Nimemsomesha, nimegharamika, leo kaniacha anaolewa na mtu mwingine

Kuwa single nako vizuri. Lakini sasa wewe nako utanunuaje kuku umuache kwa aliyekuuzia on a sasa umeambulia manyoya. Pole sana. Uwe unanunua jumla jumla siyo nusunusu. Ndo maaana ngabu alirudi bariadi kwenda kutafuta mke. Nami naelekea itilima it klima nikatufute.
 
si alikuwa anamkamua tangu A level, mpaka chuo alishakuwa mke wake mkataba umeisha.
labda kama talaka hairuhusiwi kwenye mkataba wao.
Alichonishangaza kaenda kujishitaki kwamba alikuwa anatembea na mtoto wa Ndalichako!!!Mwanaume wa kweli hajuti, anaosonga mbele, nini vihela hivyo watu wanahonga magari kwa kupata papuchi ya siku moja!Ningekuwa mimi hta nisingepoteza muda wangu mbona wanawake wazuri wengi sana na wanatabia za kuwa wake
 
Pole sana kwa hilo ndugu.

Duniani kitu ambacho kimekuwa janga kubwa ni MAPENZI. Ulifanya kwa lengo na nia njema ila hayo ndo malipo ya malimwengu. Na Zaidi unasema mliandikishana mkataba, mmmh hapo ni ukakasi, haikutakiwa MKATABA bali NDOA. Hata sasa unasema umefungua kesi mahakamani sijui ya madai au ya mapenzi, Kitu ambacho naona unakosa haki nacho. Mkataba unaokubalika wa kuunganisha watu ni NDOA na wenye dhamana hiyo ni SERIKALI(MKUU WA WILAYA), MAPADRI, MAKASISI na MASHEKHE na wote hao hupewa kibali toka serikalini cha kufungisha ndoa na kwenye kufungisha kila mmoja wenu anaulizwa mara tatu kama karidhia hiyo ndoa mbele ya kadamnasi iliyopo pale (mashahidi), asiye na kibali hicho ndoa atakazofungisha ni batili whether SHEKHE, PADRI AU KASISI. Sasa ninyi mlichofanya kwa mkataba huo haikupi nguvu kisheria kummiliki yule, ila ingekuwa unamsomesha na rehani wameweka nyumba, kiwanja au gari mkataba utakapokengekwa ingekuwa rahisi kisheria kuzuia zile mali zilizo rehani, ila kwa mtu hapo ngumu, labda wanasheria watusaidie hapo.

Nini cha kukushauri baada ya maelezo hapo juu.
-Achana kabisa na kesi hiyo (kaifute), maana hata ukipewa hela na sijui ni ngapi maana kwenye mkataba sidhani kama kuna figure kamili (i.e 3M), maana hela nyingi waweza kuwa umetumia Zaidi ya prediction mliyoandika siku hiyo kwa ku-foresee
-Jipe moyo kuwa umepata hasara kama vile ulikuwa na duka na halina bima then likaungua lote
-Ni muda wa kudeal na vitu vinavyokufurahisha Zaidi tofauti na mapenzi. Usikae peke yako muda mwingi, jichanganye na washikaji zako wengine. (Usijiingize kwenye mapenzi na mtu yeyote kwa sasa mpaka baada ya muda Fulani, let say minimum of 3 months)
-Usimfuatilie yeye na familia yake kwa ujumla. Maana tayari umekiri ni mjamzito na si rahisi hata akisema anarudi leo kama nawe upo tayari kumpokea mtu mwenye mzigo wa njemba nyingine (Hii ni siraha ya kuwaumiza kisaikolojia wenyewe na nafsi zao zitasononeka japo watajikaza kisabuni kutosema kwa uwazi kwa muda, ila mwisho wataisema kwa sauti)

Mwisho, Mitihani imeumbiwa wanadamu na inastage tatu tu, (1)KUTOKEA, (2)KUIKABILI na (3)KUISHINDA/KUISHINDWA (hapa lazima kuwe na jibu moja tu). Sasa chagua KUISHINDA na maisha yatasonga.
 
kwani kinachokuuma ni mpenzi auu gharama?,kama mliweka mkataba wa kusomesha kwa malipo ya ndoa na imeshindikana,basi warudishe gharama zako,usiwe dhaifu komaa mahakamani ukilipwa moyo utatulia tulii,wanawake sio ishu hata usiposomesha mkiachana utaumia tu,ila we hilo la gharama linakuuma zaidi,dai hela zako kila mtu afe na chake,usizisamehe alaf ukikumbuka unaumia.wakulipe hela zako!!!
 

terms za mkataba ukivunjika zinasemaje? Sio kwamba refund ulishapewa in kind in advance hapo kwenye ''best sex ever''?
 
Duh! Pole mkuu. Huyo masikini kisawasawa asikusumbue. Kama kafanya hivyo basi shukuru Mungu maana ulichopoteza ni kidogo kuliko kama ungeishi nae. Huyo ni masikini kwelikweli maana hata fadhila katindikiwa. Masikini hadi rohoni. Jitahidi tu upate haki yako huko mahakamani
 
It is not the end of the world, let it go, acha utoto, unaenda mahakamani ili iweje? huko ni kujidhalilisha, kubali matokeo, endelea na maisha. kwa hiyo na wewe utarudisha utamu na raha ulizokuwa unapewa naye? Yaani ulikuwa unatumia fedha zako kuwadhalilidha masikini, umefanya ngono na binti kabla hujamuoa huko mama yake akitambua, lakini ilibidi wakubali kwasababu walikuwa hawana kitu. Mzazi gani atakubali ufanye ngono na na binti yake na afurahie!!?? Achana na hiyo kesi haraka sana then move on maisha yako
 
Hajaenda kujishitaki bana,kuna sheria inayomkataza mtu kutrmbea na mtoto wa chuo?,
 
Pole sana mkuu! Ila hizo kesi tumeshazizoea humu! Mpo wengi sana! So jua tu haupo peke yako unaelialia kusomeshwa na kutoswa! Ila watu wanayaona haya humu na hamsikii yani nyie somesheni tuu msilete tena huo ujinga humu tuwashauri
 
Achana na kesi itakuumiza zaidi,msamehe,nyamaza na sahau,chukulia tu hiyo hela uliwekeza na a haijalipa,msamaha na kukaa kimya ni adhabu tosha
 
Jukumu lako ni kuwa rafiki, boyfriend au mume kwa mwanamke.

Jukumu la kusomesha ni kwa wadogo zako na watoto wako sasa wewe ulikimbilia majukumu ambayo hayakuhusu tena usikute hapo kuna mdogo wako ulimbania ada eti unajipendekeza kumsomesha mtoto wa watu!

Hukumu hii iwe fundisho kwa wanaume wengine wenye hizi tabia mbaya katika jamii yetu!
 
Natamani nikutukane.. Mchumba hasomeshwi.. Labda kama amekuzalia.. Pumbavu kabisa.. Tuwaimbie mara ngapi? Hadi boda boda na baashinya madala dala wameandik kuwa "mchumba hasomeshwi mjombaaaa"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…