Nimemsomesha, nimegharamika, leo kaniacha anaolewa na mtu mwingine

Nimemsomesha, nimegharamika, leo kaniacha anaolewa na mtu mwingine

Hukufanya investment risk calculations,

Ulipaswa kuhakikisha hiyo "best sex ever" anaitamka yeye.

Umeleweshwa na mkatiko ya kiuno chake kumbe mwnzio ile ndiyo atm card ya ku draw pesa zako!!! hukuangalia kama huwa unampotezea network kunako 6x6 (unapiga goli/magoli ya ufundi mpaka goli linamlazimisha kulala huku viungo vyake vimepoteana)

Unayo faraja moja iliyobaki nayo imebebwa na muda!!!!

Likuepukalo lina heri kwako. (ni bora uyaelewe maneno haya.

Next time ujue kuwa mwanamke hufelishwa na dushe!!!!! Hafelishwi na pesa.
 
Sipendi kusikia ujinga kama wa mtoa, bado wajinga wengine watafanya ujinga ule ule!
 
Pole ungekuwa msomaji haswa humu ungekuta umeshasomaga yaliyowapata wanaume wengine haya haya mambo na watu walivyochangia.

Pole sana, wewe sasa waache waende zao. Mungu atakulipia kwa maumivu uliyoyapata na akirudi ukamchukua tena shauri yako atakuacha hata kazi huna.

Waache waache acha kuwapigia simu, ongea na Mungu akusaidie upunguze hasira na chuki kwao itayaona.

Huyo mama mkwe ndie alimuonya aendelee nawe uzidi kumsaidia, ungejua ungeachia wakati ule sababu dalili zilianza ila ndio maisha ya mapenzi.

Pia mshukuru Mungu labda kakuepusha na makubwa zaidi ya hayo labda hata magonjwa na maumivu makubwa ambayo angekupa.
 
Sikujua laiti ningejua.... Najuta

Wakuu nilikutana na huyu binti miaka kadhaa iliyopita mimi nikiwa nimepangiwa kazi mkoa fulani... katika mihangaiko yangu nikakutana na huyu binti nilitokea kumpenda.. mzuri kisura na kitabia...very innocent niliamini kwake nimefika baada ya kash kash nilizopitia katika mahusiano ya nyuma.

Wanasema usiusemee moyo ila najua yule binti alinipenda kidhati tena moyoni kabisa.. na mimi kwangu she was a queen na niliapa kumuoa baada ya yeye kumaliza masomo yake. Binti huyu kwao ni familia maskini nikisema familia maskini ni familia maskini kisawasawa. Baba yake alifariki miaka kadhaa nyuma kabla sijaonana nae hivyo aliishi na mama yake na wadogo zake.. ni story ndefu kuhusu familia yao. Mimi nikawa ndio kama msaada katika familia yao, sikua na hiyana na nilisaidia niwezavyo kwani binti yule nilimpenda kutoka moyoni.

Yule binti alimaliza shule na kuhitajika kwenda chuo lakini familia ikawa haina uwezo wa kumsomesha na mkopo alikosa. Akakosa raha na ikawa kama jukumu ni langu. Mama yake aliniita tushauriane kwasababu kwao nilikua nafahamika. Kwakuwa mimi nilisema nitamuoa binti wakashauri nimsomeshe kama nina nia yakweli. Uwezo wa kumsomesha nilikua nao nikakubaliana na tukaandikishana kwamba namsomesha mimi lakini mwisho wa siku yeye atakuja kuwa mke wangu na hata mahari sintolipa kwani itakua imeingia huko. Familia ilinishukuru sana kwani waliamini kusoma kwa binti itakua afadhali katika ukombozi wa maisha yao. Binti alikuwepo wakati maandikishano yanafanyika na mashahidi walikuwepo.. nakumbuka binti alilia yule akiapa kunipenda milele na mapenzi tuliyofanya siku hiyo siwezi kusahau... ilikua best sex ever.

Wakuu nifupishe binti alianza chuo kila kitu nililipa.. Nauli.. hosteli ada matumizi kila kitu ilikua mimi ,mwaka wa kwanza ukaisha vizuri mapenzi yanachanua.. likizo naenda likizo zao anakuja.. mama mtu alinishukuru sana. Mwaka. Mwaka wa pili matatizo yakaanza nikipiga sim naambiwa yuko library.mara assignment nikiuliza zaidi anakua mkali nikasema labda labda kweli shule lakini hata mimi nilisoma muda wa kuongea na mwenzi wangu nilikua nao nikasema labda shule ya sasa ni ngumu. Binti akabadilika majibu ya jeuri nikaenda kuongea na mama yake amkanye naona akajirekebishe na kweli akatulia maisha yakaendelea. Upside zikiwa chache. Mahusiano yalitawaliwa na migororo

kufupisha...Miezi kadhaa imepita binti kaniandikia meseji eti "NAKUSHAURI UTAFUTE MWANAMKE MWINGINE MIMI SIKO TAYARI KUWA NA WEWE NIKUTAKIE MAISHA MEMA"

Naandika huu uzi wakuu acha nikipiga simu haipokelewi mara haipatikani. Nikampigia mama yake kumuuliza kama anajua lolote akasema hafaham. Nikaomba likizo kazini nifatilie sikuamini siku naambiwa ana mimba na anaishi na mwanaume mwingine. nilitamani ardhi ipasuke kumbe ndio maana niliandikiwa ule ujumbe nikajiuliza maswali bila majibu... basi angefanya nisijue na mimba juu kapata inauma sana. Kumuuliza mama yake hana analonijibu, kumbe chuo kapostpone sijui anaishi na huyo mwanaume moja ya mitaa Dar.. yote hiyo nafatilia kwa baadhi ya marafiki zake. na kibaya zaidi huyo mwanaume alishamlipa tena huyo mama pesa nyingine. Na ndio kamchukua binti yake.

Nimechukia kuuziwa mbuzi kwa gunia.. Love is blind inakuwaje sikuona yote hayo?? Why me..Why.. najiuliza sipati majibu. sikuwahi kupenda kama nilivyompenda huyo binti. Nilimpenda kutoka moyoni na kujitoa kwake sijawahi kumfanyia mwanamke yoyote niliyomfanyia leo ameniacha kwenye mataa na nyodo juu.. kuna muda natamani ningekua na bastola nimsambaratishe ila that is not me. Juzi nimeona whatsup kaweka picha yake tumbo kule na namba yake nikafuta

NILICHOFANYA

Nimepeleka hii kesi mahakamani kwasababu tuliandikishana kama mke nimekosa basi nilipwe gharama zangu najua haiwezi kuziba pengo.. kufuta maumivu naona is the least i can do for my self... wakuu nifanyaje au nimekosea kupeleka shtaka polisi tumeshaitwa mara mbili hakuna mtu aliyetokea upande wao . Nimetokea kuwachukia wanawake saaaana... kwanini mnatufanyia hivi jamani tuwapende vipi. Nimekaa hapa kitandani nimewaza mawazo mengi moyo wangu kama barafu naishia kusononeka.

Sijui nimfanyie kisasi gani aumie kama mimi nilivyoumia.

Adios.

Pole san mkuu ila at very start huyu demu ulitakiwa mfunge ndoa na mimba juu alafu ndo aende shule hata kama siku angekuja kukubadilikia lakin una damu yako ingekuwa mkombozi siku za mbelen Pole sana Mkuu Mchumba Hasomeshwi yan katika 100 mmoja ndo anauwezo wa kuvumilia tena inategemea
 
Pole mkuu.

Hizi mbinu zipo kitambo sasa.

Huyo binti na mama yake waliona udhaifu wako na wakautumia vizuri hivyo wako sahihi.

Na wewe ulimpenda huyo binti yao lakini ukashindwa kutumia nafasi hiyo kumuoa huyo binti, hivyo wewe ndie uliecheza pata potea.

Ni kosa la kiufundi tu lakini binadamu tunajifunza kutokana na makosa.

Huwezi kufanikiwa kwa kwenda mahakamani kudai fedha zako za matunzo na ada ya chuo, kwani kisheria mkataba mliowekeana na huyo architech ambae ni mama wa huyo binti ni batili na hauna nguvu kisheria.

Sahau yaliyopita, pata muda ujichanganye na marafiki zako, pitia JF ukipata nafasi usome mada zetu za kufikirisha na za kuchekesha, pata bia mbili tatu lakini usilewe, chapa kazi, jenga taifa.

Atatokea tu binti mwingine na Mungu atakuelekeza- kwa sala na maombi.
 
Umejidhalilisha zaidi kupeleka shtaka mahakamani. Nashauri kaa kimya. Usimtafute mama yake wala yeye wala ndugu yake.

Unajua Mungu siku zote hakosei. Huyo mwanamke pengine angakuja kuwa tanzi kwako na kukupotezea maisha kabisa. Mshukuru Mungu kuwa kuna kitu amekuepushia huko mbeleni badala ya kulaumu.

Kaa kimya, kama ni mtu wa maombi fanya maombi sana, soma sana neno la Mungu ili Roho wa Mungu akutawale. Najua kipindi kama hiki ndo kipindi ambacho ibilisi huvizia na kumvaa mtu vizuri na unaweza kufanya jambo ambalo utalijutia maisha yako yote. Ukiwa mwenyewe fanya maombi sana na kusoma neno la Mungu usiruhusu nafasi hata kidogo ya ibilisi kuingia ndani yako.

Ukimya wako ndo utamuumiza sana yeye binafsi na familia yake. Ila ukilipiza kisasi tu ndo utakuwa umeharibu kabisa. Mwache aendelee na maisha yake braza. Mbona wanawake wamejaa teleee🙁

Mungu atakulipia yeye mwenyewe na hutaamini kuna siku atakukumbuka tena sana tu na itakuwa too late kuurudisha moyo wako. Jikungute songa mbele boss. Mwanaume wa ukweli hakati tamaaa kirahisi so far una nguvu, u mzima, hajakunyanganya akili yako, maisha yanasonga tuu. Kwani ulizaliwa naye? Mmekutana tu ukubwani.

ONYO: ACHANA NA TABIA KUSOMESHA MWANAMKE ATI AWE MKEO. KAMA UNAMSOMESHA MSAIDIE TU KAMA MSAMARIA MWEMA ILA ACHANA NA MAWAZO YA KUTAKE ADVANTAGE YA KUOA.KAMA ITATOKEA MBELE YA SAFARI POA; ISIPOTOKEA POA!!
Wewe jamaa unashauri vizuri sana...mdau akiuzingatia ushauri wako ataishi vizuri sana! PURE GENIUS...
 
Kumpa mimba au kumzalisha is not a solution, jamaa yangu aliachwa asubuhi saa kumi na mbili....!!

Demu kamusomesha,mwaka wa pili akamchapa mimba,demu kazaa,mwaka wa tatu wakafunga ndoa,demu karudi chuo last semester,yakaanza manyau nyau,mchizi kapigwa chini,Mtoto kapewa,demu kaolewa na jamaa mwingine...

Jamaa alikonda sana,msongo wa mawazo ukawa unamkondesha balaa,akahama na kanisa,kutoka Roman Catholic hadi now anasali kwa Kakobe....
Bora kapewa damu yake! Mimi kama umenipa damu yangu...sijiulizi mara mbili, kukusahau ni fasta! Wanawake wengi sana mtaani wako mawindo...sampuli tofautitofauti!!!
 
Pole sana ndugu yangu. Kama nimekuekewa vizuri unaomba ushauri wakati tayari umeishafanya maamuzi kwa kwenda mahakamani.

Mimi ningekushauri piga moyo konde uachane na hayo mambo yasikupotezee muda Mwenyezi Mungu atakulipia tu , tuombe uzima na afya njema ipo siku utatujuza yatakayomkuta malipo ni hapa hapa duniani.
 
Ni kweli kabisa dada.ile ilikua mistake kubwa kubwa sana. Nawaza hizo pesa ningetoa hata msaada kwa watoto yatima au ndugu zangu wenye shida. Najuta najuta sana
Wengine tulifikiri kama hivi . Shukuru Mungu endelea na maisha
 
Sielewi hawa watu wana nini wakati mwingine. Kuna mmoja alikuwa akiishi na bwana na jamaa kampatia usafiri awe anatumia na kumfungulia biashara ya nguo ili awe busy. Kutokana na kujiona kapanda class na ushamba wa kumiliki gari,plus mashosti feki kumpampu,akaanza kujirusha na vitoto vya chuo mixer wajanja wa mjini. Jamaa kamkalisha chini na kumwonya lakini mwanamke hataki kusikia na kujifanya anajua sana kutukana.
Jamaa alipoona yamemshinda,akamwambia amenawa mikono,kila mtu kivyake,akamwachia biashara,gari akalichukua. Cha kushangaza,mwanamke anang'ang'ania na gari akidai ni lake mara eti walichuma pamoja na bla blah nyingi. Na asivyo na akili akadanganyika mpaka kutafuta wakili ili shauri liende mahakamani apewe gari wakati ni girlfriend tu aliepewa alitumie bila ties zozote. Inaudhi sana.
 
Back
Top Bottom