Nimemsomesha, nimegharamika, leo kaniacha anaolewa na mtu mwingine

Pole sana mkuu hapa ndo naamini ule msemo unaosema Mchumba hasomeshwi. Utakuja kula sumu bure. Na kazi ya kumuaanda MKE ni ya MUNGU PEKEE ww unaanda mazingira tu piga moyo konde maisha lazima yaendelee.. Usichoke kumuomba MUNGU NI MWAMINIFU anaandaa ushuhuda wako.
 
Na am sure ulishasikia girlfriend hasomeshwi. Lakini ulipuuza. Inawezekana tatizo likawa kwako hebu jaribu kujichunguza. Angalia ni mahala gani hasa mlikuwa mnatofautiana na kwanini na wewe ulireact vipi? Ulisema nini na Ulifanya nini? Alipenda nini? Kwanini unasema alikupenda? Mapenzi yenu yalitawaliwa na nini? Nafasi pesa ilikuwaje? Alikuvumilia ktk nini na wewe ulivumilia nini?

Acha kulalama trust me haisaidii kitu sana sana unajiongezea maradhi ya Moyo. Jifunze kisha songa mbele. Hakuna anehitimu elimu dunia. ILa tunashauriwa kujifunza kutoka kwa waliotangulia kukosea. Japo tunaelewa zaidi ama kujifunza zaidi kutokana na makosa yetu wenyewe. Maana gharama tunailipa wenyewe.

Jifunze kuishi na Mwanamke kiakili. Jifunze kushinda mihemuko yako. Don't put all your Eggs in one basket.

Nakutakia kila lakheri katika kujifunza kwako. Next time uje na thread ya nini umejifunza kutokana na kosa flani ulilofanya.
 
Usitumie muda wako kufuwatilia msaliti. Fanya umetoa sadaka songa mbele utarudi kushuhudia.
 
Sasa wewe gharama za KU DO huzioni? Wewe kila siku ukiwa na hamu ulikuwa unamaliza kwa huyo Binti hadhani kwanza ulikuwa unatembea na Mwanafunzi wa Secondari na unahitaji kufungwa miaka 30 maana inavyoonekana ulitumia nafasi ya kuwa Masikini huyo Binti. Je kwa nini usingesubiri afike Chuo Kikuu ndo uanze na harakati za kuoa?. Ushauri wangu, achana na hizo Pesa, tafuta maisha mengine. Watu wanaosomesha wachumba wengi hawajiamini, matokeo yake ndo hayo. Kwa kifupi, Mchumba hasomeshwi bali hupewa fedha za Snap Chips,Bager,Azam Juice,Nguo,Kusuka,au shopping. Hayo menyewe niliyoyataja ni zaidi ya kusomesha sasa uanze kusomesha Chuo atakutana na watu wanamkuna kwelikweli na wewe ulikuwa unagusa kisitaarabu!!!!!!!!!!!
 
Ndugu kama una amini katika Mungu samehe tu inabidi usamehe hili mambo yako mengine yakae sawa nakuhakikishia atakukumbuka sana Na ipo siku ataumia zaidi yako wewe ulivyoumia kila kitu anapanga Mungu Mungu kakutumia wewe kama daraja la yeye kufika mbali katika elimu Yake kama kapostpond muuombee Mungu amalizie awe msada kwa familia Yake achana Na mambo ya mahakamani Mungu kukuepusha Na mengi hawa ndio wale ukaja Kuoa aoni tabu kukuua kisa afanye mambo Yake kwa amani
 
Nadhani tatizo hasa lipo kwenye tafsiri. How do we define our happiness. Wapo ninao wafahamu ambao wameachana na wake zao waliozaa nao watoto and they are Okay with a different life style. Sio wanaume wote tutajaaliwa kuoa au kuwa na Familia. Maisha hayana guarantee anything can happen any time. It is somehow better to be prepared for the wost psychologically.

Haya Mambo yanaumiza sana. Na hakuna master. Jambo la Msingi ni kuomba Mungu kisha unasonga mbele.
 
Pole sana kaka, umeandika kwa uchungu kweli najua inavyouma lkn hakuna namna cha msingi jitahidi kuvumilia achana na hiyo kesi ya kudai gharama zako kaa kimya wanawake wapo wengi sana cha msingi achana na habari ya kubeba jukumu la mzazi next time maana unashindwa kuelewa kuwa je umependwa kwa dhati au umependwa coz ya msaada wako.

Pole sana, achana naye anza upya.
 
Pole sana mkuu...ila hata na wewe ulikosea toka mwanzo ~ungemtia mimba kwanza ili hata kama angebadilika kama hii leo ungekuwa na kafaida japo kidogo
 
Mkuu pole. Alikuwa anasoma chuo cha mji gani? Isije kuwa DSM?
 
Tatizo wanaonyesha kiburi hata mahakamani hawakanyagi. Na barua walipelekewa.Kusamehe nashindwa mkuu wangu.

Asante pia
Unashindwa vp kusamehe, hili ni jaribu kwako na unapaswa ulishinde ushasema mwenyewe kuwa hiyo familia ni maskini sasa unategemea kipindi hiki ndio wamekuwa matajiri wa kuweza kulipa gharama zako? misukosuko km hii ndio ukomavu wako kimahusiano, watu wanaacha asset km nyumba, gari na vitu vingine na kuanza maisha mapya sembuse hiyo ada na matumizi ambayo hata million 10 haifiki, hasara roho ndugu yangu, pesa makaratasi tu.
 
Mmhhh, pole sana mkuu hawa viumbe ndo walivyo ni wa ajabu sana hawana utu wanatanguliza tamaa mbele ila nadhani itakuwa fundisho kwa wengine
 
Kitu nilichojifunza;
1. Mchumba hasomeshwi.
2. Mchumba hakopeshwi hela.
3. Mchumba anunuliwi wala kupewa vitu vya thamani.
 
Mkuu nakushauri ukubaliane na matokeo, kubali kuachwa ama kutendwa na mtu uliyempenda kwa moyo wote, akili yote na the one whom you had sacrificed you whole body, love, heart and money to.
Achana na kesi hiyo itakupotezea muda tu na hela ndugu.
Madem hawa tulioumbiwa hawajitambui ndio maana hata maandiko matakatifu yanatuambia "ishini kwa akili sana na wanawake" fumbo ambalo mme hulifumbua tu punde aingiapo mgogoro na mke wake ampendae.
Pole sana mkuu, I know how much painful it's when you see your beloved one going away with her hand in the hand of another guy in the name of love. I'm the victim of such unbelievable breakup and taking a lover to school, taking care of her entire family. Pole sana mkuu, utapata mwingine don't worry.
 
pole sana mkuu kwa yaliyokukuta kwani hawa viumbe ni hatari sana na wakiamua kufanya ktu hawogopi na wala hawajali na hawafikiri nyuma na sijui wanatumia kiungo gani kufikiria.cha kukushauri ni kwmba ktk kpndi hki kigumu jitahid kutokaa peke yako maana kufanya hvyo kunaweza kukuletea mawazo mabaya ni bora ujichanganye tu kwa marafik mkpga stori mbili tatu ,pia hata ukimshtaki sidhani kama atakuwa na mkwanja wa kukulipa cha msingi ni kumwachia mungu tu ,sku hzi malipo ni hapa hapa duniani tukifa znaendA hesabu tu.
 
Mtu masikini si mtu wa kumwamini hata kidogo
Masikini ndo wanatuumiza sana, nimesomesha, nimelisha familia ya demu wangu nikitegemea kuja kumuoa ila ile anamalizia tu kozi yake nikaambiwa piga gharama zako unadai shiling ngapi nikulipe... Aiseee ndani joto lilipanda kwa nyuzi 40 kidogo nife na hadi hapa bado unauguza majeraha moyoni japokuwa unaelekea mwezi sasa (bado siku 4 tu mwezi ukamilike).
MCHUMBA HASOMESHWI
 
Wewe shukuru amesepa mapema ungeoa labda angekuletea ukimwi. Kuhusu kusomesha ichukulie kama hasara kwenye business.
 
Wakuu asanteni sana kwa maoni na ushauri wenu... nazidi kusoma na ninaamini nitaendelea kujifunza mengi kutoka kwenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…