeye ndio mtu pekee anayepredict the future?
Nashauri.

Tuwe na imani hata kufa, nami nitakupa taji la uzima, nafikiri tuendelee kuomba huku tukisikiliza mioyoni mwetu sauti za ndani nini Mungu anasema na sisi wenyewe Gwajima siyo atakayetupeleka mbinguni wala hawezi kuzuia mipango ya Mungu kwa wanadamu
Tusimtumie Gwajima kama reference na yeye siyo alfa na omega.
 
Back
Top Bottom