Pole sana kwa hilo ndugu.
Duniani kitu ambacho kimekuwa janga kubwa ni MAPENZI. Ulifanya kwa lengo na nia njema ila hayo ndo malipo ya malimwengu. Na Zaidi unasema mliandikishana mkataba, mmmh hapo ni ukakasi, haikutakiwa MKATABA bali NDOA. Hata sasa unasema umefungua kesi mahakamani sijui ya madai au ya mapenzi, Kitu ambacho naona unakosa haki nacho. Mkataba unaokubalika wa kuunganisha watu ni NDOA na wenye dhamana hiyo ni SERIKALI(MKUU WA WILAYA), MAPADRI, MAKASISI na MASHEKHE na wote hao hupewa kibali toka serikalini cha kufungisha ndoa na kwenye kufungisha kila mmoja wenu anaulizwa mara tatu kama karidhia hiyo ndoa mbele ya kadamnasi iliyopo pale (mashahidi), asiye na kibali hicho ndoa atakazofungisha ni batili whether SHEKHE, PADRI AU KASISI. Sasa ninyi mlichofanya kwa mkataba huo haikupi nguvu kisheria kummiliki yule, ila ingekuwa unamsomesha na rehani wameweka nyumba, kiwanja au gari mkataba utakapokengekwa ingekuwa rahisi kisheria kuzuia zile mali zilizo rehani, ila kwa mtu hapo ngumu, labda wanasheria watusaidie hapo.
Nini cha kukushauri baada ya maelezo hapo juu.
-Achana kabisa na kesi hiyo (kaifute), maana hata ukipewa hela na sijui ni ngapi maana kwenye mkataba sidhani kama kuna figure kamili (i.e 3M), maana hela nyingi waweza kuwa umetumia Zaidi ya prediction mliyoandika siku hiyo kwa ku-foresee
-Jipe moyo kuwa umepata hasara kama vile ulikuwa na duka na halina bima then likaungua lote
-Ni muda wa kudeal na vitu vinavyokufurahisha Zaidi tofauti na mapenzi. Usikae peke yako muda mwingi, jichanganye na washikaji zako wengine. (Usijiingize kwenye mapenzi na mtu yeyote kwa sasa mpaka baada ya muda Fulani, let say minimum of 3 months)
-Usimfuatilie yeye na familia yake kwa ujumla. Maana tayari umekiri ni mjamzito na si rahisi hata akisema anarudi leo kama nawe upo tayari kumpokea mtu mwenye mzigo wa njemba nyingine (Hii ni siraha ya kuwaumiza kisaikolojia wenyewe na nafsi zao zitasononeka japo watajikaza kisabuni kutosema kwa uwazi kwa muda, ila mwisho wataisema kwa sauti)
Mwisho, Mitihani imeumbiwa wanadamu na inastage tatu tu, (1)KUTOKEA, (2)KUIKABILI na (3)KUISHINDA/KUISHINDWA (hapa lazima kuwe na jibu moja tu). Sasa chagua KUISHINDA na maisha yatasonga.